Tafuta

Kuanzia Lampedusa -Italia hadi Juba - Sudan Papa  Francisko alipendelea ulimwengu wa pembeni. Kuanzia Lampedusa -Italia hadi Juba - Sudan Papa Francisko alipendelea ulimwengu wa pembeni.   (ANSA)

Papa Francisko:sauti ya huruma kwa Afrika

Papa Francisko alikuwa na moyo mkubwa kwa ajili ya Afrika na Waafrika.Anaacha nyuma yake urithi wa kujitolea kwa jitihada za amani,haki ya kijamii na maendeleo fungamani kwa Afrika na ulimwengu mzima.Ili kuyatia taji yote hayo tunaona mshikamano wa Papa na wakimbizi na wahamiaji wa Kiafrika,maskini na waliotengwa ambao utaendelea kuishi.

Na Paul Samasumo – Vatican.

Afrika inaomboleza sio tu kwa kumpoteza kiongozi wa kiroho kwa Wakatoliki lakini pia kwa mtu ambaye hakuogopa kutetea mambo yasiyopendwa na watu wa Kiafrika ambayo mara nyingi yanapuuzwa na vyombo vya kawaida vya habari. Hizi ni pamoja na histroia za udhaifu wa Afrika unaojidhihirisha kama migogoro, unyonyaji, umaskini na magonjwa.

Kukaribishwa, kusindikiza, kuunga mkono na kufungamanisha

Ilikuwa kana kwamba mada ya uhamiaji ilimchagua Papa Francisko. Safari yake ya kwanza ya upapa nje ya Roma,Julai 2013, ilikuwa kwenye Kisiwa cha Italia kiitwacho Lampedusa, ambapo vijana wengi wahamiaji wa Kiafrika walikuwa wamekufa katika ajali ya meli kwenye Bahari ya Mediterania walipokuwa wakijaribu kufikia fukwe ya Ulaya. Juu ya madhabahu iliyotengenezwa kama boti iliyopakwa rangi, Papa Francisko alitangaza, "Katika ulimwengu huu wa utandawazi, tumeangukia katika kutojali kwa utandawazi," alisema. "Tumezoea mateso ya wengine na kusema: hainiathiri; hainihusu; sio kazi yangu!"  Katika miaka ya baadaye, baada ya Lampedusa, Papa Francisko ameweza kusisitiza mara kwa mara kwamba "Wahamiaji wanapaswa kukaribishwa, kusindikizwa, kuungwa mkono, na kuunganishwa katika jumuiya zinazowapokea." Ulikuwa ujumbe usiopendwa na wengi barani Ulaya, lakini Baba Mtakatifu aliendelea kuurudia.

Ahadi ya Umisionari nchini Msumbiji

Baba Mtakatifu Francisko wa wakati ujao, wakati huo akiwa Askofu Mkuu Jorge Mario Bergoglio, alipokuwa mji mkuu wa Buenos Aires nchini Argentina mnamo mwaka 1998, aliendelea kwa ari kubwa kujitolea kutuma mapadre wamisionari wa Argentina huko Msumbiji katika Jimbo la Xai Xai. Hii ilikuwa ni kuitikia ombi la Askofu Julio Duarte Langa, Askofu mzaliwa wa Msumbiji wa Jimbo la Xai-Xai. Askofu Langa aliteuliwa kuwa Kardinali mwaka 2015.

Ziara za kukumbukwa za Kitume Barani Afrika

Safari za Papa Francisko barani Afrika zilikuwa za kukumbukwa na za kihistoria, zikisisitiza heshima yake na kujali Afrika. Labda hakuna kitu kinachoonesha safari hizi vizuri zaidi kuliko ziara yake ya kwanza ya Kiafrika mnamo 2015, Kenya, Uganda, na Jamhuri ya Afrika ya Kati.  Wakati huo, ziara ya Jamhuri ya Afrika ya Kati haikuchukuliwa kuwa hatari tu,bali ilirejewa na vyombo vya habari kama "hatari kubwa zaidi ya usalama ya upapa wake." Wengine hata walifikiri kuwa ni tukio la kipumbavu. Licha ya vurugu kubwa zinazoendelea katika nchi hiyo yenye matatizo, Papa Francisko alitua CAR tarehe 29 Novemba 2015.

