Tafuta

2025.04.23 Mazungumzo ya Dk. Bruni  Msemaji wa Vyombo vya habari na waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa II Mkuu wa Makardinali. 2025.04.23 Mazungumzo ya Dk. Bruni Msemaji wa Vyombo vya habari na waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa II Mkuu wa Makardinali. 

Mkutano wa II wa Makardinali:ratiba ya misa 9 za kuombea Papa imeanzishwa

Ratiba ya Maadhimisho ya Ekaristi Takatifu kwa ajili ya kuombea Papa imeanzishwa,kuanzia na Misa ya mazishi ya Papa itakayofanyika tarehe 26 Aprili saa 4.00 kamili asubuhi.Ofisi ya Habari Vatican,imefahamisha kuwa saa 1.30 jioni takriban waamini elfu 20 wakuwa tayari wametoa heshima yao kwa Papa Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Vatican News.

Makardinali 103 walishiriki katika Mkutano Mkuu wa pili,  tarehe 23 Aprili 2025, ulioanza saa 11:00 jioni na kumalizika saa 12:30 jioni masaa ya Ulaya katika Ukumbi wa Sinodi, mjini Vatican, na kuidhinisha Ratiba ya  (Novendiali,) yaani siku 9 za maadhimisho ya Ekaristi kwa ajili  ya Papa, kuanzia na Misa ya mazishi, tarehe 26 Aprili saa 4:00 asubuhi, saa za Ulaya ikiwa ni saa 5 asubuhi za Afrika Mashariki na Kati. Liturujia ziko wazi kwa wote, lakini kwa ushiriki, kila siku, kwa kikundi tofauti, kwa kuzingatia uhusiano wake na Papa wa Roma.

Waandishi wa habari wakipokea taarifa za mkutano wa II wa Makardinali
Waandishi wa habari wakipokea taarifa za mkutano wa II wa Makardinali

Katika taarifa iliyochapishwa na Ofisi ya vyombo vya habari usiku huu,  imebainishwa kwamba: "aina hii ya makusanyiko inaonesha, kwa namna fulani, upeo wa huduma ya Mchungaji mkuu na umoja wa Kanisa la Roma."

Ofisi ya Vyombo vya habari vile vile iliripoti kwamba makardinali hao katika mkutano huo walianza kwa sala ya (Veni, Sancte Spiritus), yaani Uje Roho Mtakatifu na kisha maombi kwa ajili ya Papa Francisko na ndipo makardinali wengine ambao walikuwa bado hawajafanya hivyo walikula kiapo.

Kardinali Rugambwa akiwa anasali
Kardinali Rugambwa akiwa anasali   (Vatican Media)

Imethibitishwa tena kuwa maadhimisho ya misa tisa zitafanyika kwa njia ifuatayo:

Siku ya 2: Dominika tarehe 27 Aprili, saa 4.30 asubuhi, kwenye Uwanja wa Basilika ya Vatican: watakuwa ni wafanyakazi na waamini wa Jiji la Vatican. Misa hiyo itaongozwa na Mwadhama Kardinali Pietro Parolin, aliyekuwa Katibu wa Vatican.

Siku ya 3: Jumatatu tarehe 28 Aprili, saa 11.00 jioni, katika Basilika ya Vatican: Kanisa la Roma. Maadhimisho hayo yataongozwa na Mwadhama Kardinali Baldassare Reina, Makamu wa Baba Mtakatifu  wa Jimbo Kuu la Roma.

Siku ya 4: Jumanne tarehe 29 Aprili, saa 11.00 jioni, katika Basilika ya Vatican: Watu wanaaohusika na shughulizi za Basilika za Kipapa. Maadhimisho hayo yataongozwa na Mwadhama Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Kanisa kuu la Kipapa la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Siku ya 5: Jumatano tarehe 30 Aprili, saa 11.00 jioni, katika Basilika ya Vatican: Kikanisa cha Kipapa. Maadhimisho hayo yataongozwa na Mwadhama Kardinali Leonardo Sandri, Makamu Dekano wa Baraza la Makardinali.

Siku ya 6: Alhamisi  Mei Mosi, saa 11.00 jioni, katika Basilika ya Vatican: Curia Romana. Misa  hiyo itaongozwa na Mwadhama Kardinali Kevin Joseph Farrell, Camerlengo wa Kanisa Takatifu la Roma.

Siku ya 7: Ijumaa tarehe 2 Mei, saa 11.00 jioni, katika Basilika ya Vatican: Makanisa ya Mashariki.  Misa hiyo itaongozwa na Mwadhama Kardinali Claudio Gugerotti, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la  Makanisa ya Mashariki.

Siku ya 8: Jumamosi tarehe 3 Mei,saa  11.00 jioni katika Kanisa Kuu la Vatican: Wahusika wa Baraza la Kipapa Maisha ya Wakfu na vyama vya Kitume. Maadhimisho haya yataongozwa na Mwadhama Kardinali Ángel Fernández Artime, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maisha ya Wakfu na Vyama vya Kitume.

Siku ya 9: Dominika tarehe 4 Mei, saa11.00 jioni, katika Basilika ya Vatican: Wahusika wa Kikanisa cha Kipapa. Misa hiyo itaongozwa na Mwadhama Kardinali Dominique Mamberti, Shemasi wa Baraza la Makardinali.

Mkutano wa makardinali
Mkutano wa makardinali   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Mkutano Mkuu ujao utafanyika kesho asubuhi saa 3.00 kamili saa za Ulaya na saa 4 .00 kamili saa za Afrika mashariki na Kati.

Msururu Mkubwa wa kutoa heshima kwa Papa Francisko
Msururu Mkubwa wa kutoa heshima kwa Papa Francisko   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Ofisi ya Vyombo vya Habari iliripoti kwamba kuanzia saa 5.00 asubuhi hadi takriban 1:30 usiku, karibu watu elfu 20 walitoa heshima kwa mwili wa Papa Francisko na kwamba takriban maombi 4000 ya kuomba kibali yalipokelewa kutoka kwa waandishi wa habari.

Msurur kwa ajili ua kutoa heshima kwa Papa Francisko
Msurur kwa ajili ua kutoa heshima kwa Papa Francisko   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)
Msururu katika Kanisa Kuu kwa ajili ya kutoa heshima
Msururu katika Kanisa Kuu kwa ajili ya kutoa heshima   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)
23 Aprili 2025, 22:00