Liberia:Msaada wa kiafya kwa watu wenye ulemavu au katika hali ya umaskini mkubwa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa miaka kadhaa sasa, Parokia ya Mtakatifu Yohane Maria Vianney huko Foya, katika kona ya mbali ya nchi ya Liberia, iliunda kikundi cha hisani kusaidia gharama za huduma za afya kwa wale ambao hawawezi kufanya hivyo, hasa walemavu na watu walio katika umaskini mkubwa. Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari za Kimisonari Fides, aliyekuwa akitunza jumuiya hiyo kwa miaka michache ni Padre Lorenzo Snider, wa Shirika la Misheni za Afrika (SMA), ambaye alizindua mpango unaojumuisha, pamoja na mambo mengine, ziara za matibabu na dawa msingi kwa watu wenye ulemavu wa viungo au katika umaskini uliokithiri, usambazaji wa dawa za lazima kwa watu wenye matatizo ya kifafa na matibabu ya magonjwa mengine ya akili; maziwa ya unga na unga wa karanga kwa watoto wenye utapiamlo na usaidizi wa upasuaji wa dharura.
Utapiamlo na kifafa
Kwa mujibu wa mmisionari ambaye ni Padre wa parokia ya Mtakatifu Yohane Maria Vianney alisema: "Kuanzia matibabu ya malaria hadi maambukizi na kliniki za wanawake wajawazito kabla ya kujifungua. Kwa kuanza kusaidia, matukio mapya yalifunguliwa: watu wenye kifafa, hawawezi kulipa matibabu yenye thamani ya senti 20 kwa siku, kisha watoto wenye utapiamlo, kutokana na kifo cha mama yao kwa sababu ya matatizo ya baada ya kujifungua au hali nyingine.”
Matatizo mengine
Hakukosekani matatizo mengine aliongenza kuwa “ya watu wanaojitokeza parokiani wakiwa na majeraha ambayo yamesahaulika kutokana na umaskini, ambao labda wameteseka kwa miaka mingi au katika hali zingine kwa miongo kadhaa.” Ikiwa yote yataenda vizuri alieleza Padre Snider, kuwa watu 500 kwa mwaka watafaidika na msaada huu, wanaotibiwa katika Kituo cha Afya cha Foya, wakifuatiliwa na mapadre wa shirika hili (SMA (takriban watu 40 kwa mwezi), katika hospitali ya Borma au ile ya Gueckedou (Guinea, kituo pekee kilicho na maabara nzuri ya uchambuzi, Ultrasound na X-Ray; Watu 20 wenye matatizo ya kifafa na familia 20 zenye watoto wenye utapiamlo.