Tafuta

Kardinali Parolin, Katibu wa Vatican. Kardinali Parolin, Katibu wa Vatican.  (foto © Comece)

Kard.Parolin:Amani haipo na mazungumzo ni njia ya kuondokana na mawimbi ya vita

Migogoro ya Ukraine na Gaza jukumu la umoja wa pande nyingi na umuhimu wa makabiliano kwa diplomasia ya Vatican ni mambo ambayo Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican alichambua kwenye masuala makuu ya mambo ya kimataifa katika mahojiano na gazeti la kila siku la"La Repubblica:"amani hujengwa kwa uvumilivu,siku baada ya siku na kwa kuheshimiana.

Vatican News

“Katika mahojiano na Gazeti la Italia ‘La Repubblica’ kuhusu masuala makuu ya kimataifa, Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin alionesha msimamo wa Vatican kwamba:  “Vatican ina wasiwasi sana kuhusu hatari ya kuongezeka kwa mzozo nchini Ukraine, ambayo inasababisha mateso zaidi na waathirika wapya huku ikitambua kwamba itakuwa ni unyama kuchukua haki ya Waukraine kujitetea. Kama Baba Mtakatifu Francisko alivyokumbusha mara kwa mara, amani hailazimishwi, inajengwa kwa uvumilivu, siku baada ya siku, kwa mazungumzo na kuheshimiana", alisisitiza Kardinali Parolin, huku akioneesha “kuthamini kila mpango unaoweza kuleta amani kwa sababu vita hivi haviwezi kuendelea.” Tatizo la msingi, kulingana na Kardinali Parolini “ni maono ya mtu binafsi yanayozidi kuongezeka na hali ya kutoaminiana kati ya wanachama wa jumuiya ya kimataifa. Hakuna mtu anayemwamini mtu yeyote tena.. Hali hii  huzalisha woga, silaha nyingine, uchokozi wa mapema na msururu wa migogoro ya kudumu.”

Ni katika muktadha huo Kardinali Parolin alibainisha kwamba kazi ya Vatican pia ni kuhamaisha hatua ndogo ndogo na kuzindua tena maneno ya Warithi wa Petro, ambao kwa zaidi ya karne wamerudia kukataa vita na mbio za silaha, kama Papa Francisko anavyoendelea kufanya. Katika kusisitiza zaidi hatua ya kuanzia, ​​yaani kwamba Vatican inaunga mkono kwa uwazi uhuru na uadilifu wa eneo la Ukraine, Kardinali Parolin alibanisha kwamba “ni juu ya Waukraine wenyewe kuamua ni kitu gani watataka kujadiliana au ikiwezekana kukubali kutoka katika mtazamo huu. Amani ya haki na ya kudumu, kulingana na Kardinali Parolin, itawezekana ikiwa itasimikwa katika  kuheshimu haki na sheria za kimataifa."

Trump Marekani

Katibu wa Vatican, ambaye pia alikuwa akutane na Makamu  Rais wa Marekani J. D. Vance katika ziara yake mjini Roma tarehe 19 Aprili 2025 alijibu swali katika mahojiano ya sera za Trump na ushirikiano wa pande nyingi. "Ni wazi kwamba mtazamo wa utawala wa sasa wa Marekani ni tofauti sana na ule tuliozoea," Kardinali  Parolin aliongeza: Vatican daima inajitahidi kumweka binadamu katikati na kuna watu wengi walio katika mazingira magumu ambao wanateseka sana, kwa mfano, kwa sababu ya kupunguzwa kwa misaada ya kibinadamu. Vatican imefafafanua mara kwa mara inaunga mkono ushirikiano wa pande nyingi na inaamini kwamba sheria za kimataifa na maafikiano ya Mataifa lazima yapendelewe kila mara." Jukumu la kulinda umoja wa pande nyingi ambalo linapaswa kusimamiwa kwanza kabisa na Ulaya. "Kwa mtazamo huu, usemi wa kurudisha silaha tena, ambao daima ni kielelezo cha kufungwa na mizozo mipya, unaonekana kutofaa kuhalalisha hitaji la Ulaya kuwekeza katika ulinzi wake, pia kwa kuzingatia kutojihusisha kwa Marekani katika suala hili.” Katibu wa Vatican hajumuishi kwamba, kwa sababu ya vita vingi, tunakabiliwa na mwaka sifuri katika mazungumzo ya imani: hatupaswi kuangukia kwenye mtego ambao tunakabiliwa na migongano ya asili ya kidini kwa sababu"ikiwa ni chochote, ni suala la uendeshaji wa dini na maadili ya kiroho kwa mwisho zaidi wa kidunia.”

Umuhimu wa mazungumzo

Kuhusu uharibifu huko Gaza, Kardinali Parolin alizungumza juu ya data na picha mbaya za kibinadamu na zisizokubalika kiadili. Kujilinda ni halali, lakini haiwezi kamwe kumaanisha maangamizi kamili au sehemu ya watu wengine au kunyimwa haki yao ya kuishi katika ardhi yao wenyewe." Akijibu swali kuhusu uhusiano na China, Kardinali alithibitisha kwamba Vatican kwa hakika hudumisha shaku ya  kuwa na ofisi yake ya mawasiliano huko Beijing, hatua ambayo imesalia kwa sasa ndani ya eneo la kile kinachohitajika. Hatimaye, kutoka kwa Katibu wa Vatican wito kwa umuhimu wa mazungumzo: "Ninaamini kwamba mchango mkubwa zaidi ambao Vatican inaweza kutoa katika mtazamo wa sasa wa kimataifa ni sawasawa na mazungumzo: kutoa ushuhuda wa umuhimu wake na kumweka katikati mtu, hata ikiwa ni ngumu, hata kama inaweza kuwa chaguo lisilopendwa, hata wakati linaweza kuonekana kuwa lisilo na tija."

 

21 Aprili 2025, 09:45