Njia ya Msalaba jijini roma:vijana kutoka Ulimwenguni kwa sala na ushuhuda!
Vatican News
Wapendwa vijana, tunataka kuonja furaha ya kuadhimisha Jubilei ya Vijana wadogo, tukirejea baadhi ya Njia za Msalaba: safari ya Kristo Mfufuka pamoja na wanafunzi wake. Maisha yetu yamejaa furaha na huzuni, maswali na majibu, lakini pia ya matarajio na matumaini. Leo kuliko wakati mwingine wowote ulimwengu kama Mtakatifu Paulo VI tayari alikuwa amaesema tunahitaji mashuhuda zaidi kuliko walimu.
Kwa sababu hiyo tunataka kujiweka wenyewe katika roho ya sala, tukitoa sauti kwa mashuhuda waliojionea ufufukoo, ili Roho wa Yule Aliyefufuka aithibitishe imani yetu, aimarishe tumaini letu, na kuwasha mioyo yetu na upendo Wake. Kwa maneno haya, Askofu Mkuu Rino Fisichella, aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, aliwakaribisha makumi ya maelfu ya wavulana na wasichana wadogo waliofika jijini Roma kwa ajili ya Jubilei ya Vijana wadogo au barubaru, ambao saa kumi na mbili jioni walikusanyika kwenye ngazi za Kanisa la Watakatifu Petro na Paulo huko EUR ili kufanya tukio la kwanza la Jubilei yao iliyokuwa imepangwa ya NJIA YA MSABA, mpango wa maombi uliozaliwa mwaka 1988 ndani ya familia ya Wasalesiani, na uzoefu kwa mara ya kwanza mwaka 1990, katika Makaburi ya wakristo wa kwanza huko Mtakatifu Callisto,jijini Roma.
Katika oktava ya Pasaka, vijana kutoka Italia na ulimwengu walisindikizana katika hali hii ya ufufuko kwa njia ya sala katika vituo saba (na sio kama vil vya kawaidia 14 vya kanuni) na usomaji wa kifungu cha Injili, sehemu ya sala ya kwaya na sehemu ya tatu iliyosomwa na vijana 4-5. Kwa hiyo ilikuwa pia gursa ya kurejea maisha ya Yesu na kumfikiria Papa Francisko katika mtazamo wa Ufufuko na uzima wa milele.
Nyimbo, sala, tafakari
Kutoka Uwanja wa Mtakatifu Petro, ambako wengi walikuwa wamekwenda kwenye Kanisa kuu la Vatican ili kutoa heshima kwa mwili wa Papa, basi walisafiri kwa Mabus binafasi na yale ya umma, ambapo lilikuwa wimbi la wavulana na wasichana wengi walihamia kwenye uwanja wa Kanisa maarufu uliowekwa wakfu kwa walinzi wawili wa Roma. Walipeperusha bendera, wakiimba pamoja na kwaya ya Jimbo la Roma na zaidi ya yote walisali katika wakati huo wa kipekee katika maisha ya Kanisa la Ulimwengu.
Kikundi kimoja cha michezo ya vijana kilisoma vifungu kutoka katika vituo saba na tafakari, zilizochukuliwa kutoka katika Injili na Matendo ya Mitume. Kwa historia ya muziki, Picha ya Bikira ilioneshwa na kuimba kwa wimbo usiosahaulika wa Siku ya vijana duniani( WYD) wa 2000, “Yesu Kristo wewe ni maisha yangu”, haukukosa.
"Njia ya Msalaba ikifuata hatua za Kwaresima kuotia kipindi hiki cha Pasaka ilirejea makutano ya Yesu mfufuka pamoja na mashuhuda wa ufufukoo, kuanzia Dominika ya Pasaka hadi Pentekoste", alieleza Padre Massimo Tellan, paroko wa Parokia ya Kirumi ambaye alipanga wakati wa maombi. Mwandishi wa maandiko mbalimbali, kuhani alieleza kwamba, kwa kuandika, "Nilifikiri juu ya kile amnacho kijana wa leo angeuliza wakati wa kukutana na mashahidi wa ufufukoo.
Vijana wawili wanaoigiza katika historia hiyo walikuwa wakisafiri kwenda Roma kujionea Jubile, lakini kutokana na hila katika programu hiyo waligunduliwa miaka 2000 iliyopita, mara tu baada ya kufufuka kwa Yesu. Vijana hawa wawili wanakutana na Mtakatifu Maria Magdalene, Mtakatifu Thomas, Mtakatifu Yohane, Mtakatifu Petro na wengine wengi, ambao huwasaidia katika jaribio lao la kutafuta njia ya kurudi Roma. Hapa, kile amabcho watoto wanaweza kugundua ni kwamba mashahidi wanaokutana nao hawaoneshi njia ya kurudi kwenye wakati wao, lakini badala yake huwasaidia kuelewa.
Kuishi maumivu kwa matumaini
Kama vile Mshumaa wa Pasaka ulikuwepo karibu na jeneza la Papa, kuanzia Jumatano iliyopita wakati wa uhamisho wa mwili wake hadi Basilika, Mshumaa huo ni mhusika mkuu wa Njia ya Msalaba na mienge saba iliwashwa kutoka katika moto wake."Kwa sisi waamini, mazishi ni kuambatana na nyumba ya Baba," alieleza Padre Massimo, "na kuweza kuomba kwa mtazamo huu kunasaidia watoto - vijana kuona wakati huu wa mpito na maumivu katika mwanga wa Tumaini ambalo halikatishi tamaa, ambaye ni Kristo mwenyewe."