Papa amemteua Askofu Koffi Oi Koffi kuwa Askofu Mkuu wa Gagnoa,Ivory Coast
Vatican News.
Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 8 Aprili 20025 amemteua kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Gagnoa nchini Ivory Coast, Mwashamu Askofu Jean-Jacques Koffi Oi Koffi ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Askofu wa Mtakatifu Pedro na Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Kuu hilo hilo.
Wasifu wake
Mwashamu Askofu Jean-Jacques Koffi Oi Koffi alizaliwa tarehe 22 Machi 1962 huko Bongouanou. Alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 4 Agosti 1990, kwa ajili ya jimbo la Abengourou.
Katika mafunzo yake pia ana Leseni ya Sheria za Kanisa, katika Chuo Kikuu cha Kipapa Urbaniana, Roma. Alishikilia nyadhifa mbali mbali kama vile kuwa Makamu Paroko wa Parokia na mhusika wa Jimbo kwa ajili ya Katesi kwa Watoto, Paroko, Makamu na Msimamizi wa Kiroho wa Chama cha Familia za Kikristo; Rais wa Mahakama ya Kikanisa Kijimbo.
Kunako tarehe 21 Novemba 2023, aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Abengourou na kuwekwa wakfu wa kiaskofu kunako tarehe 21 Desemba iliyofuata.
Kunako tarehe 3 Januari 2009 alikuwa amehamishwa kwenda Jimbo la Mtaakatifu Pedro huko Ivory Coast. Kuanzia tarehe 4 Oktoba 2023 amekuwa pia Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Kuu la Gagnoa.