Tafuta

"Sura za Injili,"Papa asimulia juu ya Zakayo mtoza ushuru

Vatican News

Tukio la Pili kati ya 18 ambayo yanaunda “Sura za Injili,” zilizopendekeza na Vatican News katika kipindi hiki cha Karesima na Pasaka, tukio linalojikita kuelezea juu ya sura ya Zakayo aliyekuwa mkuu wa Watoza ushuru, fisadi na tajiri nyuma ya migongo ya wengine, lakini ambaye alipata ujasiri wa kupanda mti ili kumwona Yesu. Mtazamo wa Mwalimu unamjaza furaha na kumfanya abadili maisha yake milele.

Kipindi hicho kililirushwa hewani kwa mara ya kwanza wakati wa Dominika ya Pasaka 2022 kwenye (Rai Uno), Runinga ya Italia na kilisimamiwa na Baraza la Mawasiliano kwa ushirikiano na Maktaba ya Kitume ya Vatican, Makumbusho ya Vatican na (Rai Cultura)- Runinga ya Italia kipindi cha utamaduni. Katika mfululizo huo, Papa Francisko anasimulia baadhi ya matukio ya Yesu. Waandishi wa mpango huo ni Andrea Tornielli na Lucio Brunelli, mwelekeo na upigaji picha ulisimamiwa na Renato Cerisola, muziki wa asili ni Michelangelo Palmacci.

Sura za Injili: Zakayo Mtoza ushuru

 

09 Aprili 2025, 09:56