"Hija ya matumaini,kiongozi na mwenzi katika safari,"Hati ya Baba Mtakatifu Francisko
Pamoja nasi, mwanahija wa matumaini, kiongozi na mwenzi katika safari ya kuelekea kwenye lengo kuu ambalo tunaitwa na Mbinguni, tarehe 21 Aprili katika Mwaka Mtakatifu wa 2025, saa 1:35 asubuhi, huku mwanga wa Pasaka ukimulika siku ya pili ya Oktava, Jumatatu ya Pasaka, Mchungaji mpendwa wa Kanisa Baba Mtakatifu Francisko alipita kutoka ulimwengu huu kwenda kwa Baba Mtakatifu. Jumuiya nzima ya Kikristo, hasa maskini, ilimsifu Mungu kwa zawadi ya huduma yake aliyoitoa kwa ujasiri na uaminifu kwa Injili na kwa Bibi-arusi la fumbo wa Kristo. Francisko alikuwa Papa wa 266. Kumbukumbu yake inabaki moyoni mwa Kanisa na wanadamu wote. Jorge Mario Bergoglio, aliyechaguliwa kuwa Papa tarehe 13 Machi 2013, alizaliwa Buenos Aires tarehe 17 Desemba 1936, kwa wahamiaji kutoka Piemonte: baba yake Mario alikuwa mhasibu, aliajiriwa kwenye sherika la reli, wakati mama yake, Regina Sivori, alitunza nyumba na elimu ya watoto wake watano.
Baada ya kufuzu mafunzo kama fundi kemikali, alichagua njia ya upadre, mwanzoni akaingia katika seminari ya jimbo na, tarehe 11 Machi 1958, akaendelea na kuwa mwanashirikia wa Shirika la Yesu. Alisomea masuala ya ubinadamu nchini Chile na, akirudi Argentina mwaka 1963, alihitimu katika falsafa katika Chuo cha Mtakatifu José huko Mtakatifu Miguel. Alikuwa profesa wa fasihi na saikolojia katika Chuo cha Moyo safi huko Mtakatifu Fé na katika Chuo cha Mtakatifu Salvador huko Buenos Aires. Alipata daraja la upadre tarehe 13 Desemba 1969 katika mikono ya Askofu Mkuu Ramón José Castellano, wakati tarehe 22 Aprili 1973 alifunga nadhiri za daima katika Shirika la Wajesuit. Baada ya kuwa Mwalimu wa wanovisi, Barilari huko Mtakatifu Miguel, baada ya kuwa profesa katika kitivo cha taalimungu, mshauri wa jimbo la Jumuiya ya Yesu na mkuu wa Chuo, tarehe 31 Julai 1973 aliteuliwa kuwa mkuu wa kanda ya kijesuit nchini Argentina.
Baada ya 1986 alitumia miaka kadhaa nchini Ujerumani kukamilisha tasnifu yake ya udaktari na, mara tu aliporejea Argentina, Kardinali Antonio Quarracino alimtaka kama mshirika wake wa karibu. Tarehe 20 Mei 1992 Mtakatifu Yohane Paulo II alimteua kuwa Askofu mkuu wa Auca na msaidizi wa Buenos Aires. Alichagua “Miserando atque eligendo” kama kauli mbiu yake ya kiaskofu na kuingiza neno la IHS Christogram, kama ishara ya Jumuiya ya Yesu, ndani ya nembo yake. Tarehe 3 Juni 1997, aliinuliwa kuwa Askofu Mkuu Mwandamizi wa Buenos Aires na, baada ya kifo cha Kardinali Quarracino, akamrithi mnamo tarehe 28 Februari 1998, kama Askofu Mkuu, na mkuu wa Argentina, wa kawaida kwa waamini wa Jimbo la Mashariki nchini humo, na Chansela Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki. Papa Yohane Paulo II alimuunda kuwa Kardinali katika mkutano wa tarehe 21 Februari 2001, kwa kupewa Kanisa la Mtakatifu Roberto Bellarmino. Oktoba iliyofuata alikuwa naibu mwandishi mkuu katika Mkutano Mkuu wa Kumi wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu.
Alikuwa mchungaji rahisi na aliyependwa sana katika Jimbo kuu lake, ambalo alisafiri mbali na mbali, hata kwa njia ya miguu hata kwa Basi. Aliishi katika ghorofa na kupika chakula chake cha jioni, kwa sababu alijisikia kama mmoja wa watu. Alichaguliwa kuwa Papa na Makardinali waliokusanyika kwenye mkutano wa huchaguzi (Conclave) baada ya kujiuzulu kwa Papa Benedikto XVI tarehe 13 Machi 2013 na kuchukua jina la Francisko, kwa sababu, kwa kufuata mfano wa mtakatifu wa Assisi, alitaka kuwa na moyo kwanza ya maskini wote duniani.
Akitokea katikati ya eneno la kutoa baraka, alijitambulisha kwa maneno haya: “Kaka na dada, habari za jioni! Safari ya udugu, ya upendo, ya uaminifu kati yetu." Na, baada ya kuinamisha kichwa chake, alisema: "Ninawaomba mniombee kwa Bwana anibariki: sala ya watu, wakiomba Baraka kwa Askofu wao." Tarehe 19 Machi, katika Sherehe ya Mtakatifu Yosefu, alianza rasmi huduma yake ya Mtume Petro. Daima akiwa makini na mdogo na wale waliokataliwa na jamii, Papa Francisko, mara tu alipochaguliwa, alichagua kuishi katika Nyumba ya Mtakatifu Marta (Domus Sanctae Marthae), kwa sababu hasingeweza kufanya kazi bila kuwasiliana na watu, na kutoka Alhamisi Kuu ya kwanza alitaka kuadhimisha Misa ya Karamu kuu ya Bwana akiwa nje ya Vatican, kwenda kila wakati kwenye magereza, vituo vya mapokezi kwa walemavu au watu wa madawa ya kulevya.
