Tabora,Tanzania,Kard.Rugambwa:Vyombo vya Habari vikue vikiinjilishwa!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa kuongozwa na Ujumbe wa Baba Mtakatifu wa Siku ya Hupashanaji habari Ulimwenguni ambapo Papa Francisko aliwaalika wataalam wa vyombo vya habari kupendeleza njia isiyo ya uadui ya kuwasiliana na kutoa taarifa ambazo haziuzi udanganyifu au hofu lakini zinazojua jinsi ya kutafuta na kueneza historia zinazosukana na wema kwa kuufanya ulimwengu uache kutosikia kilio cha maskini, Kardinali Protase Rugambwa alitoa ushauri wake katika fursa ya kuelekea hija ya wanahabari wakatoliki, jimbo kuu la Tabora, Tanzania, huku akiakisi zaidi ujumbe wa Baba Mtakatifu wa Siku wa 59 ya Hupashanaji Habari Ulimwenguni, uliochapishwa tarehe 24 Januari 2025, katika siku ambayo Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Francis wa Sales, Msimamizi wa Waandishi wa Vyombo vya habari. Ujumbe wa Baba Mtakatifu unaongoza na kauli Mbiu iliyotolewa katika kifungu cha Barua ya Kwanza ya Mtakatifu Petro kisemacho: “Shirikishaneni kwa upole matumaini yaliyomo moyoni mwenu(1Pt 3,15-16.”
Mawasiliano yaletayo matumaini
Kardinali Protase Rugambwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Tabora Tanzania, kwa njia hiyo alizungumza na wahusika wa vyombo vya habari Jimboni mwake mapema Juma hili, tarehe 20 Machi 2025, katika fursa ya maandalizi ya Hija yao iliyofanyika Jumamosi tarehe 22 Machi 2025, kwa kuongozwa na Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu hilo. Kati ya mambo mengi aliyotangulia kufafanua kuanzia na majisterio ya Kanisa, vile vile alijikita na suala la Mawasiliano ya kijamii. Katika hilo alisema kwamba: “tukiongozwa vile vile na ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa mwaka huu, wa Siku ya Mawasiliano, kwani ni kawaida ya kila mwaka, kuna ujumbe ambao huwa anautoa Baba Mtakatifu, ambaye amependa na anatukumbusha kweli kwamba mawasiliano yetu yawe ni mawasiliano ambayo yanakuja kujikita kwenye hilo ambalo ndilo wote tunalitazama, yaani la “matumaini.” Kumbe mawasiliano yawe ni mawasiliano ya kuleta matumaini. Ndiyo Baba Mtakatifu alisisitiza katika ujumbe wake ambao aliutoa katika siku hiyo ya Mawasiliano.” Kardinali Rugambwa, kadhalika alisisitiza huku akifafanua zaidi juu ya hilo kwamba: “Mawasiliano ambayo yanakuja kuleta matumaini na jinsi yatakavyokuja kutolewa sasa, yatolewe kabisa kwa unyenyekevu. Tunajishusha. Hatuenda juu kupampana, katika kutoa mawasiliano. Tatizo ambalo linakuja katika hao wanaokuja kufanya kazi ya kuleta mawasiliamo.”
Tutumie vyombo vyetu vikue vikiwa vinainjilishwa
Kardinali alisema kwamba: “Kwa kutumia vyombo vyetu ambavyo tunapenda vikue, lakini vikue vikiwa vinainjilishwa na kanuni zetu na taratibu zetu ambazo zinakuja kumkumba mwanadamu. Kama magazeti, yalete matumaini na yatuandikie vitu na viandikwe katika hali hiyo ya unyenyekevu, kiasi kwamba mimi ninayesoma, ninapata kweli matumaini, kwamba ni habari ambayo inakuja kunikomboa. Kama ni vyombo vingine vya uchapishaji na vyenyewe tunataka kuviinjilisha, vinachapisha nini, vinatoa nini? Nihayo hayo kama ni Radio zetu, ambazo tunazitumia kuleta mawasiliano, mimi kama ni mkatoliki, nipo kwenye Radio hiyo, ninafanya kazi ya kuleta habari mbali mbali, basi ziwe ni habari ambazo zitaleta matumaini kwa watu wote,” Alisisitiza kiongozi wa Jimbo Kuu katoliki Tabora.
