Papa ateua wawakilishi wake maalum katika maadhimisho huko Rijeka na Katowice
Baba Mtakatifu tarehe 12 Aprili 2025 amemteua Kardinali Matteo Maria Zuppi,Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Bologna na Rais wa Baraza la maaskofu wa Italia,kuwa mwakilishi wake Maalum katika maadhimisho ya Miaka 100 ya Jimbo Kuu la Rijeka nchini Kroatia.Na pia kumteua Kardinali Kazimierz Nycz,Askofu Mkuu Mstaafu wa Warszawa kuwa Mwakilishi wake Maalum katika maadhimisho ya miaka 100 ya Jimbo Kuu Katoliki la Katowice nchini Poland yatakayofanyika Juni 11,2025.
12 Aprili 2025, 16:48