Tafuta

2025.04.11 Jubilei Frosinone 2025.04.11 Jubilei Frosinone 

Jubilei na Frosinone,upya wa kiroho na ushirikiano kati ya Kanisa na taasisi

Mkutano huo ulihamasishwa na Chama cha Wafanyabiashara cha Frosinone Latina,tarehe 10 Aprili kwa mada:“Jubilei 2025:fursa ya ushirikiano kati ya taasisi, biashara na mashirika ya kijamii."Kardinali Ouellet:Tusipoteze matumaini ya kugundua tena utamaduni wa Kikatoliki unaotufafanua kama Wakristo na kama ndugu.

Vatican News

"Jubilei 2025: fursa ya ushirikiano kati ya taasisi, biashara na mashirika ya kijamii" ilikuwa mada ya Mkutano uliofanyika  alasiri, tarehe 10 Aprili 2025 huko Frosinone, Italia . Ni tukio lilioandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara cha Frosinone Latina, katika makao makuu ya taasisi ya Frosinone, ambayo iliwakilisha fursa muhimu ya mazungumzo na kulinganisha kati ya hali halisi tofauti za eneo, kwa lengo la kuchunguza uwezo wa Jubilei 2025 kama kichocheo cha ukuaji wa kijamii, kitamaduni na kiuchumi kwa  Wilaya ya Frosinone na eneo zima kwa ujumla.

Jubilei na eneo, sio tu athari za kidini

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wawakilishi wengi wa taasisi za wilaya  na kikanda, mameneja wa mashirika ya umma na ya kibinafsi, pamoja na wawakilishi wa ulimwengu wa biashara na mashirika ya kijamii. Wazungumzaji walijumuisha, miongoni mwa wengine, meya wa Frosinone, Riccardo Mastrangeli, Monsinyo Ambrogio Spreafico, Askofu wa Jimbo la Frosinone, Veroli, Ferentino, Anagni na Alatri na Giorgio Simeoni, rais wa tume maalum "Jubilei  2025" ya Mkoa wa Lazio.

Kardinali Ouellet: Wakati wa Neema na Upya wa Kiroho

Mjadala huo ulichangiwa zaidi na uwepo wa Kardinali Marc Armand Ouellet, Mstaafu wa Baraza la Kipapa la  Maaskofu, ambaye alihitimisha mchakato huo kwa kusisitiza kwamba: "tunaishi katika machafuko ya kijiografia na ya kibiashara ambayo hatujui yatatupeleka wapi lakini ni muhimu kugundua tena utamaduni wa Kikatoliki ambao unatufafanua kama Wakristo, kama inavyooneshwa na maisha ya kila siku kama ndugu, hata katika maisha magumu ya kila siku. Hili ndilo Tumaini ambalo hatupaswi kupoteza.” Kwa mujibu wa Kardinali Ouellet, Jubilei ya 2025 haiwakilishi tu wakati wa neema na upya wa kiroho, bali pia “fursa madhubuti ya kuimarisha uhusiano kati ya Kanisa, taasisi za kiraia, biashara na ulimwengu wa kijamii.

Matukio kama ya Frosinone ni muhimu kuunda ushirikiano

Matukio kama yale yaliyotangazwa Frosinone ni muhimu ili kuunda mashirikiano ambayo yanapita zaidi ya tukio lenyewe, na kuleta athari ya kudumu kwenye eneo. Ni kwa ushirikiano na mazungumzo ndipo tunaweza kukabiliana na changamoto za wakati wetu na kukuza ukuaji shirikishi, ambao unaweka utu na heshima ya kila jamii katikati. Wakati wa mkutano huo, matunda mengi ambayo Jubilei 2025 inaweza kuleta katika eneo hilo yaligunduliwa, sio tu kwa mtazamo wa kidini lakini pia kama fursa madhubuti ya kukuza ushirikiano kati ya taasisi, biashara na hali halisi ya kijamii. Kiukweli, kulikuwa na mazungumzo ya jinsi tukio hilo linaweza kufanya kama nguvu ya kuendesha maendeleo ya mipango mpya ya kiuchumi, kitamaduni na kijamii, kwa lengo la kuimarisha urithi wa kihistoria na kitamaduni wa jiji la Frosinone na jimbo katoliki. Katika Mkutano huo huo, rais wa Chama cha Wafanyabiashara Giovanni Acampora aliakisi fursa kubwa zinazotolewa na Jubilei 2025 kwa maendeleo ya maeneo, utalii na sekta nzima ya kiuchumi.

Jubilei haipaswi kubaki tukio la pekee

Hatu nyingine  mbali mbali zilihuisha mjadala huo kwa kuakisi uwezo wa Jubilei ya  kuvutia wageni sio tu kutoka Italia bali pia kutoka ng'ambo, na hivyo kuchangia kuongeza mtiririko wa watalii katika eneo hili na kuhamasisha sekta ya ukarimu na huduma. Mjadala huo ulionesha nia thabiti ya taasisi, biashara na mashirika ya kijamii kufanya kazi pamoja ili kujenga mustakabali wa pamoja, kwa kuzingatia maadili ya ushirikishwaji, mshikamano na maendeleo endelevu. Sio wakati tena wa kufikiria Jubilei kama tukio la pekee, lakini kama fursa ambayo inaweza kufanya upya na kuimarisha mizizi ya jumuiya, kwa nia ya ukuaji shirikishi.

Jubilei Frosinone
12 Aprili 2025, 12:38