Pasaka na imani rahisi ya wavuvi
Andrea Tornielli
Javier Cercas aliandika riwaya yake yote ya historia za kweli yenye kurasa mia tano: Uchichaa wa Mungu mwishoni mwa Ulimwengu, iliyojikita juu ya safari ya Papa Francisko kwenda Mongolia, ambayo ikiwa karibu na swali moja kuhusu ufufuko wa mwili. Yeye, mwandishi wa riwaya hiyo, ambaye alikuwa haamini kwamba Mungu yupo na asiyeamini dini, alichochewa na tendo la upendo kwa mama yake mgonjwa na uhakika ambao alikuwa ameonesha kwamba angemwona mume wake, tena mbinguni ambaye alikuwa amekufa kwa miaka mingi. Msomaji lazima afanye safari ndefu na ya kusisimua kabla ya kuwasili, kama katika mwisho unaosubiriwa kwa muda mrefu wa riwaya ya upelelezi, kwenye jibu. Tuko katika mkesha wa siku tatu muhimu zaidi kwa Wakristo ulimwenguni kote, ambapo tunakumbuka tukio ambalo liko kwenye asili ya imani yetu: mateso, kifo na ufufuko wa Yesu wa Nazareti ambayo ilitokea karibu mwaka wa 30 katika wilaya ya mbali na kandoni mwa Dola ya Kirumi. Ni vyema kusimama na kutafakari, na kulifanya swali hilo kuwa letu, ili kuepuka habari za kutisha na wasiwasi mwingi kila siku unaotukengeusha kutoka kwa moyo wa tukio hilo.
Injili zinazojulikana kisheria, hazikufukiriwa tu katika meza, kwa karne baada ya waandishi wa hadithi za uwongo za ibada au na waeneza-propaganda wenye itikadi kali za , lakini zinatokana na masimulizi ya mashuhuda waliojionea: wanawakilisha habari ya mambo ya hakika, wako mbali sana na miujiza na hawasimulizi wakati wa ufufuko. Hawasimulii ni kitu gani kilitokea ndani ya kaburi ya Yosefu wa Arimataya, “aliyeazima kwa ajili ya mazishi ya Mnazareti. Wanasimulia kile tu ambacho ni cha kibinadamu kinawezekana kusimulia na ambacho kilishuhudiwa: Yule mtu, wa kipekee katika historia anajieleza “njia, Ukweli na maisha”akidai asili ya kimungu, alikuwa ametundikwa kinyama kwenye mateso ya msalabani kama mhalifu, na akafa. Mwili wake ulikuwa umewekwa kwa haraka na kuzikwa kwa haraka. Marafiki zake, kasoro mmoja Yohane, walikuwa wamemwacha peke yake juu ya Karvario, mahali ambapo waliokuwa wajasiri kati yao walikuwa wemeonekana wanawake. Kisha alfajiri siku ya tatu, wakati mitume walikuwa na hofu kubwa na wamejifungua ndani na ufunguo katika chumba cha Karamu Kuu, wanawake walikuwa wamewashtua sana kuwa: Kaburi liko wazi na Yesu yu hai. Historia ya simulizi ya mazishi, pamoja na ile ya kaburi tupu, haihojiwi tena na wanazuoni wakubwa: kwa nini mtu yeyote angezua tuhuma ya wizi wa mwili ikiwa kaburi halikuwa tupu? Lakini imani ya Maria Magdalene, ya Petro na Yohane, ya Tomaso na mitume wengine haina msingi na haijawahi kutegemea ishara, hata iwe ni fasaha vipi, za kaburi tupu na vitambaa vya kitani visivyoharibika.
