Rais Mattarella alisali mbele ya jeneza la Papa katika kikanisa cha Mtakatifu Marta
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella alikaa kimya kwa muda mfupi mbele ya jeneza lenye mwili wa Papa Francisko, kwa kuona Papa ambaye alikuwa amejenga uhusiano wa heshima na urafiki kwa miaka mingi na ambaye tarehe 21 Aprili, katika ujumbe kwa bjia ya video uliotolewa na Ikulu wakati wa kifo chake, alifafanua Papa Francisko kama hatua ya kumbukumbu naye. Kwa njia hiyo Mkuu wa Nchi ya Italia hakika alikwenda Nyumba ya Mtakatifu Marta katika kikanisa hicho akifuatana na binti yake Laura, kutoa heshima kwa papa aliyekufa ambaye alikuwa amelaza kwenye kikanisa hicho. Kikanisa maarufu ambacho ulimwengu ulikitambua kupitia Misa za kila siku zilizoadhimishwa katika miaka ya kwanza ya upapa wake na, zaidi ya yote, wakati wa karantizi za uviko.
Kuanzia saa 3.00 usiku Aprili 21 na kuamkia Aprili 22 hadi usiku wa manane, msururu mrefu wa watu ulibadilishana kwa zamu katika eneo la Nyumba ya Papa Francisko alipoamua kuishi. Ni wafanyakazi wa Vatican wakiwa na familia zao, kisha baadhi ya makardinali, washirika wa karibu zaidi na pia rais wa Seneti, Ignazio La Russa, Meya wa Roma, Roberto Gualtieri, mkuu wa kiyahudi wa Roma, Riccardo Di Segni, na rais wa Jumuiya ya Wayahudi ya Roma, Victor Fadlun walifika kutoa heshima zao.
Barua ya Papa katika siku za operesheni ya rais
Kwa njia hiyo Rais Mattarella, baada ya kupata nafuu kutokana na upasuaji katika siku za hivi karibuni katika hospitali ya Kirumi ya ‘Santo Spirito’ ili kupandikiza kipima moyo. Operesheni ambayo ilifanikiwa na ambayo Papa, alikuwa huko Mtakatifu Marta wakati huo, aliarifiwa. Jorge Mario Bergoglio alitaka kujiweka pamoja na Rais Mattarella kwa kumtumia barua - hadi sasa ambayo haijachapishwa, iliyotiwa saini tarehe 16 Aprili ambayo, kama tunavyosoma, alionesha "ukaribu wa kindani unaoambatana na sala ili ahisi kuungwa mkono na upendo wa wale wanaokuza pongezi kwak kwa utumishi wake usio na kuchoka kwa Italia. Kadhalika: "Mheshimiwa Rais, kwa kuunganishwa na hali tete inayoashiria msimu huu wa maisha yetu, tunaalikwa kutopoteza matumaini na kuamini uwepo wa upendo wa Mungu na utunzaji wa wale wanaotujali," Papa aliandika. Na katika mkesha karibu na Pasaka, aliomba baraka zake, akimtakia rais "Pasaka njema na ahueni ya haraka."