Tafuta

Papa Francisko akiwa anasali mbele ya Sanamu ya Bikira Maria wa Fatima 12 Mei 2017 Papa Francisko akiwa anasali mbele ya Sanamu ya Bikira Maria wa Fatima 12 Mei 2017 

Askofu Marini akumbuka maneno ya Papa Francisko kuhusu uhusiano wa kina na Mama Maria

Katika mahubiri ya kuombea Papa Fransisko,Askofu wa Tortona,Guido Marini aliyewahi kuwa Mshehereshaji wa maadhimisho yake ya liturujia za kipapa kwa miaka nane alisimulia imani na ushirikiano wa Papa wa Argentina.Moyo wa huruma na ubinadamu kuwa rohoni mwake.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Askofu Guido Marini wa Jimbo la Tortona, Italia wakati alikuwa ni Mshehereshaji mkuu wa Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa, alikuwa amependekeza kwa kiasi fulani kwa Baba Mtakatifu Francisko kuhusu Rozari ya dhahabu ili kuiweka katika sanamu ya Mama Yetu wa Fatima ambayo ilipitia kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro akiwa na wasi wasi, lakini alipouliza alisikia maneno ya Papa akimjibu: “kwa mama hatufanyi mahesabu.” Askofu Mkuu Marini aliyasema hayo wakati wa misa ya kuombea Papa iliyoadhimishwa tarehe 23 Aprili 2025 katika Kanisa kuu la Tortona. "Tunajua jinsi alivyojitolea kwa Mama Yetu  kwa hamu yake, ambayo pia imeoneshwa katika Wosia wake, ilikuwa kuzikwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, karibu na kikanisa cha Salus Populi Romani, ambako alikwenda mara nyingi wakati wa Upapa wake, kabla na baada ya kila safari na katika hali zingine nyingi,"  lakini Askofu Marini alitaka kukumbuka vipindi viwili hasa kuhusu hii.

Maria wa Fatima
Maria wa Fatima

"Tulikuwa mwanzoni mwa Upapa… na katika Uwanja wa Mtakatifu Petro walikuwa wameleta Sanamu ya Mama Yetu wa Fatima na Papa ilimbidi afanye ishara ya heshima na ilifikiriwa kuwa Papa afanye ishara hii, ya kuweka rozari mikononi mwa Mama Maria. Kwa hivyo nilianza kutafuta rozari, lakini sikupata chochote cha maana isipokuwa rozari nzuri sana, nzuri sana, ya dhahabu, na lazima niseme kwamba nilikuwa na aibu kidogo, pia kwa sababu tayari nilijua vizuri kwamba Papa alipenda mambo rahisi, maskini, lakini kulikuwa na muda kidogo, sikuwa nimepata kitu kingine chochote ambacho kilikuwa muhimu angalau kidogo. Nilimwendea Papa, nikasema Baba Mtakatifu, nilipata rozari… “Nzuri, nzuri, nzuri”, kisha nikaongeza kuwa ni rozari ya dhahabu. Nilikuwa tayari kusikia jibu la hapana, hapana, hapana, na badala yake akaniambia: "Ni sawa, ni sawa, kwa sababu kwa 'kwa Mama hatufanyi hesabu, rozari ya dhahabu ni sawa.' Akiwa bado anaendelea kuzungumzia  katika ibada ya kumuombea Papa Francisko, Askofu wa  Tortona aliongeza kusema hivi: “Wakati wa sherehe hiyo walibeba sanamu ya Maria mabegani kutoka kwenye obelisk hadi jukwaani, kisha walilazimika kupanda ngazi na kufika kwenye uwanja wa Kanisa. Wakati huo Papa alinigeukia wakati msafara uliobebea  Maria unasonga mbele kabla ya kupanda ngazi na kuniambia: "Njoo, njoo, njoo, kwa sababu tunakwenda kuelekea kwa Maria, hatufanyi sisi kusubiri." Kwa njia hiyo "Hii ni ibada ya kina, lakini pia rahisi, maarufu ya Baba Mtakatifu kwa Maria.”

