Papa Francisko:Kristo ni tumaini lisilo zama,ni mustakabali wa historia!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Misa ya mkesha wa Pasaka, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 19 Aprili 2024, imeongozwa na Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Baraza la Makardinali, aliyechaguliwa na Baba Mtakatifu kuongoza sherehe hizi. Katika Ibada ya misa iliudhuriwa na makardinali 34, maaskofu 24 na mapadre 260, watawa wa kike na kiume na waamini walei. Baba Mtakatifu Francisko, hata hivyo alifika katika Basilika, kabla ya kuanza kwa Liturujia kwa muda wa sala na kuwa karibu na waamini ambao wangeshiriki, kwa hivyo alikuwa nao kiroho. Na zaidi ya hayo kwa sababu ya mahubiri yake aliyotarisha na kusomwa na Kardinali Re. Baba Mtakatifu, katika mahubiri hayo anabainisha kuwa: “Ni usiku wakati Mshumaa wa Pasaka unaendelea kuwaka polepole hadi Altareni. Ni usiku ambapo wimbo unafungua mioyo yetu katika furaha, kwa sababu ardhi imengazwa na mwana mkuu: nuru ya Mfalme Milele aliyeshinda giza la Ulimwengu. Kabla ya kumalizika usiku, Injili inasimulia matukio ambayo yalisomwa ( Lk 24,1-12): Mwanga wa Mungu wa Ufufuko, unawashwa na Pasaka ya Bwana inatokea wakati, jua linapoanza kuchomoza: katika miale ya kwanza ya asubuhi, jiwe kubwa lilionekana, katika Kaburi la Yesu, ambalo liliviringishwa na baadhi ya wanawake walifika katika mahali hapo wakiwa wamevalia shela za maombolezo. Giza liliwafunga la kutokuwa na uhakika na hofu ya mitume. Yote hayo yalitokea katika usiku
Kardinali Re akiwalekea waamini waliofika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, aliendelea kusoma mahubiri ya Papa akibainisha kuwa “Mkesha wa Pasaka unatukumbusha kwamba nuru ya Ufufuko iliangaza safari, hatua kwa hatua, ikavunja giza la historia bila ghasia, ikaangaza katika mioyo yetu kwa namna nyeti. Na hii inafanana na imani nyenyekevu, isiyokuwa na kila aina za kutafuta ushindi. Pasaka ya Bwana siyo tukio la kitamasha ambalo Mungu anajithibitisha mwenyewe na kulazimisha kuaminiwa Yeye; siyo hatima ambayo Yesu anafikia kwa njia rahisi, akizungukia Karvari; na wala sisi hatuweze kuiishi kwa namna ya kawaida na bila kusitasita ndani. Kinyume chake, Ufufuko ni sawa na vichipukizi vidogo vya mwanga ambavyo vinafanya njia kidogo kidogo, bila kufanya ghasia, wakati mwingine kwa kutishiwa usiku na kutoamini.
Mtindo huu wa Mungu unatukomboa dhidi ya udini wa kijuu juu, udanganyifu wa kufikiria kuwa ufufuko wa Bwana unasuruhisha yote kama viini macho. Hiki nii kitu kingine: hatuwezi kusheherekea Pasaka bila kuendelea kuwa na utambuzi wa giza ambalo tunabeba moyoni na vivuli vya vifo ambavyo mara nyingi vinaongezeka ulimwenguni. Baba Mtakatifu anabainisha kwamba Kristo alishinda dhambi na kuharibu kifo, lakini katika historia yetu ya duniani, nguvu hizi za Ufufuko wake zipo bado zinatimizwa. Na utumizo huo, kama kichupikizi kidogo cha mwanga tumekabidhiwa sisi, kwa sababu tuweze kutunza na kufanya kukua. Kaka na dada, huu ni wito ambao hasa katika mwaka wa Jubilei tunapaswa kuhisi kwa nguvu ndani mwetu: tufanye kichipue matumaini ya Pasaka katika maisha yetu na katika Ulimwengu.
