Tafuta

Dominika ya Huruma ya Mungu,Kard Parolin:Huruma pekee huponya na kuunda ulimwengu mpya

Baba Mtakatifu Francisko alikuwa ni shuhuda angavu wa Kanisa linaloinama kwa huruma kwa wale waliojeruhiwa na kuwaponya kwa mafuta ya huruma.Alitukumbusha kwamba hapawezi kuwa na amani bila kuwatambua wengine,bila kuwajali wale walio dhaifu;zaidi hapawezi kuwa na amani ikiwa hatutajifunza kusameheana kwa kutumia huruma ile ile aliyonayo Mungu katika maisha yetu.Ni katika mahubiri ya Kardinali Parolin katika Dominika ya Huruma ya Mungu,Aprili 27.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Pietro Parolin, aliyekuwa Katibu wa Vatican wakati wa mahubiri yake alitoa muhtasari wa Upapa wa Papa Fransisko, wakati wa misa aliyoiongoza katika siku ya pili ya misa 9 (Novendiali) kwa ajili ya Papa ambayo imeudhuriwa na watu 200,000. Kardinali Parolini kwa hiyo alisema “Ni huruma pekee inayoponya na kuunda ulimwengu mpya, kuzima moto wa kutoaminiana, chuki na vurugu na  hili ndilo fundisho kuu la Baba Mtakatifu Francisko.”  “Upendo wetu kwake, unaojidhihirisha katika masaa haya, haupaswi kubaki hisia rahisi ya wakati huu, na hivyo Kardinali  Paroli alitoa mwaliko, pamoja na heshima kwa idadi kubwa ya vijana waliokuwapo uwanjani, pamoja na wafanyakazi na waamini wa Jiji la Vatican.

Misa ya 27 Aprili 2025
Misa ya 27 Aprili 2025   (Vatican Media)
27 Aprili 2025, 19:30