2025.04.28 Giacomo Mattivi alipokutana na Papa Francisko. 2025.04.28 Giacomo Mattivi alipokutana na Papa Francisko. 

Giacomo Mattivi:Papa katika ugonjwa hakutengana na ukaribu kwa kila mtu

Katika siku za Jubilei ya watu wenye ulemavu mwanafunzi mdogo anayetembea kwenye kiti cha magurudumu kutokana na ugonjwa wa vinasaba,amekumbuka mikutano yake na Papa Fransisko na maneno ya Baba Mtakatifu kuhusu ulemavu,neno ambalo hakulipenda.

Na Fabio Colagrande na Angella Rwezaula – Vatican.

Tukia katika siku ambazo bado ni za maombolezo ya kifo cha Baba Mtakatifu Francisko, walemavu waliitwa kupita chini ya Mlango Mtakatifu mjini Vatican kwa ajili ya Jubilei hiyo maalumu kwa ajili yao. Giacomo Mattivi mwenye umri wa miaka ishirini na mbili, katekista na mwanafunzi wa sosholojia, akitumia kiti cha magurudumu kwa sababu ya ugonjwa wa "Duchenne muscular dystrophy", tayari ni mhusika mkuu wa filamu ya hali halisi, "Green lava", iliyoongozwa na Lia Beltrami, na  podikasti ya Radio Vatican - Vatican News, alitazama matukio haya ya kikanisa katika jimbo la nyumbani la Trentoga, lakini akiwa huko Trentoga alihisi ukaribu kiroho na Roma.

Giacomo Mattivi
Giacomo Mattivi

Umuhimu wa ishara

Wazo lake la kwanza ni kumbukumbu ya kibinafsi ya Papa ambaye alikutana naye, mara ya mwisho mnamo Januari 2025, na ambaye alikuwa amebadilishana naye barua kwa muda mfupi. "Nilivutiwa na nguvu ya kujieleza ya macho yake," alisema. "Nilipokutana naye kwa mara ya kwanza hatukubadilishana maneno mengi, lakini kugusa kwa mkono, tabasamu na kutazamana machoni kwa kila mmoja kwa dakika chache kulitosha. Ishara hiyo ilikuwa zaidi ya hotuba nyingi."

'Papa Francisko alikuwa na uwezo huo wa kusikiliza'

Akiwa kijana aliyejihusisha na ukuzaji wa kijamii katika nyanja ya Kikatoliki na Chama cha “Shemà”, lililoundwa na wazazi wake, na katika kazi ya kichungaji na jumuiya yake, Giacomo alivutiwa na mambo mengi ya Upapa huu. “Kwanza kabisa,” yeye alikiri, “uhakika wa kwamba alichagua jina la Mtakatifu aliyebadili kihalisi njia ya kuishi Ukristo ulinifanya nifikirie.” "Kisha, nilivutiwa na unyenyekevu wake: kukataa kwake kuishi katika vyumba vya Jumba la kitume, kumbukumbu yake ya mara kwa mara ya mizizi yake na matumizi yake ya gari ndogo kuzunguka Roma". "Nilimpenda Papa Francisko - Giacomo alielezea - ​​kwa sababu alikuwa mtu ambaye hana barakoa.

Alipotaka kuonesha kutokubali, hakuficha usemi wa upinzani. Wakati mwingine alijua jinsi ya kuwasiliana, hata kwa ukali, ukweli waukweli, hata wakati wa kushughulikia watu muhimu." "Lakini wakati huo huo - aliongeza - nilivutiwa na uwezo wake wa kusimama na kusikiliza kila ombi ambalo lilishughulikiwa kwake. Uchongaji wake wa mara kwa mara nje ya wakati wa kusoma barua ambazo alitumwa kwake." "Kumbukumbu iliyo wazi sana katika kichwa changu - aliongeza Giacomo - ni uzinduzi, mwaka  2017 na 2019, mashine za kufulia nguo na bafu zilizoanzishwa na Papa Francis kwa wasio na makazi jijini Roma. Na kisha umakini wake kwa suala la wakimbizi, ambao kwa bahati mbaya hupoteza maisha kila siku kwa kuzama baharini huku wakitegemea safari za hatari sana za matumaini”. Licha ya ugonjwa na kufiwa kaka yake Mattia, Giaccoma alijua kubadilisha matuatizo yake katika kuuisha usanii.

