Mazishi ya Papa Francisko:Hatua ya mwisho ya kulaza mwili kaburini
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jeneza na Papa Francisko limewasili Jumamosi tarehe 26 Aprili 2025 kwenye kilima cha Esquiline na kuwekwa kwenye kaburi ndogo kabisa kati ya mabasilika manne ya kipapa, la kipekee lililowekwa wakfu kwa ajili ya Bikira, na la zamani zaidi lililopewa jina la kale katika Ukristo wa Magharibi, kwa ajili ya maziko baada ya Misa ya mazishi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican na kufikishwa katika Kanisa Kuu la Bikira maria Mkuu, mahali hapo ambapo kwa moyo wote na maandishi, Baba Mtakatifu Francisko alipenda sana katika maisha ya utume wake. Kwa hakika leo ilikuwa ni mwanga uliochanganyikana na maumivu. Ni hakika kwa chachu ya wema iliyopandwa katika pembe za dunia, wema uliofurika. Papa Francisko anabakia kuwa kichocheo kwa vijana na kubaki mwamko kwa vijana ambao kwa neema ya Mungu walikuwa wameunganika kwa ajili ya Jubilei yao na ambayo inabaki katika wazee ambao wamedhoofika kwa miaka, katika wafanyakazi wa upendo ambao wanaweza kuendelea kumtazama Bwana wa kusikiliza, huruma ikiwakaribisha.
Kila mahali yeye amekuwa ni Papa wa maskini. Na kwa namna ya pekee na ya kupendelea walikuwa ni masikini waliokaribisha kuwasili kwa jeneza kwenye Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu. Takriban watu arobaini kati yao, wote wamepangwa kwenye uwanja wa Kanisa, kila mmoja akiwa na waridi jeupe, walitoa heshima kwa “baba" yao. Hawa walikuwa ni maskini, wasio na makazi, wafungwa, na wahamiaji. Waliunda mduara kuzunguka jeneza. Maua yaliyokusanywa na watoto wanne ambao waliingia pamoja na wasimamizi wa sherehe za mazishi ya kibinafsi. Makofi bila kukatizwa kutoka kwa mahujaji karibu na Uwanja wa kanisa ambao baadaye watasali Rozari usiku. Dominika tarehe 27 Aprili 2025 katika Dominika ya Huruma ya Mungu Baraza la Makardinali watafika kuadhimisha Ibada ya Pili ya Dominika ya Huruma ya Mungu katika wakati ambao Papa Francisko ameingia katika nyumba yake milele.
Kwa hiyo hili ni Kanisa ambalo Mtakatifu Ignatius wa Loyola, mwanzilishi wa Shirika la Yesu, aliadhimisha misa yake ya kwanza usiku wa Noeli mwaka 1538, lililomkaribisha Papa Mjesuit ambaye atapumzika hapo kwa mapenzi, Papa wa kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 120 kwa kuchagua kuzikwa nje ya Vatican. Kwa njia hiyo “Francis ameweza kuendelea katika mapokeo ya Kanisa, akiyasasisha katika roho ya nyakati,” aliyasema hayo mtawa wa Wabenediktini wa Vallombrosa, mwenye asili ya Brazili, Padre Pedro Savelli, msimamizi wa Basilika Mtakatifu Praceda hatua chache kutoka kwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu.
Kwa njia Papa Francisko amekuwa Papa wa nane kuzikwa hapo, karibu na Papa Honorius III, Papa ambaye alitoa sheria iliyotiwa muhuri kwa Wafransiskani. Amezikwa kwenye kaburi lililowekwa kwenye ukuta wa kushoto, kati ya kikanisa cha Pauline na Kikanisa cha (Sforza) chenye kaburi la Makadinali Guido Ascanio Sforza wa Mtakatifu Fiora na Alessandro Sforza. Mnamo 1562, ndugu hao wawili walifanikiwa kumhusisha Michelangelo mwenye umri wa miaka 87 katika mpango huo. Michelangelo alipokufa, kazi iliendelea chini ya uongozi wa Tiberio Calcagni na Giacomo della Porta, ambao walitengeneza makaburi ya pembeni, kuvikwa taji na malaika wa tarumbeta. Kwa hiyo basi Nuru ya leo inachonga ukuu wa mahali hapo patakatifu ambapo Jorge Mario Bergoglio alikwenda mara 126 katika ibada yake ya Maria mbele ya Picha ya Salus Populi Romani, au Afya ya Waroma.