Nafasi ya Utamaduni katika Taasisi za Magereza,Tukio la Vatican
Vatican News.
"Utamaduni ni maisha katika maeneo ya magereza” ndicho kichwa cha tukio litakalofanyika Alhamisi, tarehe 10 Aprili 2025, saa 12:00 jioni, masaa ya Ulaya, katika Ukumbi wa Mtakatifu Pio X katika Njia ya Hospitali lililohamasishwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu pamoja na Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Mkutano huo utakaosimamiwa na mwanahabari Riccardo Iacona, utashuhudia ushiriki wa wataalamu kutoka katika ulimwengu wa taaluma, sanaa, uandishi wa habari na utamaduni ambao watajadili thamani ya utamaduni kama nyenzo ya ukuaji, ukombozi na hadhi ya binadamu katika mazingira ya magereza.
Hatua za kuingilia kati
Mkutano huo utafunguliwa kwa salamu za kitaasisi kutoka kwa Kardinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza ala Kipapa la Utamaduni na Elimu na Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Vile vile Stefano Anastasia wa (Unitelma Sapienza) pia atazungumza; msanii Laurie Anderson; Roberta Barbi mwandishi wa habari wa Radio Vatican - Vatican News; Rosa Galantino, mwandishi na mtayarishaji wa filamu ya maandishi ‘Le Farfalle della Giudecca’; Teresa Paoli, mwandishi wa habari wa Presadiretta (Rai 3); Cristiana Perrella, msimamizi wa CONCILIAZIONE 5 na mkurugenzi wa MACRO; Pisana Posocco na Marta Marchetti wa Chuo Kikuu cha Sapienza cha Roma; Marcello Smarrelli, mkurugenzi wa kisanii wa Mfuko wa Pastificio Cerere; msanii Tommaso Spazzini Villa.
Uwasilishaji wa mpango
Wakati wa hafla hiyo, mipango kadhaa itawasilishwa, ya zamani, ya sasa na ya baadaye, ya kitaifa na kimataifa, ambayo imeona utimilifu wake ndani ya taasisi za jela. Kwa mfano Laurie Anderson, msanii na mtunzi mashuhuri wa kimataifa, ataonesha mpango wa Dal Vivo,uliuondwa kwa ajili ya Mfuko wa Prada mnamo 1998 katika gereza la Mtakatifu Vittore, na mpango wa 2015 wa Habeas Corpus, usakinishaji ambao unaonesha sura ya mfungwa kijana kutoka Guantanamo. Cristiana Perrella, msimamizi wa nafasi mpya ya sanaa ya kisasa ya Baraza la Kipapa la Utamaduni na elimu "Conciliazione 5", atachukua nafasi kuwasilisha mpango wa kisanii wa Yan Pei-Ming, wa Oltre il muro, yaani “zaidi ya kuta”; mchoraji wa Kichina aliunda picha 27 zinazotoa sura kwa ubinadamu anayeishi na kufanya kazi katika gereza la Regina Coeli, taasisi kuu na inayojulikana zaidi ya wafungwa jijini Roma, iliyoko mita chache kutoka jijini Vatican.