"Nyuso za Injili",Papa anazungumza kuhusu Thomasi
Vatican News
Katika sehemu ya nane kati ya 18 zinazounda "Nyuso za Injili", iliyopendekezwa tena na Vatican News katika kipindi hiki cha Pasaka, inaakisi sura ya Thomasi, mtume ambaye ana shaka."Mtu mkaidi lakini pia mfuasi wa kwanza aliyemwabudu mwana wa Mungu. Bwana alichukulia kutokuamini kwake ili kuthibitisha umungu wake. Kwa hiyo ni majeraha yanayotengeneza njia ya kukutana na Yesu." Hivi ndivyo Papa Francisko alisimulia baadhi ya matukio ya Yesu katika kipindi, kilichotangazwa wakati wa Dominika ya Pasaka 2022 kwenye Rai1, kipindi kilichosimamiwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa ushirikiano na Maktaba ya Kitume ya Vatican, Makumbusho ya Vatican na Rai Utamaduni. Waandishi wa mfululizo wa vipindi hivi ni Andrea Tornielli na Lucio Brunelli, picha zilipigwa na Renato Cerisola, Muziki asili liandaliwa na Michelangelo Palmacci.