Tafuta

Uharibifumkubwa wa tetemeko la Ardhi nchini Myanmar. Uharibifumkubwa wa tetemeko la Ardhi nchini Myanmar. 

Myanmar,CEI yatenga euro 500 elfu kwa huduma ya kwanza kwa waathiriwa wa tetemeko la ardhi

Kardinali Zuppi,Rais wa Baraza la Maaskofu(CEI) nchini Italia alieleza rambirambi zake kwa watu waliokumbwa na tetemeko ambalo limesababisha zaidi ya vifo vya watu 2000 nchi ya Asia huku likiacha uharibifu mkubwa wa makazi na miundo mbinu.Fedha zilizotengwa kwa dharura zitaratibiwa na Caritas Italia.

Vatican News

Urais wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI)umeonesha mshikamano na watu walioathiriwa na tetemeko la ardhi lililoharibu Myanmar mnamo Ijumaa, tarehe 28 Machi 2025 na athari mbaya  pia kwa nchi zingine za Bara la Asia. Tetemeko hilo la ardhi ambalo ndio kitovu chake katika eneo la Mandalay limesababisha maelfu ya vifo, majeruhi na watu waliokimbia makazi yao pamoja na kuharibu makazi na miundombinu. "Tuko karibu na dada na kaka zetu nchini Myanmar: rambirambi na ukaribu wetu uwaendee. Tunawaombea wahanga, wakiwemo watoto wengi, na familia zao, kuhakikisha msaada wa Makanisa yetu," alisema Kardinali Matteo Zuppi, Askofu Mkuu wa Bologna na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia (CEI.)

Mifuko ya fedha zinazoratibiwa na Caritas Italia

Ili kukabiliana na hali ya dharura, Urais wa Baraza la Maaskofu Italia umeamua kutenga euro 500 elfu za awali kutoka katika mfuko wa  fedha za ‘8xmille’ ambazo wananchi wa Italia  hutenga kwa ajili ya Kanisa Katoliki ambazo zitatumika kwa huduma ya kwanza, inayoratibiwa na Caritas Italia ambayo, tangu mwanzo, imekuwa ikiwasiliana moja kwa moja na KMSS (Karuna ambao ni Mtandao wa utume wa mshikamano wa kijamii wa Caritas Myanmar na mitandao mingine ya kimataifa ya Caritas. Myanmar kwa muda mrefu imekuwa ikikumbwa na hali ngumu na hatari: mzozo wa kibinadamu nchini humo unaathiri watu milioni 19.9 - zaidi ya theluthi moja ya wakazi - ambao walikuwa tayari wanahitaji msaada kutokana na migogoro ya ndani, hatari ya kiuchumi na majanga ya asili.

Unaweza kuchangia dharura hiyo

Tetemeko la ardhi lilizidisha haya yote, likijaribu sana rasilimali za kitaifa na uwezo wa kukabiliana. Kwa matumaini kwamba uhasama wa ndani utakoma na misaada ya kibinadamu itafikia lengo lake, Urais wa (Baraza la Maaskofu Katoliki Italia-CEI) unakaribisha jumuiya za kijimbo na parokia kuchangia mshikamano unaopaswa kutekelezwa mara moja na kwa ujenzi wa nyenzo na jamii utakaotekelezwa katika miezi na miaka ijayo. Habari na masasisho kuhusu hali nchini Myanmar na jinsi ya kuchangia zinapatikana kwenye tovuti ya Caritas Italia:www.caritas.it.

01 Aprili 2025, 15:00