Alipendekeza kwamba mapadre wawe tayari daima kutoa sakramenti ya huruma, kuwa na ujasiri wa kuacha sakrestia ili kwenda kuwatafuta kondoo waliopotea na kuweka milango wazi ya Kanisa ili kuwakaribisha wale wanaotamani kukutana na Uso wa Mungu Baba. Alitumia huduma ya Mtume Petro kwa kujitolea bila kuchoka katika kupendelea mazungumzo na Waislamu na wawakilishi wa dini zingine, wakati mwingine akiwaita kwenye mikutano ya maombi na kutia saini matamko ya pamoja ili kupendelea maelewano kati ya washiriki wa imani tofauti, kama vile Hati ya Udugu wa Kibinadamu iliyotiwa saini tarehe 4 Februari 2019 huko Abu Dhabi na kiongozi wa Sunni al-Tayyeb. Upendo wake kwa maskini, wazee na watoto wadogo ulimsukuma kuanza Siku za Maskini, Mababu na Watoto Duniani. Pia alianzisha Dominika ya Neno la Mungu.
Zaidi ya watangulizi wake wote, alipanua Baraza la Makardinali, akiitisha Mabaraza kumi ambapo aliunda makardinali 163, kati yao 133 walikuwa wapiga kura na 30 wasio wapiga kura, wakitoka mataifa 73, na kati yao 23 walikuwa awajawahi kuwa na makardinali. Aliitisha Mikutano 5 ya Sinodi ya Maaskofu, 3 ya jumla ya kawaida, iliyojitolea kwa ajili ya familia, vijana na sinodi, isiyo ya kawaida tena kwa familia, na maalum kwa ajili ya Kanda ya Amazonia. Sauti yake imepazwa mara nyingi kuwatetea wasio na hatia. Wakati janga la Uviko-19 lilipoenea, jioni ya tarehe 27 Machi 2020, alitaka kusali peke yake katika uwanja wa Mtakatifu Petro.
Miaka ya mwisho ya kiti chake cha upapa iligubikwa na maombi mengi ya amani, dhidi ya vita vya tatu vya dunia vinavyoendelea hivi sasa katika nchi mbalimbali, hasa Ukraine, pamoja na Palestina, Israel, Lebanon na Myanmar. Baada ya kulazwa hospitalini mnamo tarehe 4 Julai 2021, ambapo alidumu kwa siku kumi, kutokana na upasuaji katika Hospitali ya Agostino Gemelli, Papa Francisko alirudi katika hospitali hiyo hiyo mnamo tarehe 14 Februari 2025 kwa kukaa kwa siku 38 kwa sababu ya nimonia ya pande mbili. Mara tu aliporudi Vatican alikaa juma za mwisho wa maisha yake huko nyumba ya Mtakatifu Marta, akijitolea hadi mwisho na kwa shauku sawa kwa huduma yake ya Mtakatifu Petro, ingawa alikuwa bado hajapona kabisa.
Mafundisho ya Papa Francisko yamekuwa tajiri sana. Shuhuda za mtindo wa kiasi na unyenyekevu, unaosimikwa katika uwazi kwa kazi ya kimisionari, ujasiri na huruma ya kitume, makini ili kuepuka hatari ya kujitafutia marejeo na mambo ya ulimwengu wa kiroho ndani ya Kanisa, Papa alipendekeza mpango wake wa kitume katika Waraka wa Evangelii gaudium yaani Furaha ya Injili (24 Novemba 2013). Miongoni mwa hati kuu, kuna nyaraka 4: Lumen fidei (Juni 29, 2013) ambayo inazungumzia mada ya imani kwa Mungu, Laudato si’ (24 Mei 2015) ambayo inagusa tatizo la ikolojia na wajibu wa jamii ya binadamu katika mgogoro wa tabia nchi, Fratelli tutti (3 Oktoba 2020) juu ya udugu wa kibinadamu na urafiki wa kijamii, Dilexit nos (Oktoba 24, 2024) juu ya kujitolea kwa Moyo Mtakatifu Zaidi wa Yesu.
Alitangaza Nyaraka 7 za Kitume, Katiba 39 za Kitume, Barua nyingi za Kitume, nyingi zikiwa katika mfumo wa Motu Proprio, Matangazao ya hati 2 za Miaka Mitakatifu, pamoja na Katekesi zilizopendekezwa katika Katekesi zake na Hotuba mbali mbalizilizotakwa katika sehemu mbalimbali za dunia. Baada ya kuanzisha kwa Baraza la Mawasiliano na Uchumi, na Baraza ka Walei, Familia na Maisha na Huduma ya Maendeleo ya Kibinadamu, aliifanyia marekebisho ya Kanisa la Roma kwa kutoa Uinjilishaji wa Katiba ya Kitume Praedicate (19 Machi 2022). Ilirekebisha mchakato wa kisheria wa kutangaza ubatili wa ndoa katika (CCEO na katika CIC (M.P. Mitis et misericors Iesus na Mitis Iudex Dominus Iesus) na kuifanya sheria kuwa kali zaidi kuhusu uhalifu uliofanywa na wawakilishi wa kazi dhidi ya watoto au watu walio katika mazingira magumu (M.P. Vos mundi estis). Papa Fransisko alimwachia kila mtu ushuhuda wa ajabu wa ubinadamu, wa maisha matakatifu na ubaba wa ulimwengu mzima.
CORPUS FRANNCISCI P.M