Sudan Kusini,Jimbo la Torit: hofu kwa shambulio la Parokia ya Mama Yetu Mpalizwa huko Loa
Na Paul Samasumo – Vatican.
Katika taarifa iliyoshirikishwa kwa vyombo vya habari vya Sudan Kusini na kutolewa kwa Vatican News tarehe 3 Aprili 2025, Askofu Emmanuel Bernardino Lowi Napeta, wa Jimbo Katoliki la Torit, alitoa wito wa kufanya "uchunguzi usio na upendeleo wa tukio mashambulizi" ya moja ya Parokia ya jimbo lake.
Hali ya hofu na wasiwasi
Jimbo Katoliki la Torit lilisema jinsi lilivyotazama shambulio la tarehe 26 Machi 2025 kwenye majengo ya Parokia ya Mama yetu wa Kupalizwa huko Loa, wilaya ya Magwi, kwa wasiwasi mkubwa. Kwa mujibu wa Askofu Napeta, wahusika wa shambulio hilo ni kikosi cha ndani cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini(SSPDF). Askofu huyo alisisitiza zaidi kwamba wauaji hao waliondoka na mwili wa marehemu. Kwa njia hiyo Jimbo hilo linatoa wito kwa mamlaka ya Sudan Kusini kusaidia kurejesha mwili wa marehemu. Jimbo limetaka uchunguzi ufanyike bila upendeleo. Hakukuwa na taarifa za hali ya mtu aliyejeruhiwa na hadi sasa, serikali haijazungumzia suala hilo. Sababu ya shambulio hilo kwenye parokia bado haijafahamika.
Kujitolea kwa Haki na Amani
Askofu Napeta hata hivyo alisisitiza kuwa Jimbo la Torit limejizatiti kwa ajili ya amani na haki kwa wote na litaendelea kuweka kipaumbele katika huduma yake kwa binadamu na kukomesha aina zote za ukatili. "Ahadi ya Jimbo Katoliki la Torit la kukuza haki na kuishi pamoja kwa amani imethibitishwa vyema na inajulikana na uongozi mzima wa Serikali ya Sudan Kusini," Askofu Napeta alisisitiza.
Wapendwa wa Sudan Kusini
Mkataba wa kugawana madaraka wa mwaka 2018 kati ya Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na Riek Machar, Makamu wa Kwanza wa Rais, ulimaliza vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka mitano. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS hivi karibuni ulitoa wito kwa viongozi wa Sudan Kusini kujizuia kufuatia kukamatwa nyumbani kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar na vikosi vya serikali. Katika tamko la Misheni za Umoja wa Mataifa(In a statement, UNMISS), lilisema Sudan Kusini inaelekea ukingoni mwa kurejea kwenye vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe huku ghasia zikiongezeka na mivutano ya kisiasa inazidi kuongezeka. Pia "Kuna hofu kwamba Sudan Kusini inaweza kuingizwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan.”
Wito wa Papa Francisko wa amani
Papa Francisko alitoa maombi kadhaa ya amani kwa miaka mingi na hata alisafiri hadi Sudan Kusini kati ya Februari 3 na 5, 2023 ili kusaidia kuimarisha mchakato wa amani. Juma lililopita wakati baada ya tafakari ya Sala ya Malaika wa Bwana, Papa alirudi na wito unaogusa kwa ajili ya Sudan Kusini( touching appeal for South Sudan).
"Ninarudia wito wangu wa dhati kwa viongozi wote kufanya kila wawezalo kupunguza mvutano nchini. Ni lazima tuweke kando tofauti zetu na, kwa ujasiri na uwajibikaji, kuketi mezani na kushiriki mazungumzo yenye kujenga. Ni kwa njia hiyo tu itawezekana kupunguza mateso ya wapendwa wa Sudan Kusini na kujenga mustakabali wa amani na utulivu,” alisema Baba Mtakatifu.
Hata hivyo ombi la Papa la amani, katika miaka miwili iliyopita, limeenea hadi kwa jirani ya Sudan Kusini yaani Sudan, ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoharibu vimesababisha moja ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani yanayotokea hivi sasa.