Tafuta

Siku ya Kuombea Kazi ya Uumbaji 2025: Mbegu za amani na matumaini Siku ya Kuombea Kazi ya Uumbaji 2025: Mbegu za amani na matumaini 

Siku ya kuombea Kazi ya Uumbaji Ulimwenguni 2025:“Mbegu za Amani na Tumaini”

Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Maombi kwa ajili ya Kazi ya Uumbaji kwa mwaka 2025 imechapisha mada iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa ni “Mbegu za Amani na Matumaini.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, amechagua mada itakayoongoza  Siku ya Kimataifa ya Maombi kwa ajili ya Utunzaji wa Kazi ya Uumbaji kwa mwaka 2025 kuwa ni “Mbegu za Amani na Matumaini.” Kwa mujibu wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha, Maendeleo Fungamani ya Binadamu inabanisha kuwa Kipindi cha kuombea kazi ya Uumbaji ni mpango wa kiekumene ambao unakuwa wa kawaida na unafanyika kuanzia Septemba 1 hadi Oktoba 4 ya kila mwaka.

Amani pamoja na uumbaji

Mada ya toleo la 2025, katika mwaka wa Jubilei na kumbukumbu ya miaka kumi ya kuchapishwa kwa Waraka wa Kitume wa Papa Francisko wa  Laudato si’, kuhusu Utunzaji wa Mazingira Nyumba yetu ya Pamoja ni “amani pamoja na uumbaji” na, kama maandishi ya Biblia ya marejeo ya mpango huo kutoka Nabii Isaya 32:14-18 iliyochaguliwa.

Uharibifu wa nyumba yetu ya pamoja

Kama ilivyosisitizwa katika Majisterio ya Papa Francisko na watangulizi wake wa hivi karibuni, uhusiano kati ya amani na utunzaji wa kazi ya uumbaji uko karibu sana (tazama Jumbe za Siku ya Amani Duniani 1990 na 2010). Vile vile, kuna uhusiano wa karibu sana kati ya vita na vurugu kwa upande mmoja, na uharibifu wa nyumba yetu ya pamoja na upotevu wa rasilimali (uharibifu na silaha) kwa upande mwingine.

Maombi kwa ajili ya amani

Kwa njia hiyo Ujumbe unahimiza maombi ili hali za amani ziweze kuundwa, amani ya kudumu iliyojengwa pamoja, ambayo inatia matumaini. Mfano wa  mbegu unaoneesha hitaji la kujitolea kwa muda mrefu. Ujumbe huo unaonesha mazoea mazuri na mbegu za amani na tumaini kutoka kwa mabara mbalimbali.

Siku ya Kuombea Kazi ya Uumbaji 2025
07 Aprili 2025, 15:01