Jubilei ya Wagonjwa na ya Ulimwengu wa kiafya 5-6 Aprili 2025
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Katika mwaka Mtakatifu wa 2025, tumefikia Jubilei ya Wagonjwa na Ulimwengu wa kiafya kuanzia tarehe 5 na 6 Aprili 2025, ikiwa ni tukio kuu la saba kati ya matukio mengi makuu yaliyopangwa kwenye ratiba ya mwaka huu Mtakatifu wa "Hija ya Matumaini."
Misa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Makundi hayo yanaonekana katika Video yakipita katika Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Misa Dominika tarehe 6 Aprili
Dominika ya Tano ya Kipindi cha Kwaresima tarehe 6 Aprili 2025, Misa takatifu itaadhimishwa kwa ajili yao katika Uwanja wa Mtakatifu Petro saa 4.30 majira ya Ulaya, wakati huo itakuwa ni saa 5.30 majira ya Afrika Mashariki na kati.
Tukumbuke Papa anasema kuwa "Safari ya mhujaji si tukio la mtu binafsi,bali ni la kijumuiya,linaashiria chapa ya mabadiliko yanayoongezeka ambayo yanaelekea msalabani na ambayo daima hutupatia uhakika wa uwepo na usalama wa matumaini,”(katika Hati ya Papa ya kutangaza Jubilei 2025).