Kardinali Becciu hataingia kwenye mkutano wa uchaguzi wa Papa
Tangazo la Kardinali wa Sardegna katika uthibitisho wake:“nimeamua kutii utashi wa Papa Francisko,licha ya kuamini kwamba sina hatia.”Uamuzi kwa ajili ya wema wa Kanisa na kwa ajili ya kuchangia umoja na utulivu wa mkutano wa uchguzi.”
Vatican News
Kardinali Giovanni Angelo Becciu hatashiriki katika mkutano wa uchaguzi wa Papa mpya ambao utafunguliwa Jumatano tarehe 7 Mei 2025. Ametangaza yeye mwadhama wa Sardegna kwa uthibitisho huu: “Nikiwa na moyo wa wema wa Kanisa, ambalo nimelitumikia na nitaendelea kulitumikia kwa uaminifu na upendo, pamoja na kuchangia ushirika na utulivu wa mkutano wa uchaguzi(Conclave), nimeamua kutii, kama nilivyofanya siku zote, mapenzi ya Baba Mtakatifu Francisko ya kutoingia kwenye Mkutano wa uchaguzi(Conclave) huku nikiendelea kusadiki kwamba sina hatia.”
29 Aprili 2025, 10:35