Tafuta

Papa Francisko alikwenfa Alessano kutoa heshima katika jimbo la Lecce,kwenye kaburi la Don Tonino Bello,mnamo 2018. Papa Francisko alikwenfa Alessano kutoa heshima katika jimbo la Lecce,kwenye kaburi la Don Tonino Bello,mnamo 2018.  (LUIGI MAURAMATII)

Tumaini linafungua dirisha katika uzima wa milele la maisha ya mwanadamu!

Tunachapisha dibaji ya Papa Francisko ya kitabu cha Padre Tommaso Giannuzzi chenye kichwa:"Manabii wa matumaini.Don Tonino Bello na Papa Francisko.”Katika kitabu hicho Padre wa Salento anachukua maneno Papa wa Argentina na Askofu wa Molfetta ili kutafuta njia ya kutoa uso wa fadhila za matumaini,kisima kinacho bubujika katika moyo wa mwanadamu.

Papa Francisko

Miongoni mwa maswali mengi ambayo mwanadamu amejiuliza katika kipindi chote cha historia, moja zaidi ya yote siku zote limepata jibu lisilo na uhakika, lakini ambalo linaweza kutuwezesha kulikabili tukio ambalo kutokana na hilo swali la awali linatokea, yaani, maisha baada ya kifo; itakuwaje kwa mwanadamu baada ya kufa? Itakuwaje kwangu? Sote tunafahamu kwamba hakuna anayeepuka fumbo la kifo na kwamba maswali mengi yanayotokana na tukio hili hayawezi kushindwa kutilia shaka fadhila hiyo ambayo, zaidi ya mengine, inamruhusu kila mwanamume na mwanamke kutazama zaidi ya mipaka ya mwanadamu yaani: matumaini! Kwa sababu matumaini ni maisha, ni kuishi, yanatoa maana ya safari, ni kutafuta sababu za kusonga mbele kwa kuhamasisha maana ya kuwepo kwetu, ya sasa, ya kuwepo kwetu hapa, sasa. Katekisimu ya Kanisa Katoliki inaeleza jinsi gani fadhila ya kitaalimungu ya matumaini inavyosimikwa katika neno la Yesu, ikisema kwamba:

“Tumaini la Kikristo ni fadhila ya kitaalimungu ambayo kwayo tunatamani ufalme wa mbinguni na uzima wa milele kama furaha yetu, tukiweka tumaini letu katika ahadi za Kristo na si kutegemea nguvu zetu wenyewe, bali kwa msaada wa neema ya Roho Mtakatifu (1); zaidi ya hayo, inajibu shauku ya furaha, ambayo Mungu ameiweka ndani ya moyo wa kila mtu; inabeba matarajio ambayo yanahamasisha shughuli za watu; inawatakasa ili kupanga ufalme wa mbinguni; kulinda dhidi ya kukata tamaa; inasaidia katika wakati wote wa kuachwa; hupanua moyo katika kutazamia raha ya milele (2).”

Matumaini hutoa dirisha katika Umilele katika maisha ya mwanadamu. Tunafahamu vyema, hata hivyo, kwamba jibu la swali kuhusu hatima ya safari ya Kikristo linaweza kupata jibu hasi, kutokana na athari nyingi mbaya zinazotoka duniani; zaidi ya hayo, mbele ya kukabiliwa na hofu ya kufikiri kwamba hakuna kitu baada ya mwisho wa safari, inawezekana kwamba ubinadamu kuangukia katika kukata tamaa. Ikiwa fadhila ya tumaini inakosekana, fadhila nyingine zinazoitegemea pia huporomoka. Leo hii, nguzo hii ya maisha ya imani mara nyingi hupigwa kejeli na kutoeleweka kiasi kwamba hutawala  msemo maarufu “aishie kwa matumaini, hufa kwa kukata tamaa.” Kuna hatari, ambayo inazidi kuvizia, ya kufikiria kuwa tumaini ni: aina ya chumba cha kuwekea shauku zilizoshindwa, [...]. Badala yake, tunahitaji kuwafanya watu waelewe kwamba tumaini ni jamaa wa karibu wa uhalisia. Ni mvutano wa mtu ambaye, baada ya kuanza kwenye njia, tayari amesafiri sehemu yake na kuzielekeza hatua zake, kwa upendo na woga, kuelekea matazamio ya kumalizia ambayo bado hayajafikiwa. Ni ahadi yenye nguvu, kwa ufupi, ambayo haina uhusiano wowote na kutoroka (3).

