Tafuta

2025.04.03 Misa ya Kardinali Matteo Zuppi katika hitimisho ya Mkutano wa Kisinodi wa Baraza la maaskofu Katoliki nchini Italia. 2025.04.03 Misa ya Kardinali Matteo Zuppi katika hitimisho ya Mkutano wa Kisinodi wa Baraza la maaskofu Katoliki nchini Italia. 

Kard.Zuppi:Njia ya Kanisa si ratiba iliyoainishwa bali ni kumfuata Yesu katika ubinadamu

Kardinali Zuppi aliongoza Misa iliyohitimisha Mkutano wa Pili wa Sinodi ya Kanisa la Italia katika Basilika ya Mtakatifu Petro mjini Vatican,Aprili 3 ambapo katika mahubiri yake alisisitiza juu ya ulimwengu unavyohitaji mabadiliko ya kutokuwa na aibu,mateso,kurudisha nyuma jumuiya za watu binafsi katika umoja wa watu binafsi.Tunahitaji kuanza tena kukumbuka mwaliko wa Papa kwa kulitazama Kanisa jinsi gani Roho anavyofanya na si kama ulimwengu unavyofanya.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Umoja katika upendo kwa Papa Francisko, Makanisa na jumuiya mbalimbali za Italia, ambao wametembea na kushiriki katika mashauriano na majadiliano mengi. Yote  hayo yaliibuka katika Mkutano mjini Vatican, kuanzia Machi 31 hadi tarehe 3 Aprili 2025, ukiwa ni Mkutano wa Pili wa Sinodi  ya Kanisa la Italia na kuhitimisha kazi yao, kwa Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Kardinali Matteo Zuppi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Bologna na Rais wa Baraza la Maaskofu, Italia (CEI).  Katika mahubiri yake kwa waamini,  washiriki wa Mkutano huo wa kisinodi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Kardinali Zuppi alitoa wito wa kuwa na umoja kwamba, "Tunapenda na kutetea umoja kwa gharama yoyote, kutoka Mashariki hadi Magharibi, ambayo daima ni msingi wa amani.” Kardinali huyo  alisisitiza kwamba,  njia ya sinodi inaturudisha kwenye mwelekeo muhimu wa jumuiya, katika ulimwengu uliojaa  mateso, ubinafsi, ambao unakufanya ujisikie vibaya na  ambapo sio kwa bahati mbaya kwamba mantiki ya nguvu inatawala, ya utaifa wa zamani ambao hurekebishwa tena na kupata nafasi nyingi hasa  kwa sababu kuna hisia kidogo ya jumuiya na ya jamii ya ulimwengu inayokuja pamoja.

Misa ya hitimisho la Mkutano wa Kisinodi Italia
Misa ya hitimisho la Mkutano wa Kisinodi Italia   (ANSA)

Na ikiwa, kama Papa Francisko alisema, kuwa nabii daima ni kutetea mawazo ya mtu wa jino kwa jino na msumari kwa msumari , akiamini kwamba ni nzuri kwa kila mtu, na kukubaliana tu na wale wanaofikiri kama sisi, badala yake  ni Roho ambaye anatuunganisha, Roho ambayo inakuwa ushirika ambayo huzalisha ushirika, ambayo inatufanya kubadili njia au ambayo inatufanya tupate na kutetea utakatifu daima, alisisitiza Kardinali Zuppi. Na hapo lazima tujihadhari na wale wanaotukomboa kwa kiburi cha imani zao ambazo mara nyingi husababisha kudharau wengine na kuacha kuleta asili ya mtu mwenyewe. Na ni lazima tuanze tena kukumbuka mwaliko wa Papa wa kulitazama Kanisa jinsi Roho anavyolitazama, si kama ulimwengu unavyofanya kwa sababu ikiwa mtazamo wa kidunia utaona miundo inafanywa kwa ufanisi zaidi, mtazamo wa  kiroho unawaona  kaka na dada wakiomba huruma. Kwa rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia, alisisitiza kuwa katika sinodi safari iko pamoja tukiwa watumishi wa kila mmoja wetu, tukiunganisha sisi kwa sisi, kujenga uhusiano wenye hisia, kwa sababu Kanisa si wazo bali ni kukutana, uhusiano ambapo katikati ni Bwana ambaye kwa ajili yake mtu hupoteza maisha au mawazo ya mtu yanayoihifadhi. Iwapo, badala yake, mipango  yetu, miundo yetu na madhumuni yetu  ya mageuzi yanakuja kwanza tutaanguka katika utendakazi, ufanisi, usawa na hatutazaa matunda aliongeza  Kardinali Zuppi akinukuu maneno ya Papa Francisko tena.

Misa ya Hitimisho la Mkutano wa CEI
Misa ya Hitimisho la Mkutano wa CEI   (ANSA)

Kwa hiyo, njia ya Kanisa, ambayo si ratiba iliyoainishwa, lakini ya kumfuata Yesu, hutufanya tukutane ubinadamu kwenye njia kulingana na Roho, n asio  Bunge ambamo kudai haki na mahitaji kulingana na ajenda ya ulimwengu na sio fursa ya kwenda mahali ambapo upepo unakupeleka, lakini fursa ya kuwa mtulivu kwa pumzi ya Roho. Hivyo kutiwa moyo  na kiongozi wa Kanisa  ni kutembea pamoja, kwa sababu tumeitwa kuwa moyo mmoja na nafsi moja, ili kutambua sauti ya Roho ambaye mbele ya njia panda ya maisha, anatupendekezea njia bora zaidi ya kuchukua”. Katika ulimwengu wa migawanyiko, vurugu na hofu ni muhimu kwenda nje kutangaza na tusibaki tumefungwa ndani yetu alihimiza Kardinali kwamba tunapaswa kuwa nyumba ya kukaribisha na sio kuzingatia shida na masilahi ya mtu binafsi tu, juu ya ulinzi mkali wa utaifa wa kila mtu binafsi.

Kardinali Zuppi alisisitizia umoja wa Kanisa
Kardinali Zuppi alisisitizia umoja wa Kanisa   (ANSA)

Kanisa haliwezi kuratibiwa na miradi ya kisasa haitoshi.  Roho hutuweka huru kutokana na mashaka ya dharura na hutualika kutembea kwenye njia za ushuhuda, za umaskini, za utume, ili kutukomboa kutoka kwetu na kututuma ulimwenguni. Wakristo, kwa ufupi, hawana budi kujishuhudia wenyewe bali Bwana, na kwa Bwana tu, kwa sababu sisi ni kiakisi cha upendo wa Mungu na tuko hivyo ikiwa tunamulika nuru yake juu, tunajiweka huru wenyewe kutoka katika ukimbelembele.  Yesu hapokei utukufu kutoka kwa wanadamu. Utukufu mkuu zaidi ni upendo. Kwa kuhitimisha Kardinali Zuppi alifafanua kwamba  watu wa kiroho pekeeyaani, wale wenye uwezo wa kubadili moyo katika imani na ambao wana shauku kuu juu ya ulimwengu wanaweza kuongoza ubinadamu kwenye hatima bora zaidi.”

Mahubiri ya Kardinali Zuppi 3 Aprili 2025
04 Aprili 2025, 14:11