Askofu Mariani aidha alitaja mada kuu ya Upapa, wake hasa ya huruma kwamba: “Nakumbuka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro liturujia ya kwanza ya toba ambayo Papa alikuwapo wakati wa Kwaresima. Kulikuwa na wakati ambapo yeye na mapadre wengine walikuwa wamekaa kwenye maungamo ili kusikia maungamo ya wale wote waliokuwepo na niliitwa kuandamana naye kwenye maungamo yake. Tulipokuwa karibu na kuungamisha kwake, yeye alibadili mwelekeo  ambao haikutarajiwa na  akasogea karibu na kituo kingine cha maungamo kilichokuwa karibu na hapo akapiga magoti mbele ya muungamishi ambaye alishangaa, na akafanya ungamo lake hapo, ili kila mtu amwone. Kisha, wakati tukiwa ndani ya Sakrestia  aliniambia: "Samahani ikiwa sikukusikiliza, nilikwenda kwa njia nyingine, lakini nilitaka ishara hii ya Papa kusaidia kila mtu kuelewa uzuri wa kuungama, kuelewa uzuri wa huruma ya Mungu, kuelewa jinsi ilivyo kweli sababu ya furaha kumkaribia Bwana na kuomba msamaha.”

Papa aliungamisha na aliungama
Papa aliungamisha na aliungama

Kuhusu shangwe hiyo ya Injili iliyotoa Waraka wake wa kitume wa Papa wa Argentina, Askofu Marini alisema: “Wakati mmoja alisema hivi: ‘Unaona, napenda sana kwenda miongoni mwa watu nikiwa na tabasamu midomoni mwangu, labda nyakati fulani kwa kufanya ishara fulani ya pekee, kwa sababu ninataka kuwasilisha furaha ya Bwana, ninataka kila mtu aweze kugusa kwa mikono yake, kwamba maisha ya Injili ni ya kweli. Hii hapa ni furaha ya Injili, furaha ya Yesu." Kisha askofu alikumbuka neno lile la "Todos" lililorudiwa mara tatu kwenye Siku ya Vjana  Duniani (WYD) ya mwisho huko Lisbon: "Todos, todos, todos, yaani 'wot, wote, wote'. 

Papa na vijana Lisbon
Papa na vijana Lisbon

Je iliimanisha nini? ni kwamba Kanisa haliwezi kujizuia kuwa moyoni mwake na hamu ya kuwafikia wote, kuwasikiliza wote, kuingia katika mazungumzo na wote, kuleta uzuri wote wa Injili inayookoa, na ya Bwana ambaye ni Mwokozi." Kisha askouf Marini alitaja sinodi: "Tumehusika katika safari hii ya sinodi, safari ambayo Papa kwa kukazia alitaka na anataka, yeye binafsi aliniambia hivyo mara kadhaa, sivyo nyaraka kadhaa kwamba: "Sipendezwi na hati mpya zinazofanywa, ninavutiwa zaidi ya yote wakati huu, safari hii inatusaidia sisi sote kuishi katika ushirika wenye maana zaidi, wa kweli, wa kina zaidi, ushiriki, uwajibikaji wa pamoja, kuwa kweli mwili mmoja, pia kwa sababu, Papa alijua vyema, utume unafikiwa pale tu ambapo kuna ushirika na ni upendo tu  wa ndani ya Kanisa, na kwa ushirika ndani ya Kanisa.”

