2025.04.28 Kikanisa cha Sistina mahali ambapo mkutano mkuu wa uchaguzi utafanyika. 2025.04.28 Kikanisa cha Sistina mahali ambapo mkutano mkuu wa uchaguzi utafanyika. 

Kutoka maeneo,umri,watawa:ni makardinali watakaomchagua Papa mpya

Makardinali ambao kuanzia tarehe 7 Mei wataungana pamoja kumchagua Papa mpya wanatoka nchi 71 tofauti.Idadi kubwa ni kutoka Ulaya(53).Aliye kijana zaidi wa Australia,Mikola Bychok,kwa umri wa miaka 45 na mzee zaidi ni mhispania Carlos Osoro Sierra(79).Kwa mara ya kwanza Kikanisa cha Sisistina kitawakilishwa na chini 13 zenye wapiga kura wa Asilia miongoni mwao ni kutoka Haiti,Capo Verde,Papua New Guinea,Sweden,Lussemburg na Sudan Kusini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ulimwengu mzima kwa sasa ni kutazama kile ambacho kitatokea hivi karibuni katika mji wa Vatican, mara baada ya kifo cha Baba Mtakatifu Francisko, kilichotokea tarehe 21 Aprili 2025. Kufuatia na tukio hilo, lazima kumchagua mrithi wake kwa makardinali wapiga kura 135. Kufuatia na makardinali wawili kutoshiriki, kwa hiyo watakaoingia kwenye Mkutano mkuu wa kuchagua Papa wa 267, watakuwa 133 wanaotoka katika nchi 71 tofauti katika mabara matano. Yanayowakilishwa ma makardinali wa mataifa 17 kutoka Afrika, mataifa 15 kutoka Amerika, mataifa 17 kutoka Asia, mataifa 18 kutoka Ulaya na mataifa 4 kutoka Oceania.

Makardinali kutoka ulimwenguni
Makardinali kutoka ulimwenguni   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kwa mara ya kwanza, makardinali  15 wapiga kura ni wa asilia, kutoka upande mmoja wa sayari hadi mwingine hawa ni: Kardinali Chibly Langlois kutoka Haiti, Arlindo Furtado Gomes kutoka Cape Verde, Dieudonné Nzapalainga kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, John Ribat kutoka Papua New Guinea, kutoka Malesia Sebastian Francis, Kutoka Sweeden, Anders Arborelius, kutoka Lussemburgo, Jean-Claude Hollerich, kutoka Timor ya Mashariki, Virgilio do Carmo da Silva, Myanmar Charles Maungo Bo, kutoka Singapore - William Seng Chye Goh, kutoka Paraguay - Adalberto Martínez Flores, kutoka  Sudan Kusini - Stephen Ameyu Martin Mulla na kutoka Serbia - Ladislav Nemet, Rwanda Antoine Kambanda, Tonga- Soane Patita Pain Mafi. Katika Kikanisa cha Sistina watakuwapo makardinali 53 wa Ulaya, 37 Amerika (kaskazini 16 , Kati 4 na Kusini 17), 23 kutoka Asia , 18 Afrika, na 4 wa bara la Oceania.

Mkutano wa makardinali mjini Vatican
Mkutano wa makardinali mjini Vatican   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Wapiga kura walioundwa na Mapapa watatu wa mwisho

Mpiga kura mdogo kabisa ni kardinali wa Australia Mikola Bychok, mwenye umri wa miaka 45, na mwenye umri zaidi ni Mhispania Carlos Osoro Sierra, mwenye umri wa miaka 79. Walio wengi zaidi ni wale waliozaliwa mwaka 1947, ambapo kuna 13 kati yao kati ya wale ambao watapiga kura, wana umri wa miaka 78 au wanatarajia kutimiza. Ni Kardinali Baldo Reina pekee aliyezaliwa mwaka 1970, ambaye atafikisha miaka 55 mnamo tarehe 26 Novemba. Na hata Makardinali Leo Frank, aliyezaliwa mwaka 1971, na Rolandas Makrickas, aliyezaliwa mwaka 1972, hawana watu wa rika moja. Wapiga kura katika mkutano huo kuna makardinali 5 walioundwa na Mtakatifu Yohane Paulo II. Mfaransa Philippe Barbarin, Mcroatia Josip Bozanić, kutoka Bosnia na Herzegovina Vinco Pulić na kutoka Ghana Peter Turkson. Kinyume chake kuna wapiga kura 22  waliopokea kofia ya ukardinali mikononi mwa Papa Benedikto XVI na 108 ni wale ambao walipewa mikononi mwa Papa Francisko.