Tatizo la habari za kugushi kupitia vyombo vya habari mamboleo
Mkuu Jimbo Kuu la Tabora hakuishia hapo hata kwa upande wa mwendo kasi wa vyombo vya habari mambo leo kuwa: “Leo hii tunavyo vyombo hivi, vyombo vingine kabisa, kupitia Intaneti, mnazifahamu, ambazo nimesikia za Radio “Toronto Online”, ni vingi… ambazo zamani, ilikuwa siyo rahisi, lakini siku hizi kila mmoja tu, ana simu yake, anatengeneza, namna yake ya chombo cha kuleta habari na taarifa mbali mbali, nyingine hawalipii ushuru, na bila ruhusa, wanakwenda kukamatwa kila leo. Haya ni matatizo makubwa, kwa anayetaka kutoa taarifa. Lakini basi tusiingie huko na sisi wakatoliki, ambapo tunajua kabisa kuna utu, alafu kuna kanuni hizo na taratibu, na maadili ya kikristo ambayo yanapaswa yaendane na taratibu zinazotumika. Sio kwenda na kuiba, alafu ninaanza kufanya mambo ya kurusha taarifa nyingine ambazo kinyume cha kuleta matumaini, zinakuja kuleta vilio na vifo kama nilivyosema hapo awali.” Na kumbe mwaka huu, Baba Mtakatifu amesisitiza kitu hicho.
Tujitazame kama waandishi wa habari na maskitiko kuhusu habari za uongo
Kardinali Rugambwa, aliendelea kusisitiza kwamba: “mimi ninaomba tujitazame kama waandishi wa habari, kama watangazaji na kama wasimamizi wa vyombo hivyo vya mawasiliano na kazi zetu hizo tunazifanyaje. Katika hilo alionesha masikitiko kuhusu kutangaza habari za uongo kwamba: “ Mimi ninasikitishwa sana, siyo leo tu, hata nilipokuwa nje, nilikuwa ninafutilia sana taarifa za kwetu Tanzania. Ninakumbuka, na iliniumiza sana wakati ule kabla Mhesh ambaye sasa ameondoka: Magufuli, John Pombe, aliposimama, ilikuwa inaelekea mwishoni mwishoni. Nakumbuka wakati ule walipokuwa wanarusha habari za uongo, hizo ambazo hazileti matumaini, hazileti furaha. Kuhusiana na Mhesh Mpango. Mnakumbuka hata ninyi waandishi wa habari. Ilibidi usomwe ujumbe uliotoka kwake, ambaye walikuwa wamemmaliza, wamemuua. Na siyo mara moja wanafanya kitu hicho. Na siyo yeye peke yake. Kwa kuachana na hayo ya kwetu, hata juzi juzi mmeyasikia hayo ya Baba Mtakatifu ambavyo wanataka habari hizo ambazo ni “Fake news”, habari za uongo, badala ya kuleta matumaini,” alikazia kusema Kardinali Rugambwa.
Maswali ya Kardinali Rugambwa: vyombo vya habari tuvitumieje?