Giacomo Mattivi
Giacomo Mattivi

'Nilihisi huruma kwake'

Giacomo alizaliwa na ugonjwa wa maumbile unaoendelea ambao husababisha udhaifu wa  misuli, ugonjwa adimu ambao pia uliathiri kaka yake Mattia, ambaye alikufa mnamo Januari 2022 kutokana na matokeo ya ugonjwa huo. Lakini badala ya kujifungia katika maumivu yake mwenyewe, kwa msaada wa familia yake na marafiki, alipata nguvu ya kubadilisha mateso kuwa upendo kwa wengine na ulemavu wake katika nguvu ya ubunifu, kuandika mashairi na kutengeneza filamu. Kama wengi, alifuata siku za ugonjwa wa Papa kwa wasiwasi na hisia. "Ilinipa hisia kubwa ya huruma kumuona kama mzee anayekaribia mwisho". Giacomo aliendelea kusema "Francesco aliishi maisha yake kwa ukamilifu, kuwa mjenzi wa amani, alihubiri msamaha na tahadhari kwa angalau, na  alipendelea kuishi hata siku ngumu zaidi kwa ukamilifu, kuwa karibu na watu na kufanya kile anachopenda sana. Hii ilinikumbusha juu ya kaka yangu, ambaye alifariki miaka michache iliyopita, ambaye alipenda kufurahia furaha ndogo za kila siku.".

'Unajifunza zaidi kutokana na kile ambacho hakifanyi kazi'

Papa Fransisko mara nyingi ametumia maneno makali na yaliyo wazi anaposhughulikia suala la ulemavu na huduma ya kichungaji inayoihusu. Giacomo Mattivi, aliyezoea kuishi na mashine ya kupumua kwenye kiti cha magurudumu, ana maono wazi juu ya somo hilo. "Katika Mkutano wa Mataifa yaliyoendelea kiviwanda (G7) juu ya Ujumuishi na Ulemavu, Oktoba iliyopita, Papa alitumia maneno makali sana kujieleza juu ya dhana ya ulemavu." "Aliomba kujumuishwa, lakini pia huduma za kutosha, ambazo hazimaanishi ustawi, lakini haki na heshima kwa utu wetu." Na tena - Giacomo alisisitiza  kuwa hakupenda neno 'ulemavu' sana, lakini alipendelea 'uwezo tofauti'. Kila binadamu - Giacomo anaonesha - kwa maoni yangu ana talanta yake mwenyewe ya kugundua na kuweka katika huduma ya wengine." "Mara nyingi, watu wanaokuja dhidi ya vikwazo hufanikiwa kuvishinda na kutafuta njia mbadala za kuishi maisha yao. Unajifunza mengi kutoka kwa vitu ambavyo havifanyi kazi inavyopaswa, kuliko kutoka kwa vitu vinavyofanya kazi vizuri," alisema kwa urahisi na kwa busara

"Asante, Francisko!"

Mnamo Oktoba 2024, Giacomo Mattivi, baada ya kutuma moja ya mashairi yake kwa Papa, alipata mshangao usiotarajiwa: "Papa alinitumia barua. Na kilichonivutia zaidi ni jinsi alivyohitimisha, akitia sahihi 'kidugu', Francisko.  Kwa bahati mbaya - aliongeza - mtu anaelewa bahati ya kukutana na mfu fulani wakati umechelewa. Lakini nitajitolea kushirikisha uzoefu huu mzuri na wengine. Asante sana, Francisko!"

Makardinali kwa hiyo kutoka Ulimwenguni wako tayari na watamchagua Papa Mpya kuliongoza Kanisa.

Makardinali watakaomchagua mpya
Makardinali watakaomchagua mpya   (ANSA)
30 Aprili 2025, 12:33