Haitoshi kutokuwepo ili kutoa imani hivyo ya "kichaa" kama vile ufufuko wa mwili ambao unaweza kuguswa lakini wakati huo huo unaishi katika mwelekeo mwingine na unaweza kupita kwenye kuta. Ni kweli kwamba Yohane, akivitazama vitambaa vilivyokuwa kaburini, “aliona na kuamini”, lakini kwa asili ya imani ya wale wanaume kumi na wawili waliopotea, na katika kundi hilo dogo la wanawake waliomsaidia mama wa Yesu chini ya msalaba, kungeweza tu kuwa na uwepo wa kutisha zaidi kuliko ishara fulani. Yeye aliyekuwa amekufa na kuzikwa amefufuka tena. Wakamwona, wakazungumza naye, wakamgusa, wakala pamoja naye. Maria Magdalene na wale wanawake wengine walikuwa mashahidi wa kwanza. Kuna Big Bang (au Mlipuko Mkubwa) katika asili ya Ukristo ambao hauelezeki na kategoria za kisosholojia. Ni nini ambacho kingeweza kugeuza kikundi kidogo cha wanafunzi walioingiwa na woga na waliokatishwa tamaa kuwa watangazaji wasiochoka wa kifo na ufufuko wa Kristo, wakiwa tayari kutoa ushuhuda kwa yote waliyokuwa wameona na kufa wakiwa wafia-imani ili kueleza juu yake?
Kilichowasukuma kinashuhudiwa tangu mwanzo, katika maneno haya ya Paulo katika Barua ya kwanza kwa Wakorintho: “Kwa maana niliwatolea ninyi kama muhimu sana kile nilichopokea mimi pia: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na Maandiko, kwamba alizikwa, kwamba alifufuliwa siku ya tatu kulingana na Maandiko, na kwamba alimtokea Kefa, kisha kwa wale Thenashara. Baada ya hayo aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa wakati mmoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengine wamelala. Pia alimtokea Yakobo, kisha kwa mitume wote.” Maneno ambayo wanazuoni wanaamini hayakutoka moja kwa moja kutoka katika kalamu ya Mtume, bali yalichukuliwa kutoka kwenye mapokeo ya awali yaliyoanzia miaka ya thelathini ya karne ya kwanza ya enzi ya Ukristo. Injili, ambazo ziliandikwa baadaye, zinakubaliana kabisa na muunganisho huu wa fumbo la Pasaka. Msomi Myahudi Paula Fredriksen, profesa mstaafu wa Maandiko katika Chuo Kikuu cha Boston, aliandika hivi katika kitabu chake “Jesus of Nazareth: King of the Jews” Yesu Kristo wa Nazarth: Mfalme wa Wayahudi: “Ninajua kwamba kulingana na wao aliyechomwona ni Yesu aliyefufuliwa.
Hivi ndivyo wanafunzi wanavyosema. Ushahidi wote wa kihistoria tulionao tangu wakati huo unathibitisha imani yao kwamba ndivyo walivyoona. Sisemi kweli walimwona Yesu aliyefufuka. Sikuwepo, sijui waliona nini. Lakini kama mwanahistoria ninajua lazima wameona kitu. Imani ya wanafunzi kwamba walikuwa wamemwona Kristo mfufuka… ina misingi ya kihistoria, ukweli ambao bila shaka unajulikana kuhusu jumuiya ya kwanza baada ya kifo cha Yesu.” Raia wakati huo wa Venezia, Albino Luciani(yaani Papa Paulo VI) alibainisha katika Mahubiri ya Pasaka ya kukumbukwa ya 1973: kutoamini kwa awali, kwa hivyo, haukuwa ule wa Thomas peke yake, bali wa mitume wote, watu wenye afya njema, wenye nguvu, wa kweli, wenye mzio wa jambo lolote la kuona, ambao walijisalimisha tu mbele ya ukweli wa matukio. Kwa nyenzo kama hizo za kibinadamu pia haikuwezekana sana kuhama kutoka katika wazo la Kristo anayestahili kuhuishwa kiroho mioyoni hadi wazo la ufufukoo wa mwili kupitia tafakari na shauku. Zaidi ya hayo, badala ya shauku, baada ya kifo cha Kristo, kulikuwa na kuvunjika moyo tu kati ya mitume. Kisha hapakuwa na wakati: sio katika siku kumi na tano kwamba kundi la watu wenye nguvu, wasiozoea kubahatisha, wanaweza kubadilisha mawazo yao kwa wingi bila msaada wa ushahidi thabiti!