Alikataa mapendekezo ya kuvaa vazi kuzuia risasi au kutumia ngao ya kuzuia risasi kwenye Gari la Papa wakati wa kuzungukia watu katika ziara yake.  Mwandishi wa makala haya alikuwa miongoni mwa wanahabari wengine katika safari hiyo ya Papa na alimshuhudia Papa Francisko akienda kwenye mkutano na jumuiya ya Waislamu katika msikiti wa kati wa Koudoukou mjini Bangui. Wakati huo, sehemu hiyo ya jiji, PK5, ilionekana kuwa eneo la kutokwenda kwa mtu asiye Muislamu. Hata hivyo imamu mkuu katika msikiti huo, Tidiani Moussa Naibi, alimkaribisha Papa kwa furaha na kumshukuru kwa ziara yake. Hakukuwa na uadui wowote. Wakati wa Upapa, Baba Mtakatifu alisafiri hadi Kenya, Uganda, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Misri, Morocco, Msumbiji, Madagascar, Jamhuri ya Congo na Sudan Kusini. Ziara yake nchini Sudan Kusini ilifanyika pamoja na Askofu Mkuu wa Kianglikani wa Canterbury na Msimamizi wa Kanisa la Scotland.

Papa wakati wa ziara yake Madagascar
Papa wakati wa ziara yake Madagascar   (Vatican Media)

Katika pwani ya mashariki ya Afrika, Papa Francisko pia alitembelea Mauritius wakati wa safari hiyo hiyo ya Kitume kwenda Msumbiji na Madagascar. Katika safari hizi barani Afrika, Baba Mtakatifu Francisko alizungumza kwa shauku juu ya amani, upatanisho na haki ya kijamii, akiakisi uthabiti wa watu wa Kiafrika bila kujali shida nyingi wanazokabiliana nazo kama watu. Akikutana na viongozi wa serikali, kiraia na kidiplomasia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Papa Francisko alisema katika hotuba yake, “ Ondoeni mikono kutoka  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo! Ondoeni mikono mbali na Afrika! Acha kuisonga Afrika; Afrika sio mgodi wa kuvuliwa au eneo la kuporwa," Papa alisema.

Papa wakati wa ziara ya Sudan Kusini
Papa wakati wa ziara ya Sudan Kusini   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Wakati mwingine Papa ndiye pekee aliyeweza kuibua masuala yanayohusu bara la Afrika, kama vile athari za mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa usawa wa kiuchumi na ukosefu wa utulivu wa kisiasa. Alikumbusha ulimwengu juu ya historia za wanadamu nyuma ya takwimu, zinazotetea sera zinazolinda haki za binadamu na kutetea mahitaji ya walio hatarini zaidi. Alikuwa fasaha zaidi wakati wa janga la UVIKO-19 alipotoa wito wa usambazaji wa haki na "roho ya uwajibikaji wa kimataifa" kuhakikisha kuwa Afrika na mataifa mengine yanayoendelea hayakuachwa katika ugawaji wa chanjo za UVIKO-19.

Papa alifungua mlano  Mtakatiu huko Afrika ya Kati
Papa alifungua mlano Mtakatiu huko Afrika ya Kati

Msisitizo wa Papa Francisko kwa Afrika

Mapenzi makubwa ya Papa Francisko kwa Afrika yalienea zaidi ya hotuba na matamko. Alikuwa, juu ya yote, Mchungaji na Mchungaji wa ulimwengu wote.  Kwa mfano, Papa aliadhimisha Misa mara mbili kwa ajili ya jumuiya ya Wacongo walioko Roma (mnamo Desemba 2019 na Julai 2022). Katika matukio haya, na katika ziara ya mwaka 2023 nchini Congo, Baba Mtakatifu Francisko alionesha uungwaji mkono na faraja yake kwa Ibada ya Liturujia ya Zaire.  Hata aliweza kusema kwamba Ibada ya Zaire ilikuwa mfano wa kuahidi kwa tamaduni zingine. Kumwona Papa akiwa nyumbani na kutokerwa kabisa na uchangamfu wa kitamaduni na hali ya kiroho ya Afrika ilikuwa ya kushangaza.

Papa alpotembelea Congo Dr
Papa alpotembelea Congo Dr   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Aliwataka Waafrika kukumbatia maadili yao ya zamani ya kuheshimu babu na bibi na wazee na daima kuona tofauti za kikabila kama furaha ya kukumbatiwa. Kamwe tishio. Kwa hakika, Papa Francisko “aliporudi katika nyumba ya Baba" Mashahidi wa Uganda, ambao hekalu lake alitembelea mwaka wa 2015, walikuwa wa kwanza kwenye mstari wa kumkaribisha Baba Mtakatifu nyumbani.

Papa na Afrika
24 Aprili 2025, 10:16