Tafuta

Ask.Sorrentino:“Carlo Acutis ni Mfransiskani asiye na mavazi”

Aprili 2,jijini Roma kitabu kilichotiwa saini na Askofu wa Assisi-Nocera Umbra-Gualdo Tadino na Foligno kuhusu“Carlo Acutis katika nyayo za Francis na Clara wa Assisi.Kuwa asili na siyo nakala,”kiliwasilishwa mbapo mwandishi anonesha uhusiano wa kina wa kijana mwenyeheri kwa Assisi na Mtakatifu Francis.Askofu wa Jimbo hilo akizungumza na Vatican alisema:"Carlo yuko anakung’uta dhamiri na roho huku akiwatia moyo vijana katika mabara yote.”

Na Stefanie Stahlhofen,Daniele Piccini na Angella Rwezaula – Vatican.

Carlo Acutis alifuata nyayo za Fransis. Alitaka kwenda Assisi kwa sababu Mtakatifu Fransis ndiye aliyemtia moyo. Hakutaka kuwa Mfransiskani mwenye mavazi ya kifransiskani, yaani Mfransiskani wa kawaida, kama wana wa Francis. Bali yeye alitaka kuwa wa Asili katika hilo pia. Alitaka kupata msukumo kutoka kwa Mtakatifu Francis, lakini kwa mfano wa utakatifu  wake wote mwenyewe. Ni kwa maneno hayo Askofu Domenico Sorrentino, wa Jimbo Katoliki la  Assisi - Nocera Umbra - Gualdo Tadino na Foligno, nchini Italia alielezea kwa vyombo vya habari vya Vatican kuhusu uhusiano wa nguvu kati ya mwenyeheri wa milenia, ambaye alikufa kwa saratani ya damu akiwa na umri wa miaka kumi na tano tu na yuko kwa Maskini wa Assisi. Alisema hayo  alasiri  tarehe 2 Aprili 2025 katika Chuo Kikuu cha Anci jijini Roma wakati akiwasilisha kitabu  kuhusu Carlo Acutis. Kitabu hicho chenye kichwa: “Katika nyayo za Francis na Clara wa Assisi. Kuwa Asili na  siyo nakala,” kilichochapishwa mnamo Desemba 2024 na Toleo la Nyumba ya Uchapishaji ya  Wafransikani.

Mwenyeheri Carlo Acustis
Mwenyeheri Carlo Acustis   (ANSA)

Kuvuliwa nguo kwa Carlo na Francis

Iwe Carlo  na Mtakatifu Francis wa Assisi wote  wana  asili  moja ya kinabii ya “kujivua” alisema  Askofu  Sorrentino kwamba  “Mtakatifu Francis wa Assisi kwa miaka 800 iliyopita, alifanya ishara hiyo ya kinabii ya kujivua nguo zake, kukataa pesa zake na hata urithi wake, kwa sababu alitaka kuwa mali ya Yesu tu na maskini, ambapo Yesu anajidhihirisha. Vivyo hivyo, Carlo pia ni mtakatifu wa kuvua nguo. Hili lingeonekana kuwa gumu kuelewa kutumika kwa mtu kama yeye ambaye alitoka katika familia tajiri, na ambaye hakukosa chochote. Francis alijivua kila kitu, hata tofauti na baba yake. Carlo, kwa upande mwingine, hadi mwisho, alikuwa na kila kitu ambacho kijana wa umri wake angeweza kuwa nacho. Bado hata kwa Acutis kulikuwa na wakati ambapo Bwana alimwomba avue nguo zake, yaani, wakati ambapo kile ambacho Francis wa Assisi alikiita 'Dada Kifo' kilipomfikia yeye.” Askofu Sorrentino aliendelea kusema kwamba Dada kifo kwa hiyo alifika mapema sana, kama inavyosemwa wakati wa kuangalia maisha kwa ujumla. Kijana anapokufa tunasema ni jambo la kipekee, la uchungu na la kusikitisha. Carlo alikufa akiwa na umri wa miaka kumi na tano."

Mwili wa Carlo Acustis
Mwili wa Carlo Acustis

Video ya kutabiri na kumkaribisha "Dada Kifo"

Kijana mwenyeheri alifahamu kuvuliwa kwake ambako Bwana alikuwa akimtaka. Kwa hakika, aliacha alama ya "ndiyo" yake kwa Kristo katika video, kama vile mtu angetarajia kutoka kwa mtakatifu wa kisasa na wa kidijitali.” Jambo moja ambalo lilinishangaza sana na kunifanya nielewe mpango wa Mungu kwa maisha yake ni kile ambacho mama yake alikuta  kwenye kompyuta yake. Hicho ni , klip ya video  ambayo alikuwa ametengeneza mwenyewe, ambapo Carlo anaonesha jambo fulani la utabiri kwamba kifo kinakuja, miezi miwili kamili kutokana na saratani ya haraka  na kweli kumchukua kutoka katika  maisha,” alisema Askofu Sorretino. Katika video hiyo, mvulana huyo alisema: “Nimekusudiwa kufa” halafu, askofu akaongeza, pia anatabasamu kwa uzuri, kana kwamba tayari yuko Mbinguni, na kufungua mikono yake kana kwamba anamkaribisha Dada Kifo au, ukipenda, kutaka kumpigia makofi. Na kwa hiyo nikilinganisha na Mtakatifu Fransis, ilionekana kwangu kuwa huu ulikuwa wakati ambao Yesu alimwomba ajivue mwenyewe kabisa."

Carlo Acutis na Francis wa Assisi
Carlo Acutis na Francis wa Assisi

 Carlo, chanzo cha matumaini

"Matunda ya kiroho ya ushirikiano huu, ulioanzishwa Mbinguni, kati ya Kristo, Carlo Acutis na Francis wa Assisi yanaonekana. Anafanya dunia kusonga mbele," alisema Askofu Sorrentino. "Tuna mtiririko wa ajabu wa mahujaji hapa. Katika miaka kumi na tisa ya huduma kama Askofu sijawahi kuona kitu kama hicho. Carlo ni tumaini kubwa kwa ulimwengu. Anatikisa dhamiri na roho, anatia moyo vijana katika mabara yote. Shukrani kwa 'timu hii maalum' inayojumuisha Yesu, Carlo, Francis na Clara, na bila shaka watakatifu wengine wengi wa Kanisa la ulimwengu wote, pia sisi tunaweza kutumaini na kusonga mbele kwa ujasiri,” alihitimisha Askofu wa mji wa Assisi.

Antonia, Mama yake Carlo Acutis
Antonia, Mama yake Carlo Acutis   (ANSA)
Kanisa la mahali alipo Carlo Acutis
Kanisa la mahali alipo Carlo Acutis
Kitabu kuhusu Carlo Acutis
04 Aprili 2025, 10:19