Tafuta

2025.04.05 wakati wa uwasilishaji wa kitabu "Mwendawazimu wa Mungu Mwishoni mwa Ulimwengu" na Javier Cercas. 2025.04.05 wakati wa uwasilishaji wa kitabu "Mwendawazimu wa Mungu Mwishoni mwa Ulimwengu" na Javier Cercas.  (©Pasqualini, Musacchio/Musa)

Cercas:kwa Papa kwanza kabisa ni kumuona kama Padre

Kumbukumbu ya mwandishi wa kihispania,aliyeandika kitabu kilichojikita juu ya ziara ya kitume ya Papa nchini Mongolia.

Andrea Tornielli

"Baada ya dakika ya kwanza ambayo unasema ndio, huyu ndiye Papa, katika mazungumzo ya kibinafsi unagundua kwamba, kwanza kabisa mtu huyu alikuwa kuhani ...". Haya ni maneno ya mwandishi Mhispania Javier Cercas, mtu aliyejitangaza kuwa hamwamini Mungu, mwandishi wa kitabu cha: "The Fool of God at the End of the World"- “Mwehu wa Mungu katika Mwisho wa Dunia”, ambacho kinasimulia ziara ya Papa Francisko  ya kwenda Mongolia. Tulimfikia kwa njia ya simu kumuuliza jinsi gani alivyopokea taarifa za kifo cha Papa.

"Ni wazi nilishangaa, kwa sababu niliamini, kama labda ulimwengu wote ulivyoamini, kwamba Francisko sasa alikuwa nje ya hatari. Siku moja tu kabla alikuwa ametoka nje katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Nilihisi kama amekufa mtu wa karibu sana  na mimi: ni ukweli. Nimesikitia sana.”

Cercas anakumbuka hisia ya ubaba aliyoiweka kwa wale waliokutana naye: “Alikuwa Papa ambaye alikubali makosa yake mwenyewe, ambaye hakuficha kasoro zake, ambaye alijionesha kama mtu na kwa hiyo angeweza kuwa baba kwa watu wengi. Bila shaka, kuna Wakatoliki pia wanaofikiri kwamba Papa anapaswa kuwa karibu "nusu-mungu." Lakini ninaamini kwamba Papa ni mtu wa kwanza kabisa. Petro alikuwa mtu. Papa wa kwanza alikuwa mtu mwenye kasoro nyingi ambaye alimsaliti Kristo mara tatu. Kanisa ni mahali pa wanyonge, mahali pa wenye dhambi."

Mwandishi alisisitiza umuhimu wa utambuzi huu: "Ni kana kwamba alisema: Mimi sio ‘Superman’, mimi ni mtu. Ninataka kukumbuka kwamba jambo la kwanza alilosema katika Kikanisa cha Sistine baada ya kukubali hatua hiyo kwamba: “Ninakubali hata kama mimi ni mwenye dhambi.”  Ufahamu huu wa ubinadamu wake, wa udhaifu wake, ni wa ajabu kwangu. Kwangu mimi, mtu anaweza kusema juu ya Papa Francis kile  ambacho Anna Harendt alisema juu ya Yohane XXIII: yeye ni Mkristo aliyeketi kwenye kiti cha enzi cha Mtakatifu Petro. Na ukaribu wake ni sehemu ya hilo.

Alikuwa mtu mwenye uwezo wa kufanya mambo ya ajabu, ambayo hakuna mtu anayetarajia kutoka kwa Papa. Na nilipitia mambo haya. Mwisho wa kitabu changu, kama ningekuwa muumini kama Papa na kama mama yangu, ningesema ni muujiza mdogo." Cercas anakumbuka mazungumzo aliyokuwa nayo na Papa Francisko kwenye ndege ya kwenda Mongolia: “Kuna muda katika kitabu ambacho mama yangu, ambaye alikuwa muumini wa kina, ananiuliza: lakini ulifikiria nini kuhusu Papa? Papa yukoje? Mama yangu tayari alikuwa mzee sana, afya yake haikuwa nzuri. Jambo la kwanza lililokuja akilini lilikuwa kujibu: yeye ni kama Padre Florian, yaani, kama Padre  wake, Paroko wake, ambaye alimfungisha ndoa na  baba yangu. Hisia ya kwanza ya Papa - baada ya muda wa awali ambapo ulisema ndiyo, hii ni Papa - ilikuwa kwamba kwanza kabisa ulimwona mtu huyu kuhani. “Kwanza kabisa alikuwa kuhani, na kisha alikuwa pia mambo mengine mengi: mtu mwenye akili sana, na utamaduni mkubwa, na uzoefu mkubwa."

Kilichokuwa kinashangaza katika uandishi huo ni kwanza kabisa "unyenyekevu, unyenyekevu wa mtu wa kawaida, hata kama alikuwa mtu tata. Ni ajabu kwangu kwamba huyu ndiye Papa wa kwanza aliyejiita Francisko. Papa Bergoglio alichagua jina hili na fadhila ya kwanza ya Francis wa Assisi ni unyenyekevu hasa. Kujua kwamba sisi ni wadogo sana, kwamba tuna hadhi yetu ya kibinadamu, lakini kwamba sisi ni kitu kidogo." Hatimaye, Cercas alikubali kile anachokiona kuwa fundisho kuu ambalo Papa Francisko alituachia. "Francisko alileta "mapinduzi" kwa Kanisa. Walakini, kila kitu kinategemea maana iliyotolewa kwa neno hili. Ni jambao jema kusema kwamba kumekuwa na "mapinduzi ya mafundisho:"hii ni uongo tu, hata kama kuna watu wanaosema hivyo. Lakini ikiwa yalikuwa ni “mapinduzi”, na pengine ndiyo, yalikuwa yale yaliyooneshwa na Mtaguso wa Pili wa Vatican, Papa Francisko ndiye mwana wa kwanza wa kweli wa Baraza ambaye alikuwa Papa. Alichukua kwa uzito kile ambacho Mtaguso wa Vatican II ulisema, yaani, kurudi kwa Kanisa la Kristo, kwa Kanisa la kwanza.

Katika mahojiano yake ya kwanza na La Civiltà Cattolica, alipoulizwa ni nini alitaka kufanya katika Kanisa, jibu la Papa lilikuwa lisilo na shaka: Nataka kumtoa Kristo nje ya madhabahu na kuingia mitaani. Hiyo ndiyo  maana ya kurudi kwa Ukristo wa Kristo." Mwandishi, wakati wa safari yake kwenda Mongolia, alipata fursa ya kukutana na baadhi ya wanamapinduzi wakubwa wa Injili: “Kurudi huku kwa Yesu Kristo, kulingana na Fransisko na pia kulingana na mimi, kunamwilishwa vyema zaidi katika wamisionari. Ninaamini kwamba Wakristo bora wa Fransisko ni wamisionari, kama tulivyowaona huko Mongolia: watu wanaoacha kila kitu, kama mitume wa Kristo walivyofanya, na kwenda hadi miisho ya dunia kusaidia watu wenye mahitaji. Hii ni asili msingi wa ujumbe wa Kristo. Yesu hakuwa mtu wa nguvu, hakuwa mtu wa mali, lakini mtu ambaye alikwenda na maskini. Kwangu mimi huu ni  msingi: ukosoaji wa ukasisi, ukosoaji wa Constantinism, na kurudi kwa Ukristo. Francisko alikuwa Papa ambaye alichukulia hili kwa uzito na havyo yake ni mageuzi ambayo bado hayajakamilika."

23 Aprili 2025, 16:53