Ni lazima izingatiwe, hata hivyo, kwamba tumaini si zawadi inayotokana na sifa za kibinadamu pekee, bali ni neema inayotokana na shauku ya ndani ya kuwa na furaha. Kwa njia ya Kristo aliyekufa na kufufuka, neema hii, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, inapandikizwa ndani ya moyo wa kila mwanamume na mwanamke: “Shauku hii ina asili ya kimungu; Mungu aliiweka ndani ya moyo wa mwanadamu ili kumvuta kwake, kwa sababu Yeye peke yake aweza kuijaza” (4). Nimeandika katika Hati ya Kuelekeza Jubilei ya Mwaka Mtakatifu 2025 kwamba:  Kila mtu anatumaini. Katika moyo wa kila mtu kuna tumaini kama hamu na matarajio ya mema, hata bila kujua kesho italeta nini. Kutotabirika kwa siku zijazo, hata hivyo, wakati mwingine husababisha hisia zinazopingana kama vile “kutoka kwa uaminifu hadi hofu, kutoka utulivu hadi kukata tamaa, kutoka kuwa na uhakika hadi kuwa na shaka. Mara nyingi tunakutana na watu waliovunjika moyo wanaotazamia wakati ujao kwa mashaka na kutokuwa na matumaini, kana kwamba hakuna kitu kinachoweza kuwapa furaha (5).

Kwa kupata msukumo kutoka kwa mawazo ya Don Tonino Bello na kutoka katika maneno na katekesi yangu juu ya fadhila ya tumaini, Padre Tommaso Giannuzzi amejaribu kusoma tena baadhi ya vipengele vyake, ambavyo, kupitia maneno yetu, huwa kwa msomaji mwaliko wa kushangazwa na nguvu hii ambayo hupata kwa Aliyefufuka mwanzo wake na kilele chake. Kupitia uchambuzi wa baadhi ya maandishi ya Don Bello na hasa kupitia katekesi juu ya mada hii niliyoifanya katika moja ya Jumatano  mnamo mwaka 2017, msomaji wa maandishi hayo atajaribu kutoa uso kwa chanzo hiki kinachobubujika katika moyo wa mwanadamu. Mwaliko huu basi unakuwa dhamira ya kumsaidia "mtoto huyu mdogo" kukua ndani yetu, kama alivyofanya Don Bello alipenda kufafanua fadhila hii kuu, akifanya kuwa yake mwenyewe kwa maneno na mawazo ya mshairi mkuu na mwandishi Charles Péguy kuwa: “Ni sababu gani ya neema yangu na nguvu ya neema yangu ziwe nini ili kwamba tumaini hili dogo, likiyumba-yumba kwa pumzi ya dhambi, likitetemeka kwa kila upepo, likiwa na wasiwasi kwa pumzi kidogo, liweze kuwa lisilobadilika, la uaminifu, lililo sawa, safi sana; na lisiloshindwa, na lisiloweza kufa, na lisilowezekana kuzima [...]. Kinachonishangaza, asema Mungu, ni tumaini. Siwezi kuamini. Tumaini hili dogo ambalo linaonekana kuwa si kitu. Mtoto huyu anatumaini, hawezi kufa (6).

Dipaji ya Papa
19 Aprili 2025, 10:20