Kuhusu upendo wa Papa kwa maskini, Mshereheshaji wa zamani wa Maadhimisho ya Kipapa alisema: “Maskini walikuwa moyoni mwake, alikuwa na mahitaji yote ya ubinadamu moyoni na haikuwa pozi. Siku moja katika sakrestia baada ya mkutano na baadhi ya watu maskini nilimwona akilia na alilia kwelikweli, kwa sababu alihisi umaskini wa mwanadamu katika hali zake zote kama maumivu yake mwenyewe, maumivu ya kibinafsi yaliyogusa moyo wake. Kiukweli alilia kwa machozi katika usiri wa mtakatifu, akikumbuka mkutano aliokuwa nao na mmoja wa watu hawa maskini na siku chache baada ya kuchaguliwa kwake kuwa Papa tulikwenda kwenye gereza la watoto. Nakumbuka kwamba kabla ya misa alisema hivi: "Unajua kwamba kila wakati ninapokuja kwenye mojawapo ya maeneo kama haya najiuliza kwa nini wao na sio mimi? Ningeweza kuwa huko. Na akaniambia: "Fikiria juu yake."

Papa Francisko mara kadhaa alikwenda magereza
Papa Francisko mara kadhaa alikwenda magereza   (ANSA)

Tena, Askofu Marini alitaja ahadi yake ya amani, kama nabii ambaye mara nyingi hasikiki, ambaye "hakuchoka kuitangaza, kuitangaza, akiiomba kama zawadi kwa ubinadamu wetu maskini vitani." Mchungaji ambaye aliupenda ulimwengu kwa shauku na jambo moja ambalo limenigusa kila mara ni kwamba alipendezwa na kila kitu, katika kila kitu, kwa sababu kila kitu kilichomhusu mwanadamu kilimvutia, maonesho yote ya ubinadamu yalimvutia, kila kitu kilichokuwa na uhusiano na mwanadamu kilikuwa moyoni mwake na alikiweka moyoni. Alitaka kuwa… kidogo kama Paroko wa parokia ya ulimwengu, lakini fikirieni simu alizopiga kwa watu wa kawaida au salamu alizotuma kila sehemu ya dunia. Alikuwa na ulimwengu moyoni mwake na labda kipengele hiki cha upapa kiliwekwa wazi mara moja na kwa wote katika historia mnamo tarehe 27 Machi 2020, mwaka wa Uviko -19 , wakati Papa alionekana peke yake katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Macho ya ulimwengu yalikuwa katika uwanja huo, macho ya ulimwengu yalikuwa kwa Papa na Papa wakati huo alimpelekea ulimwengu wote pamoja naye mbele ya Bwana. Labda hiyo itabaki kuwa sura nzuri zaidi ya Papa ambaye kweli  ndani ya  moyo wake alikuwa na ulimwenguni daima."

Tarehe 27 Machi 20220 Papa alisali peke yake katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Tarehe 27 Machi 20220 Papa alisali peke yake katika Uwanja wa Mtakatifu Petro

Hatimaye, Askofu wa Tortona alikumbuka “ujasiri na uhuru” wa Papa Fransisko: “Alitaka kuchangia mageuzi ya Kanisa. Kanisa katika kila kipindi cha historia linahitaji kurekebishwa katika mwelekeo wake wa kibinadamu. Kwa nini? Kwa sababu wakati hutokeza miunganisho, mifumo mingine  haifanyi kazi tena inavyopaswa kuwa. Kwa ujasiri na uhuru alijaribu kutoa mchango wake katika mwelekeo huu. Na hakika hii pia ilimfanya akaribishwe kila wakati. Siku ya sherehe yake ya kwanza ya kuanza kuwa Papa mnaweza kufikiria shangwe iliyokuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Tukirudi kwenye sakrestia, fikiria kile alichosema: “Unaona leo shangwe hii ya watu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ilinifanya nifikirie juu ya kuingia kwa Yesu Yerusalemu. Na kisha mara baada ya kuwaza na nikajisemea kumbuka hili wakati siku za Mateso na Msalaba zitakapokuja." Na ndivyo ilivyokuwa. Kwa sababu ndivyo ilivyo kwa Mapapa wote.

 

29 Aprili 2025, 11:47