Tafuta

2025.04.09 Wanafunzi wanaoshiriki mpango wa Siku ya HIV/AIDS nchii India. 2025.04.09 Wanafunzi wanaoshiriki mpango wa Siku ya HIV/AIDS nchii India.  #SistersProject

Banahappa,India:Mwanga wa Matumaini kwa Watoto Walioathiriwa na VVU/UKIMWI

Katika nchi ambayo VVU/UKIMWI bado vinanyanyapaa shule ndogo ya Bweni huko Jharkhand inabadilishana maisha.Hii ni Shule ya Msalaba Mtakatifu ya Snehdeep ambayo inatoa elimu,huduma ya afya na kimbilio kwa watoto walioambukizwa na walioathiriwa.Ilizinduliwa mwaka 2014 ikiwa na wanafunzi 45 pekee,kwa sasa inahudumia watoto 230 na kuthibitisha kuwa huruma na uvumilivu vinaweza kuvunja vikwazo.

Na Sr. Margaret Sunita Minj, SCSC – Vatican.

Shule ya Msalaba Mtakatifu ya Snehdeep inatoa elimu, huduma ya afya na kimbilio kwa watoto walioambukizwa na walioathiriwa na VVU/UKIMWI. Ilizinduliwa rasmi kunako mwaka 2014 ikiwa na wanafunzi 45 pekee, ambapo kwa sasa inahudumia watoto 230 na kuweza kuthibitisha kwamba huruma na uvumilivu vinaweza kuvunja vizingiti vyote.

Utume una mizizi katika Huruma

Safari ya Shule ya Bweni ya Msalaba Mtakatifu ya Snehdeep ilianza kunako Mei 2014, wakati Sista Britto Madassery, muuguzi muhitimu na mwanzilishi wa shule hiyo, pamoja na Masisita wenzake, waliposhuhudia hali mbaya ya maisha inayowakabili watoto wanaoishi na VVU/UKIMWI. Wakati wa ziara za kifamilia, waligundua kwamba wengi wa watoto hawa hawakwenda shule kwa sababu ya kunyanyapaliwa, matatizo ya kifedha, au masuala ya afya. Jambo la kusumbua zaidi, walezi mara nyingi hawakujali ustawi wao, na kuacha shule kutokana na sababu za kimatibabu kulikuwa jambo la kawaida.

Kituo cha Afya katika shule ya wanafunzi
Kituo cha Afya katika shule ya wanafunzi

Kujenga kuanzia chini kwend Juu
Idadi ya watoto ilipoongezeka, shule ilibidi kuhamia maeneo mara sita hadi saba kabla ya kukaa Banahappa mwaka 2017. Hata hivyo, safari hiyo haikukosa matatizo. Wengi ikiwa ni pamoja na wa watawa walimdharau Sr. Britto, na wengine hata walikataa kumruhusu kuingia vyumbani mwao, wakimwita “Sr wa UKIMWI.” "Rafiki yangu mmoja alisema hataniruhusu kuja chumbani kwake! Walikuwa wakisema, 'Tazama, Sr wa UKIMWI anakuja kuomba chakula!'” Sr. Britto alikumbusha. Kununua ardhi ilikuwa changamoto nyingine kubwa, kwani maafisa wa serikali walipuuza mpango huo, wakisema kuwa watoto hao “hawana manufaa” kwa jamii. Lakini uvumilivu ulizaa matunda. Mswami wa Kihindu akitazama juhudi zisizo na kuchoka za Sr. Britto aliamua kufadhili ardhi kwa ajili ya shule hiyo. Usaidizi zaidi ulitoka kwa Mjesuit wa Australia Padre Crotty, ambaye alisaidia kufadhili hosteli, na Chama cha mikono iliyounganishwa(Manos Unidas,) ambacho kilichangia ujenzi wa shule. Shirika la Kitaifa la Kudhibiti Ukimwi (NACO) liliingilia kati kulipia gharama za matibabu, huku Serikali ya India ikiwajibika kwa mishahara ya wafanyakazi, chakula na sare. CRS pia ilitoa msaada wa matibabu. “Tunapofanya kazi ya Mungu, Yeye hushughulikia mahitaji yetu,” Sr. Britto mara nyingi alisema.

Elimu na Mustakabali zaidi ya Unyanyapaa


Shule ya Bweni ya Msalaba Mtakatifu ya Snehdeep inatoa fursa kamili za maendeleo kwa watoto wanaoishi na VVU/UKIMWI na wale wa wazazi walioambukizwa VVU. Zaidi ya elimu, shule inahakikisha watoto wanapata huduma nzuri za afya, mafunzo ya ufundi stadi, na malezi ya tabia. Taasisi hiyo inakuza vipaji vya kila mtoto—iwe katika taaluma, sanaa, bustani, au michezo—na kumsaidia kufikia uwezo wake kamili. Shule hiyo inatoa elimu hadi darasa la nane, lakini jitihada zinaendelea za kuipanua hadi darasa la kumi. “Nina furaha kuwaambia kwamba shule yetu hivi karibuni itakuwa hadi darasa la 10. Mawasiliano muhimu yanafanywa kwa hili. Baada ya darasa la 8, wanafunzi wetu huenda katika shule ya serikali iliyo karibu na kukamilisha masomo yao,” Sr. Britto alishirikisha hayo.

Ishara ya kukumbusha siku ya Ukimwi duniani
Ishara ya kukumbusha siku ya Ukimwi duniani   (REUTERS)

Utambuzi Unaostahiki


Mnamo Septemba 2024, Sr. Britto alitunukiwa tuzo ya “Uendelevu wa Misheni na Huduma” katika Mkutano Mkuu wa 81 wa Mwaka wa Bodi (AGBM) katika Chuo cha Matibabu cha Mtakatifu Yohane, Bengaluru, kwa kujitolea kwake kuelimisha na kuwainua watoto walioathiriwa na VVU/UKIMWI. Vyombo vya habari huko Hazaribagh pia vilitambua kazi yake, vikiakisi zaidi athari za utume wake

Shirika la Huruma ya Huruma ya Msalaba Mtakatifu nchini India(1894)

Sr. Britto ni wa Shirika la Masista wa Huruma ya Msalaba Mtakatifu, shirika la kitawa linalohudumu nchini India tangu 1894. Utume wao unabaki thabiti: “Tukichochewa na upendo wa Bwana wenye huruma, unaochanganyikana na mahitaji ya wakati, na kama washiriki katika fumbo la Kifo na Ufufuko wa Kristo, tunajitolea kutangaza Habari Njema na kujitahidi kuunda jamii mpya ya watu binafsi, familia na jumuiya, hasa wale wasiojiweza." Shule ya Bweni ya Msalaba Mtakatifu ya Snehdeep, inayoendeshwa na Masista hao, ni ushuhuda wa kile kinachoweza kupatikana wakati huruma inapokutana na hatua.
 

14 Aprili 2025, 10:52