Tafuta

Tarehe 27 Aprili 2025, Mwenyeheri Carlo Acutis atatangazwa kuwa Mtakatifu. Tarehe 27 Aprili 2025, Mwenyeheri Carlo Acutis atatangazwa kuwa Mtakatifu. 

Carlo Acutis,alifungulia wengine njia ya kwenda mbinguni

Tarehe 27 Aprili 2025,inakaribia ambapo wakati wa hafla ya Jubilei ya vijana barubaru na watoto,kijana mwenyeheri atatangazwa kuwa Mtakatifu. Mkurugenzi wa Jumba la Makumbusho la Hazina ya Basilika la Mtakatifu Francis huko Assisi,Ndugu Thomas Freidel(OFMConc),akizungumza na Vatican News alieleza mambo makuu ya hali yake ya kiroho:“Alitufundisha kwamba maisha yetu yanapatikana hapa na sasa na si maisha ya baada ya kifo.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwenyeheri Carlo Acutis alielewa kweli maana ya kuwa Mkristo katika maana kamili. Awali ya yote, mwelekeo wa kiroho kwa Mungu, ambao tunaweza kuufafanua kama jadi, unaojumuisha sala, kuabudu Ekaristi, adhimisho la Misa, kusali Rozari. Pili, kuwashuhudia wengine na kuwajali masikini na wahitaji." Hiki ndicho kichocheo cha utakatifu wa Carlo Acutis - kijana mwenyeheri ambaye alikufa kwa sababu ya saratani ya damu, akiwa na umri wa miaka kumi na tano tu, ambaye atatangazwa kuwa mtakatifu tarehe 27 Aprili 2025,  wakati wa Jubilei ya Vijana barubaru, ambayo yalisisitizwa na  Ndugu Mdogo Mfansiskani Thomas Freidel,(OFM Conv,) ambaye ni  mkurugenzi wa Makumbusho ya Hazina ya Basilika ya Mtakatifu Francis huko Assisi, akikutana na mwaandishi wa habari wa Radio Vatican, Stefanie Stahlhofen.

Karlo Acutis
Karlo Acutis

Alionesha njia ya kwenda kwa Mungu

Kijana huyo mwenyeheri, Carlo Acuti, aliishi Ekaristi kwa uangalifu kama "njia kuu ya kwenda Mbinguni" kama alivyokuwa akisema mwenyewe. “Mtu anapokufa akiwa na umri mdogo, haachi kwa kawaida kitu chochote cha maandishi, lakini kwa Carlo Acutis, ni kinyume kwa sababu haya ni maneno ambayo yanavutia sana. Alikuwa na maana ya kusema kwamba Ekaristi, kukutana na Mungu, kumpokea Kristo, ni njia inayoongoza kwenye utimilifu wa maisha, inayoongoza kwenye ukamilifu pamoja na Mungu. Hasa njia kuu ya Mbinguni. Kwa hivyo, kukaa kwenye njia hiyo kunahakikisha utimilifu wa maisha,” alisisitiza Padre Freidel kwa vyombo vya habari Vatican.

Carlo Acutis alikuwa gwiji wa Intaneti
Carlo Acutis alikuwa gwiji wa Intaneti

Kuishi uhusiano pamoja na Mungu 

Katika hali ya kiroho ya Carlo Acutis ni wazi sana kwamba utimilifu na maisha yaliyofufuliwa tayari yana uzoefu katika maisha haya. Imani yetu si kitulizo kwa nyakati bora zaidi za maisha ya baada ya kifo.” Na Carlo Acutis ni kielelezo kizuri cha jambo hilo. Alijua kwamba kuishi katika uhusiano pamoja na Mungu hutimiza hapa na sasa, kwa shangwe, kwa tumaini, kwa kutumainiwa. Kutembea katika njia yangu ya imani, ambayo lengo lake kuu ni kile tunachoita Mbingu, yaani, ukamilifu na Mungu. Uhusiano na Kristo, adhimisho la Ekaristi, ni njia ya uhakika ya kufika huko. Kwa hivyo, katika nukuu hiyo, hata kwa taswira ya kisasa ya barabara kuu, uelewa wa kibinafsi wa Carlo Acutis wa imani umeoneshwa vyema."

Mwenyeheri Carlo Acutis
Mwenyeheri Carlo Acutis

Aliongoka na utu wake

Hata hivyo hakuwa mjanja, lakini mtu wa kawaida sana. "Hivi ndivyo kila mtu aliyemfahamu alisema. Kwamba hakuwa mgeni hata kidogo, lakini aliunganishwa vyema katika mzunguko wa marafiki zake. Alicheza mpira wa miguu hapa Assisi na shuleni, huko Milano. Alikuwa ni mtu wa kupendwa tu. Pia alipendwa na wanafunzi wenzake au marafiki ambao hawakuwa na mwelekeo wa imani. Hili ndilo ambalo kila mtu anashuhudia juu yake, yaani, alipata mengi, kwa urahisi kupitia nafsi yake, kupitia tabia yake: hivyo aligusa mioyo ya watu wengi,” Ndugu Mdogo Thomas Freidel alihitimishwa kusema hayo kwa vyombo vya habari vya Vatican.

Siku ya kutangazwa mwenyeheri (2021)
Siku ya kutangazwa mwenyeheri (2021)
Kutangazwa Mtakatifu Carlo Acutis
16 Aprili 2025, 11:27