Mshindi wa Toleo la 7 kwa tuzo ya kimataifa ya uchumi na jamii ya Centesimus Annus pro Pontefice
Vatican News
Pamoja na insha ya "Binadamu katika Kitanzi. Maamuzi ya Binadamu na Akili Mnemba", Padre Paolo Benanti,(TOR) alishinda toleo la saba la Tuzo ya Kimataifa ya "Uchumi na Jamii" iliyohamasishwa na Mfuko wa Kipapa wa Centesimus Annus pro Pontifice. Mpango huo, ambao ulizaliwa miaka kumi na miwili iliyopita, unafanyika kila baada ya miaka miwili na unalenga kukuza kazi ambazo zinasimama wazi kwa mchango wao wa awali katika kujifunza na kutumia Mafundisho Jamii ya Kanisa na yenye mshikamano unaotambulika wa kimafundisho, na pia unaoleweka kwa umma kwa ujumla.
Akili Mnemba zipo katika kila nyanja ya maisha ya kila siku na kama Padre Paolo Benanti mwenyewe anavyoandika kwenye Tovuti yake (www.paolobenanti.com), kujitolea kwa mada za maadili, (Bioethics) utafiti wa masuala ya kimaadili, kijamii na kisheria ambayo hutokea katika madawa na utafiti wa matibabu, na teknolojia: "Ninajaribu kuzingatia maana ya maadili na anthropolojia ya teknolojia kwa Homo sapiens: sisi ni aina ambayo imeishi duniani kwa miaka 70,000, kuibadilisha, hali ya kibinadamu ni hali ya teknolojia ya kibinadamu.”
Padre Benanti
Padre Paulo Benenati(TOR), Mfransiskani wa Kanuni ya Tatu, alizaliwa tarehe 20 Julai 1973 ambaye anajihusisha na masuala ya utafiti na maadili ya kiteknolojia. Kwa namna ya pekee hasa masomo yake yanazingatia usimamizi wa uvumbuzi: Mtandao na athari za Enzi ya kidijitali, teknolojia ya kibayoteknolojia kwa ajili ya uboreshaji wa binadamu na usalama wa viumbe, sayansi ya neva na teknolojia ya neva. Katika moja ya mikutano kuhusu masuala haya Padre Benanti alisema kuwa “Ili kuendeleza uvumbuzi kuelekea maendeleo halisi ya binadamu ambayo hayadhuru watu na hayaleti usawa mkubwa wa kimataifa, ni muhimu kuchanganya maadili na teknolojia. Kufanya thamani hii ya kimaadili kuwa kitu kinachoeleweka kwa mashine, inahusisha uundaji wa lugha ya ulimwengu wote ambayo inamweka mwanadamu katikati: maadili ya miendendo ya kidijitali hutukumbusha kila wakati kuwa mashine iko kwenye huduma ya mwanadamu na sio kinyume chake.”