Kwa upande wa Kardinali Rugambwa, katika mahojiano hayo aliongeza kusema: “alafu sasa …. Mimi sina shida na hilo, la kumtafuta huyo ni nani, anafanya hilo, lakini kinachonishangaza, ni sisi wengine ambao tungelipaswa tuzuie vitu kama hivyo, ndiyo tunakuwa wa kwanza… Tunataka eti tuwe wa kwanza kurusha habari hizo. Hapa ndipo sielewi. Mpaka hata mtu wa heshima kabisa! Mtu wa hesima ambaye ungefikiria angelikusaidia, lakini huyo ndiye anakuwa wa kwanza kurusha kitu ambacho ni Fake News,” alionesha mshaangao mkuu wa Kanisa nchini Tanzania. Kwa kuongeza: “sasa unajiuliza …. ninyi watu wa habari, mnatuelimisha mnatufundisha: hivi vyombo tuvitumieje? Habari hizi tuzitumieje? tuzipeleke namna gani? na habari mzipokee namna gani? Hilo ndilo swali langu linakuja hapo.”
Kadhalika Kardinali alisema: “Mimi ninafikiri kwamba tunayo haja ya kufanya hivyo Baba Mkurugenzi na ndugu zangu mnapokuwa mnatuelimisha au mnarusha habari hizo. Mnatuletea hizo hizo; mnazipokea sijuhi kutoka kwa nani, na sasa ndiyo balaa kabisa, kwa sababu ya Teknolojia ya kileo ambayo kila mmoja akiama tu anaweza kwa haraka kwa sababu ni dakika, ni sekunde anatuma kitu alafu, sasa kwa bahati mbaya hao ambao ni kama vile wamechanjwa.” Kardinali alitoa mfano wa usemi utumikao mahalia kuwa: “sisi nyumbani huwa tunasema kuwa watoto wengine wamechanjiwa kutembea! Akisimama tu yeye ni kuondoka! Kwa hiyo, sasa wengine kuhusu mambo ya habari ni hivyo hivyo; kama vile amechanjiwa. Ni mwehu, mlevu huyo wa kupokea mara moja. Ni kama vile hawalali wale. Inakuwa kama vile watu wanaotaliwa na pombe, wanaotawaliwa na dawa za kulevya hizo! Unataliwa, hujijuhi, lakini unatawaliwa. Kwa sababu kila unapoamka kwanza ni hicho, kabla hujanywa chai, hujapiga hata mswaki. Awe wa kwanza kutoa habari, lakini je ni taarifa gani unazozitoa?
Wanahabari mtusaidieni na kutufundisha
Kardinali Rugambwa hatimaye alisema:“mimi nimewaachia hayo kwa sababu staki kusema mengi, bali mtusaidieni kutufundisha na wafundishe hasa hawa ambao ndiyo wa kwanza wa kukurupuka wakifikiri ni heshima, wanapotoa habari, wakati wanatuletea habari ambazo si kweli; siyo habari za kuleta matumaini, kama Baba Mtakatifu anavyotuomba, badala yake ni habari ya kuleta mfarakano, habari za kuleta jazba, habari za kuleta maumivu na mahangamizi katika Jumuiya nzima, katika familia zetu na katika jamii zetu.” Kardinali Rugambwa kadhalika alionesha masikitiko kwamba: “Inasikita lakini basi, mtakapofanya hija hiyo tumuombe huyo Mtakatifu Gabrieli ambaye ni msimamizi wetu aweze nasi kwa maombezi yake au tukifuata mfano wake, tuhakikishe kabisa kwamba mawasiliano yetu yanakuwa ni mawasiliano ya kuleta matumaini, mawasiliano ya kujenga, na siyo ya kubomoa, siyo ya kuleta taharuki, bali yawe mawasiliano ambayo daima yanatukomboa,” alihitimisha.
