Tafuta

2025.04.07 Kardinali Krajewski apeleka magari ya wagonjwa nchini Ukraine. 2025.04.07 Kardinali Krajewski apeleka magari ya wagonjwa nchini Ukraine. 

Kardinali Krajewski apeleka Magari manne ya kubebea wagonjwa zawadi ya Papa kwa Ukraine

Utume wa kumi katika nchi ya Mashariki kwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo ambaye,kwa maelekezo ya Papa Fransisko na kwa msaada wa madereva wengine wa Ukraine, amepeleka magari yenye kila chombo cha matibabu muhimu ili kuokoa maisha ya binadamu, ambayo yataelekezwa kwa maeneo ya vita.

Vatican News

Hali halisi ya Pasaka Mpya bado inakiwakilisha  ndani ya Vita nchini Ukraine na kwa sababu hiyo Baba Mtakatifu Francisko anaendelea "kuelezea ukaribu wake kwa watu wanaoteseka kwa ishara madhubuti, miaka mitatu baada ya kumbukumbu ya uchungu na ya aibu kwa ubinadamu," kama Papa alivyokuwa amesema hapo awali.

Magari manne ya wagonjwa zawadi ya Papa kwa Ukraine
Magari manne ya wagonjwa zawadi ya Papa kwa Ukraine

Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo imeripoti maneno ya Papa Francisko ya  Urbi et Orbi 2024, ambayo ni chachu ya kuchukua hatua. “Ni Yesu pekee anayetufungulia milango ya uzima," Papa alisema kwamba "milango hiyo ambayo tunaifunga mara kwa mara na vita vilivyoenea ulimwenguni kote.” Hatua hiyo inahusisha kutuma Magari manne ya Wagonjwa yakiwa na  nembo ya Mji wa Vatican, yenye kila chombo cha matibabu kinachohitajika kuokoa maisha ya binadamu, ambazo zitapelekwa kwenye maeneo ya vita kuwa pamoja na watu walioathirika sana na migogoro, ili kusali pamoja nao na kuwa kielelezo cha ukaribu wa Askofu wa Roma.

Magari manne ya Wagonjwa, zawadi ya Papa kwa Ukraine
Magari manne ya Wagonjwa, zawadi ya Papa kwa Ukraine

Kwa hiyo ni misheni ya kumi nchini Ukraine kwa Kardinali Conrad Krajewski, Mwakilishi wa Papa, misheni ambayo imezaliwa katikati ya Jubilei ya Matumaini 2025! Katika Hati ya kutangaza Jubilei Kuu ya matumaini,ya (Spes non Confundit, ya Papa Francisko anaandika kwamba: "Ishara ya kwanza  ya matumaini itafsiriwe katika amani kwa ulimwengu, ambayo kwa mara nyingine inajikuta imezama katika janga la vita. Hitaji la amani ni changamoto kwa kila mtu na linahitaji kufuatilia mipango madhubuti." Zawadi ya magari 4 ya wagonjwa (ambulensi ) kwa hivyo inakuwa ishara ya tumaini la Jubilei linalojikita ndani ya  Nanga ya Kristo.

ZAWADI YA PAPA KWA UKRAINE
07 Aprili 2025, 11:21