Tafuta

2023.11.17 Mons. Emilio Nappa 2023.11.17 Mons. Emilio Nappa 

Korea Kusini:Ask.Mkuu Nappa:miaka 60 ya PMS:Kanisa la utume ni Kanisa linalotembea!

Askofu Mkuu Nappa aliadhimisha misa huko Seoul,Machi 31 kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 60 tangu kuanzishwa PMS.“Wazee wenu katika imani,walilinda imani yao chini ya mnyanyaso mkali,wakiota uzima wa milele.Wenyeheri na watumishi waliketi pamoja wakiitana kaka na dada,alisisitiza Rais wa zamani wa PMS na hakukosa kushukuru na kumsifu Mungu kwa ajili ya wale wote ambao wametumikia PMS ya Korea Kusini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ni kwa hisia kubwa kwamba ninatembelea nchi hii ya Mashahidi wa  Korea, nchi ya pekee katika historia ya Kanisa, ambayo imani iliendelea ndani yake yenyewe kabla ya kufika kwa wamisionari. Ndivyo alivyoanza Askofu Mkuu Emilio Nappa, Katibu Mkuu Msaidizi wa mji wa  Vatican na Rais wa zamani wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa(PMS), katika  Ibada ya Misa Takatifu katika Jimbo kuu la Seoul, Nchini Korea Kusini wakati wa  mahubiri yake katika misa ya ukumbusho wa mwaka wa 60 tangu kuanzishwa kwa Kurugenzi ya Kitaifa ya Utume wa Kimisionari  wa Kipapa,(PMS),  Jumatatu, tarehe 31 Machi 2025. Katika maadhimisho hayo yaliyoudhuriwa na Askofu Mathias Iong-hoon Ri, Rais wa Baraza la Maaskofu wa Korea, Askofu mkuu Giovanni Gaspari, Balozi wa Vatican nchini Korea Kusini, mapadre wengi, wakurugenzi wa zamani wa PMS, na wa wasasa, watawa wa kike na wamisionari walei, pamoja na mamia ya waamini katika Kanisa Kuu la Jimbo kuu la Seoul, Myeongdong ,

“Wazee wenu katika imani, walilinda imani yao chini ya mnyanyaso mkali, wakiota uzima wa milele. Wenyeheri na watumishi waliketi pamoja wakiitana kaka na dada, alisisitiza Rais wa zamani wa PMS na hakukosa kushukuru na “kumsifu Mungu kwa ajili ya wale wote ambao wametumikia PMS ya Korea katika historia yao, akiwaalika waamini wasihi kwa nia ileile […].” Rais wa zamani wa PMS hata hivyo  mwishoni mwa mahubiri yake vile vile aliezea shukrani zake kwa Kanisa la Korea, ambalo linawaweka mapadre  wake katika matumizi ya Kanisa la Ulimwengu.

Katika salamu zake, Kardinali Andrew Soo-jung Yeom, Askofu Mkuu Mstaafu wa Seoul, alirejea historia ya PMS nchini Korea, huku akikumbusha kwamba “Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa ya Korea yalianzishwa tarehe 29 Juni 1965 kama ‘Tume ya Kipapa ya Kueneza Imani’. Zaidi ya hayo, aliakisi jinsi ambavyo “katika kipindi cha miaka 60, kumekuwa na mabadiliko kutoka katika Kanisa linalopokea” (akirejea kipindi ambacho Korea ilikuwa bado katika umaskini na seminari zilinufaika na ruzuku kutoka PMS),  hadi kufikia Kanisa linalotoa.” Hii ni kwa sababu alisema “Kanisa la utume, ni Kanisa linalotembea, Kanisa linaloeneza manukato ya Kristo kwa njia ya mapendo ya maisha ya kila siku.”

Ushuhuda wa Walei

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Habari za Kimsionari Fides, linabainisha kuwa adhimisho la Ekaristi lilifuatiwa na Kongamano la utume na shuhuda kadhaa kutoka kwa wamisionari waliowekwa wakfu na walei. Kutoka Jimbo la Suwon, wanandoa wamisionari walei wa Consolata, Thomas Aquinas Seong-ho Song na Rosa Eun-hyung Rosa Yang, babu na bini wa wajukuu 3, walisimulia jinsi walivyoitwa wakiwa na umri wa miaka 60 kwenda katika utume nchini Tanzania baada ya uzoefu wa hapo awali nchini Msumbiji. "Kuishi na watu na kuwapenda ili kuweza kumtangaza Kristo zilikuwa sifa kuu za misheni iliyoshuhudiwa na wanandoa. Wanahudumu kama wasimamizi katika Kituo cha Wamisionari na wao kama makamu mkurugenzi.

