Rais mpya,mwanamke wa Tume ya Ulinzi wa Makumbusho ya kihistoria ya Vatican
Vatican News
Kardinali Pietro Parolin tarehe 10 Aprili 2025 amemteua Profesa Cajano kuwa Rais wa Kamishna ya Ulinzi wa Makumbusho ya Kihistoria na Kisanaa ya Vatican. Bi Elvira Cajano, ni profesa mgeni katika Kitivo cha Historia na Turathi za Kiutamaduni za Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana mjini Roma.
Profesa Cajano alizaliwa Parma, Italia mnamo tarehe 29 Mei 1955, na kupata digrii ya Usanifu na Uzamimi na ana shahda ya PhD katika Historia, Usanifu na Urejeshaji wa Usanifu kutoka Chuo Kikuu cha “La Sapienza" Roma.
Nyadhifa mbali mbali aliwahi kuwa na jukumu la usimamizi wa Akiolojia, Sanaa Nzuri na Mazingira ya Umbria. Alikuwa profesa wa nadharia ya urejesho na uhifadhi katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, Roma na ndiye mwandishi wa machapisho mengi. Katika jukumu hili, anachukua nafasi ya Profesa Francesco Buranelli, Mkurugenzi wa zamani wa Makumbusho ya Vatican, na rais tangu Januari 2017.