Umati mkubwa wa waamini watoa heshima kumuaga Papa Francisko usiku kucha
Vatican News
Mara baada ya kuleta geneza lenye mwili wa Papa Francisko kutoka katika kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican, Jumatano tarehe 23 Aprili 2025 asubuhi, waamini waliruhusiwa kuanzia saa 5.00 asubuhi hiyo hadi saa 11.30 alifajiri ya leo na baadaye kufungua saa 1.00 kamili. Kwa hiyo kufikia saa 2.30 asubuhi ya leo tarehe 24 Aprili watu 48,600 walitoa heshima zao kwa mwili wa Baba Mtakatifu Francisko. Usiku mzima kuanzia saa 6.00 kamili hadi saa 11.30 alfajiri waamini waliotoa heshima walikuwa ni 13,000, kwa mujibu wa taarifa.
Rozari katika Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu
Wanafunzi wa Emau, sura zilizopotea katika giza la imani, wanakuwa uso wa Kanisa linalosonga, wakiwa wamechoshwa na uchungu na wakati mwingine hawawezi kumtambua Mfufuka wakati wa majaribu. Kardinali Baldo Reina, Makamu wa Papa Jimbo la Roma alivyoeleza jumuiya ya kikanisa iliyokusanyika katika sala ya Rozari kwa ajili ya Baba Mtakatifu Francisko, aliyerejea katika Nyumba ya Baba Jumatatu tarehe 21 Aprili 2025. Katika ukimya uliojaa kumbukumbu zinazosindikiza siku hizi, upendo wa watu wa Mungu haufifii. Unakuwa ishara, sauti, na kuwa katika sala ya Rozari. Kwenye ngazi za Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu ambapo Papa ameomba kuzikwa, waamini walikusanyika mbele ya Salus Populi Romani, yaani Picha ya Maria iliyopendwa sana na Papa, ambayo pia usiki wa tarehe 23 Aprili waamini waliweza kusali.
Mwanzoni mwa matendo ya mafumbo ya utukufu ya Rozari, Kardinali Reina alisema, tukio la Pasaka linahimza kuwa maisha ni neno la mwisho na ambalo huleta jibu jipya kwa wale wanaohoji maana ya kuteseka na kufa. Maneno ambayo huwa kubembeleza kwa watu waliochoka, moyo wa pamoja ambao kwa hakika umejaribiwa, labda kuzimwa, lakini ambao huruhusu mwanga kuchuja wakati unaruhusu kuangaziwa na imani. Picha ya Maria Afya ya Waroma ambayo Papa alisali kabla na baada ya kila Safari ya Kitume, sasa inaalikwa kwa nguvu zaidi kuliko hapo awali. Ili maumivu haya yanaweza kubadilishwa kuwa tumaini. Kwa sababu anatukumbusha uzima na kifo sio neno la mwisho. Hata hivyo katika Basilika hiyo siku nzima, mstari katika ukimya na wa kihisia ulipitia Mlango Mtakatifu huo kama ule wa Basilika ya Mtakatifu Petro, kama hija ya roho kuelekea mwisho ili kutoa heshima na kuaga Papa.