Thomas na Rosa pia walikumbuka jinsi ilivyokuwa muhimu kujifunza lugha kama kitambulisho kikuu cha kuanza kuhudhuria jumuiya za eneo mahalia  na kuzoea maneno yao ya kiutamaduni, pia wakiakisi jinsi hali waliyokumbatia ni mahali ambapo ni vigumu kuishi bila kuwa  sala.” Ushuhuda mwingine muhimu ulikuwa ule wa Sr Anna Kang, wa Wamisionari wa Shirika la Masista Wanaofundisha  na Umisionari katika Ufilipino tangu 2018 hadi 2023. Sr Anna, kwa msaada wa PMS na shukrani kwa msaada wa wafadhili wengine wengi, ametekeleza Mpango wa shule ya awali, iliyoundwa malumu ili kutoa mahali pa kukaribisha na kuelimisha watoto wa nyumbani ambao uishi katika  nyumba yenye chumba kimoja,ambacho ni mahali pa kulala na bafu pale pale.

Kongamano

Katika Kongamano lililoongozwa na Padre Pietro Dong Won Kim, mkuu wa Idara ya Utume wa watu ( ad gentes) wa Jimbo kuu la Seoul, alisimulia uzoefu wake wa kimisionari huko Taiwan katika parokia ya wenyeji wa milimani, na kuakisi jinsi safari ya umisionari haiamriwi na matakwa ya kibinafsi (hata kama inaonekana hivyo), lakini kwa mwitikio wa wamisionari wa Mungu."   Aidha Padre  Marco Sungsu Kim, ofisa wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, kitengo cha kwanza na Makanisa mapya ambaye alifuatana na Askofu Mkuu katika ziara yake ya Japan na Korea Kusini, akimgeukia  Askofu Mkuu Nappa ambaye baada ya kuteuliwa na Baba Mtakatifu hivi karibuni, moja kwa moja kuacha  PMS alisema kuwa "Tunatumaini kwamba roho wa kimisionari uliyoipata ukiwa Rais wa PMS itaendelea kukusindikiza katika kutekeleza utume wako mpya".

Ziara ya Askofu Mkuu Nappa nchini Korea Kusini

Ziara ya Askofu Mkuu Nappa nchini Korea Kusini ilianza tarehe 26 Machi kwa kutembelea Ubalozi wa Vatican, Askofu Mkuu Giovanni Gaspari na kuhitimishwa asibuhi tarehe 31 Machi 2025. Wakati wa kukaa kwake Askofu Mkuu  Nappa alishiriki kwa ujumbe wa matashi mema katika misa iliyoadhimishwa tarehe 26 Machi tena huko Myeongdong, kwa ajili ya kuadhimisha miaka 12 ya kuchaguliwa kwa Papa Francisko pamoja na maaskofu wote wa Korea waliokusanyika kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Baraza la Maaskofu wa Korea.

Askofu Mkuu pia aliadhimisha misa na Masista Wasalesian (watawa wapatao 30) mnamo Machi 27 na alichukua fursa hii kuwashukuru kwa kujitolea kwao kwa vijana wa Korea Kaskazini. Siku hiyo hiyo alitembelea Baraza la Maaskofu la Maaskofu wa  Korea ambako alikaribishwa kwa “shukrani nyingi” na Katibu Mkuu Stefano Cheol-soo Lee na kuwasilisha salamu za Kardinali Tagle, Mwenyekiti Mwenza wa Baraz ala Kipapa la Uinjilishaji. Kipindi cha siku kilihitimishwa kwa mahojiano na wanafunzi wa shule ya kati wa Kikatoliki. Mnamo Machi 28 alikwenda jimboni Daegu ambapo aliadhimisha misa na kuwa na mkutano mfupi na  Monsinyo Thaddeus Hwan-kil Cho, alitembelea Seminari Kuu ya Jimbo Kuu la Daegu, Gwandeokjung (makumbusho ya wafiadini), Kanisa Kuu, makao makuu ya "Nyakati za Kikatoliki" na makao makuu ya kikanda ya "Shirika la Utangazaji la Amani la Kikatoliki".

Tarehe 29 Machi, alitembelea Jimbo la  Suwon, ambapo Askofu wake ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Korea, Askofu Mathias Iong-hoon Ri. Alasiri, baada ya kutembelea Madhabahu ya Maria ya Namyang (hapo awali iliwekwa wakfu kwa mashahidi wasiojulikana, na kisha, mnamo 1991, kwa Bikira Maria), akaadhimisha Misa na watoto wapatao 200 katika parokia ya Mtakatifu Pieltrelcina huko Hwaseong (Dongtan Bansong-dong Kanisa Katoliki), kisha akatembelea Seminari kuu ya Sh "Seosomun", mahali ambapo Wakatoliki wengi wa zamani  wa Korea waliuawa, akiwemo  Peter Seung-hun Yi aliyebatizwa wa kwanza. Zawadi ambazo Askofu Mkuu Nappa alipeleka  kwa ajili ya Maaskofu na washiriki wa Japan na Korea ni pamoja na uchoraji wa mbao wa msalaba uliotolewa na Mtakatifu Yohane Maria Vianney kwa Mwenyeheri Pauline Jaricot (Mwanzilishi wa Shirika la Kipapa la Uenezaji wa Imani, POPF) na vijitabu vya maisha ya mwanzilishi wa kazi ya Bigard Bigard (P.A rozari za kimisionari za Baraza la Kipapa la Uinjilishaji.

01 Aprili 2025, 15:58