Ujumbe wa Papa Francisko wa Siku ya Hupashanaji habari Ulimwenguni 2025
Kumbe basi katika fursa ya wito wa Kardinali Rugambwa, kwa wanahabari, ni vema kurudia kuusikiliza ujumbe huu wa mawasiliano wa Papa Francisko. Papa Francisko alisisitizaia juu ya Mawasiliano yanayoibua woga na kukata tamaa, ubaguzi, chuki na itikadi. Katika Ujumbe huo wa Papa ulioanzia kwenye uchunguzi wa njia za sasa za kutoa taarifa ambazo anasisitiza kuwa mara nyingi huwa hazina matumaini. Papa Francisko anaandika kwamba kuna mawasiliano ambayo huibua woga na kukata tamaa, ubaguzi na chuki na itikadi.” Kuhusiana na hilo mara nyingi sana hurahisisha ukweli kwa kuupunguza kuwa kauli mbiu ya kuchochea hisia za kisilika hadi kufikia hatua ya kueneza habari za uwongo au potofu kwa ustadi wa kutuma jumbe zinazokusudiwakusisimua akili za watu, kuchokoza na kuumiza. Njia ya kujieleza, ambayo inasaliti mawasiliano yanayotokana na uchokozi kuanzia maonesho ya mazungumzo hadi "vita vya matusi kwenye mitandao ya kijamii, dhana ya ushindani, na upinzani kuna hatari wakati wote, hadi udanganyifu kwa maoni ya umma.
Kuna Ndoto ya Papa ya kuwa na: Mawasiliano ya kusindikiza kaka na dada katika tumaini. Katika kukabiliana na hali hii iliyoakisiwa na matukio ya kutia wasiwasi na sio kwa uchache kile ambacho Papa anafafanua kama utawanyiko uliopangwa wa tahadhari, unaosababishwa na mifumo ya kidigitali ambayo inatuonesha kulingana na mantiki ya soko na kurekebisha mtazamo wetu wa ukweli, ni muhimu, kuepuka mantiki ya mawasiliano ambayo yanahitaji kutambua na kisha kushambulia adui. Matumaini ya Papa Fransisko, au tuseme ndoto yake ni ile ya mawasiliano yanayoweza kutufanya kuwa wenzi katika safari ya kaka na dada zetu wengi, ambayo yanawasha upya matumaini ndani yao katika wakati wa taabu. Kwamba yanazungumza kwa moyo yakiamsha si miitikio ya shauku ya kufungwa na hasira, bali mitazamo ya uwazi na urafiki; yenye uwezo wa kuzingatia uzuri na matumaini hata katika hali zinazoonekana kukata tamaa.
Papa anatoa ushauri wa Kutunga historia zenye matumaini. Dhana inayotia msukumo wa maono ya Papa, ambayo tunayosoma katika ujumbe wake inatokana na waraka wa kwanza wa Mtakatifu Petro, ambamo mtume huyo anawaalika Wakristo “wawe tayari siku zote kumjibu mtu awaye yote awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yake:” Msukumo ambao Papa Fransisko anabainisha kuwa una ujumbe wa aina tatu za kawaida za mawasiliano ya Kikristo: kujua jinsi ya "kuona mabaki ya mema yaliyofichwa hata wakati kila kitu kinaonekana kupotea; kujua jinsi ya kurejesha uzuri wa upendo wa Mungu na upya wake, na kujua jinsi ya kuwasiliana kwa upole. Papa Francisko anabanisha kuwa "Ninaota mawasiliano ambayo hayauzi udanganyifu au hofu, lakini yanaweza kutoa sababu za matumaini."
Papa anakazia kuwa lazima tupone magonjwa ya kimbele mbele na kujitosheleza. Na ili kufanya hivyo, Papa anaonesha, njia kwamba “lazima tupone kutokana katika magonjwa' ya kimbele mbele na kujitoshereza, na kuepuka hatari ya kujizungumza sisi wenyewe." Na kutunga mawasiliano hata zaidi katika mwelekeo wa Jubilei, iliyojaa “athari za kijamii,”Papa Francisko kwa mara nyingine tena anapendekeza matumizi ya historia zenye matumaini, historia hizo za wema wa kugunduliwa na kusimuliwa kwa kuzifuatilia"katika mikunjo ya habari. Inapendeza kupata mbegu hizi za tumaini na kuzifanya zijulikane na ili ulimwengu uwe angalau kiziwi kidogo kwa kilio cha wa walio maskini, kutojali kidogo na kufungwa kidogo.”