"Sura za Injili,"Papa asimulia kuhusu Lazaro
Vatican News.
Sehemu ya nne kayi ya 18 zinazounda "Sura za Injili", iliyopendekezwa tena na Vatican News katika Kipindi hiki cha Pasaka, inaakisi Lazaro, kaka ya Martha na Maria, ambaye Yesu alimfufua baada ya kutokwa na machozi. "Ishara ya Yesu inaonesha jinsi ambavyo nguvu ya neema ya Mungu inavyoweza kufika na kwa hiyo ni umbali gani wa uwongofu wetu unaweza kufikia." Hivi ndivyo Papa Francisko alisema, huku akisimulia baadhi ya matukio ya Yesu katika kipindi hicho, kilichotangazwa wakati wa Dominika ya Pasaka 2022 kwenye Rai Uno, (Runinga ya Matangazo na Televisheni Italia) iliyosimamiwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa ushirikiano na Maktaba ya Kitume ya Vatican, Makumbusho ya Vatican na RAI -Utamaduni. Waandishi wa mfululizo huo ni Andrea Tornielli na Lucio Brunelli, mwelekeo na upigaji picha uliratibiwa na Renato Cerisola, muziki asilia wa Michelangelo Palmacci.