Tafuta

Mtakatifu Maria Mkuu,masifu ya jioni ya makardinali na sala za watu kwa ajili ya Papa

Jioni ya Dominika 27 Aprili 2025 kulikuwa na maandamano ya Makardinali,waliofika katika Mikutano mikuu kwa mtazamo wa uchaguzi baada ya kifo cha Papa Francisko, walitembelea kaburi la Papa na kuadhimisha Masifu ya pili ya jioni,yaliyoongozwa na Kardinali Makrickas.Zaidi ya watu elfu 20 wamekuwa kwenye foleni tangu asubuhi ya leo ili kumsalimia Papa,kusali mbele ya jiwe lake la kaburi na kutoa heshima za maua katika kaburi hilo.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Katika Dominika ya Pili ya Pasaka, ambayo ni Dominika ya Huruma ya Mungu, tarehe 27 Aprili 2025, washiriki wa Baraza la Makardinali walikwenda kwenye Kanisa kuu la Kipapa la Mtakatifu Maria Mkuu kutoa heshima zao kwa Baba Mtakatifu Francisko kwenye kaburi lake lililofunguliwa kwa umma tangu saa 1 asubuhi ya leo.

Makardinali wakitoa heshima katika kaburi la Papa
Makardinali wakitoa heshima katika kaburi la Papa   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)
Makardinali wakitoa heshima
Makardinali wakitoa heshima   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)
Makardinali wakitoa heshima
Makardinali wakitoa heshima   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kisha walikusanyika kwa pamoja katika masifu ya pili ya jioni, yaliyoongozwa na Mkuu wa Kanisa la hilo, Kardinali Rolanda Makrickas.

Masifu ya jioni
Masifu ya jioni   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)
Masifu ya jioni
Masifu ya jioni   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Nyuma yao, kulikuwa na makundi ya wamini walijumuika, huku wengine wakiendelea kuwasili wakati wa sherehe hizo kwa ajili ya kutoa heshima zao kwa Papa Francisko. Takriban watu elfu ishirini walikuwa tayari wametembelea kaburi hilo tangu asubuhi na mapema.

Nyuma ya makardinali makundi ya waamini
Nyuma ya makardinali makundi ya waamini   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Waamini wakitoa heshima

Mwamini akitoa heshima katika kaburi ya Papa
Mwamini akitoa heshima katika kaburi ya Papa   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)
Kutoa heshima katika kaburi la Papa Francisko
Kutoa heshima katika kaburi la Papa Francisko   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)
27 Aprili 2025, 19:49