Tunapohisi bado uzito wa kifo ndani ya moyo wetu, tunapoona vivuli vya ubaya kuendelea katika njia za ghasia ulimwenguni, tunaposikia kuungua mwilini mwetu, na katika jamii majeraha ya ubinafsi, au vurugu, tusife moyo, turudi katika tangazo la usiku huu: nuru inayoangaza polepole hata kama tumo kwenye giza; tumaini la maisha mapya na ya ulimwengu ambao hatimaye umekombolewa unatusubiri: mwanzo mpya ambao unaweza kutushangaza, licha ya kufikiri kuwa haiwezekani, kwa sababu, Kristo alishinda kifo. Tangazo hili, ambalo linapanua moyo linatujaza matumaini. Katika Kristo mfufuka, kiukweli tuna uhakika kwamba historia yetu binafsi na safari ya ubinadamu, licha ya kukumbwa bado na giza, mahali ambamo mianga inaonesha kuzimwa, imo mikononi mwa Mungu; na Yeye, katika upendo wake mkuu, hatuachi kuyumbayumba na hataruhusu ubaya uwe na neno la mwisho. Na wakati huo huo, matumaini haya, tayari yameshatimizwa katika Kristo, kwa hiyo kwetu sisi inabaki hata hatima ya kufikia: na sisi tulikabidhiwa ili tuweze kuwa mashuhuda aminifu na kwa sababu Ufalme wa Mungu ufungue njia katika mioyo ya wanawake na wanaume wa leo hii.
Baba Mtakatifu katika mahubiri hayo yaliyosomwa alikazia kubainisha kuwa “kama mtakatifu Agostino anavyotukumbusha kuwa: “ ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo unadhihirisha maisha mapya kwa wale wamwaminio: na fumbo hili la kifo chake na fufuko mnampaswa kuujua ninyi katika ukina na kulitafakari katika maisha yenu(Hotuba 231,2). Ni kuzaliwa tena Pasaka katika maisha yetu na kugeuka kuwa wajumbe wa matumaini, wajenzi wa matumaini wakati pepo nyingi za kifo zinavuma bado juu yetu.
Tunaweza kufanya kuwa maneno yetu, kwa ishara zetu dogo za kila siku, kwa chaguzi zetu zinazohuishwa na Injili. Maisha yetu yote yanaweza kuwa uwepo wa matumaini. Tunataka kuwa kwa wasio na imani katika Kristo, kwa wale waliopoteza njia, kwa ajili ya waliojiuzulu, au ambao migongo yao imeinama kwa sababu ya uzito wa maisha: kwa waliopeke yao au wamejifungia katika huzuni zao: kwa ajili ya maskini na waliokandamiza na dunia; kwa ajili ya wanawake walionyenyekezwa na kuuawa: kwa ajili ya watoto ambao hawakuzaliwa katu, na wale ambao wanateswa; kwa ajili ya waathirika wa vita. Kwa kila mmoja na kwa wote tunawapelekee matumaini ya Pasaka!
Katika hilo Papa ameongeza: “Ninapenda kukumbusha mwanaibada kuu wa miaka ya 200, Hadewijch wa Anversa ambaye kwa kuhuishwa na Wimbo ulio bora na kufafanua mateso kwa sababu ya kumkosa mpendwa aliimba kiitikio cha upendo kwa sababu anasema: “Kuwepo mageuzi katika giza langu (HADEWIJCH, Poesie Visioni Lettere, Genova 2000, 23). Kristo Mfufuka na ni hatua ya mwisho ya kugeuka ya historia ya kibinadamu. Yeye ni tumaini lisilozama. Yeye ni upendo ambaye anatusindikiza na kutusaidia. Yeye ni mustakabali wa historia, hatima ya mwisho kuelekea mahali tunapoelekea, ili kuweza kukaribishwa katika maisha yake mapya ambayo Bwana mwenyewe atafuta kila chozi, hapatakuwapo mauti, wala maombolezo wala kilio, wala maumivu(Uf 21,4). Na hili ni tumaini la Pasaka, ni hatua ya kugeuka gizani” kwa hiyo tunapaswa kuwatangazia wote.
Dada na Kaka katika kipindi cha Pasaka, ni wakati wa matumaini, Papa amekazia. “Bado kuna hofu, bado kuna huzuni wa dhamiri ya dhambi, lakini pia kuna nuru inayovunja.(…) Pasaka inaleta habari njema ambayo ingawa mambo yanaonekana kuwa mabaya zaidi duniani, ubaya tayari umeshindwa. Pasaka inaturuhusu kuthibitisha kwamba ingawa utafikiri Mungu yuko mbali na sisi, lakini tunabaki kuvutwa na hali halisi ndogo, kwamba Bwana wetu anatembea njiani na sisi(…). Kuna miale mingi ya matumaini ambayo yanatupa nuru katika njia ya maisha yetu(H. NOUWEN, Preghiere dal silenzio. Il sentiero della speranza, Brescia 2000, 55-56). Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu anatushauri kuwa “ tutengeneza nafasi ya mwanga wa Mfufuka! Na tutakuwa wajenzi wa matumaini kwa ajili ya ulimwengu.”