Makardinali watawa wa mashirika

Katika kundi hilo la makardinali wapiga kura ni pamoja na makardinali 33 kutoka familia 18 za kitawa; Wasalesia ndio wengi zaidi: 5 (Charles Maung Bo, Virgilio Do Carmo da Silva, Ángel Fernández Artime, Cristóbal López Romero, Daniel Sturla Berhouet). Makardinali 4 kutoka katika Shirika la Ndugu Wadogo wafransiskani OFM: (Luis Cabrera Herrera, Pierbattista Pizzaballa, Jaime Spengler na Leonardo Steiner) na Wajesuit: (Stephen Chow Sau-yan, Micheal Czerny, Jean-Claude Höllerich na Ángel Rossi), huku Wafransiskani waconventuali ni 3( François-Xavier Bustillo, Mauro Gambetti na Dominique Mathieu).

Katika Kikanisa cha Sistine watapiga kurazao hata watawa 2 wa shirika la  Mkombozi (Redentorist)ambao ni (Mykola Bychok na Joseph Tobin) na Waverbite  wa 2 (Tarcisio Kikuchu na Ladislav Nemet) pia watapiga kura yao, pamoja  Magostiniani, Robert Prevost, Mkapuchini Fridolin Ambongo Besungu, Mkarmelite peku, Anders  Arborelius, mcistercense Orani João Tempesta, Mclarettian Vicente Bokalic Iglic, Gérald Lacroix  wa Taasisi ya kidunia ya Pio X, Mazalist Berhaneyesus Demerew Souraphiel, Mmisionari wa consolata Giorgio Marengo, Mmisionari wa Moyo Mtakatifu wa Yesu John Ribat,  Mscabriani Fabio Baggio  na Msipiritani Dieudonné Nzapalainga.

Kuingia ukumbi wa Sinodi
Kuingia ukumbi wa Sinodi   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Gombo la Kanoni ya Kanuni ya Sheria za Kanisa inasema nini

Gombo la  349 la Kanoni za Sheria za Kanisa inabainisha kwamba makardinali "wanaunda Baraza maalum ambalo kazi yake ni kuandaa uchaguzi wa Papa wa Roma,” na inaongeza kwamba makardinali "wanamsaidia" Papa "kwa kufanya kazi kwa pamoja wakati wanaitwa pamoja ili kushughulikia mambo muhimu zaidi na kama watu binafsi, katika shughuli  mbalimbali zinazofanyika, huku wakifunika kazi yao katika huduma, hasa kila siku, kwa Kanisa la Ulimwenguni." Katiba ya Kitume ya Universi Dominici Gregis kisha inathibitisha kwamba makardinali wanaomchagua Mrithi wa Petro, kabla ya siku ya kifo cha Papa "au siku ambayo Kiti cha Kitume kinakuwa wazi," hawajafikisha umri wa miaka 80, ndio wanaomchagua Mrithi wa Petro, kwa sababu hiyo wanatofautishwa kati ya makardinali wapiga kura na wasio wapiga kura. Hadi sasa, Baraza la Makardinali linaundwa na jumla ya makardinali 252, kati yao 135 ni wapiga kura na 117 ni wasio wapiga kura.

Ukumbi wa Sinodi
Ukumbi wa Sinodi   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)
Ushuhuda Papa Francisko
29 Aprili 2025, 10:52