Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuhimiza umuhimu wa waamini wa dini mbalimbali duniani kufahamiana, kuheshimiana na kushirikiana kwa dhati katika huduma kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuhimiza umuhimu wa waamini wa dini mbalimbali duniani kufahamiana, kuheshimiana na kushirikiana kwa dhati katika huduma kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.  (AFP or licensors)

Umuhimu wa Majadiliano ya Kidini Katika Kudumisha Haki na Amani

Ni katika muktadha wa majadiliano ya kidini huko Senegal kati ya tarehe 7 hadi 8 Aprili 2025 kumefanyika mkutano wa majadiliano ya kidini, nchini Senegal kwa kunogeshwa na kauli mbiu “Diplomasia ya kidini;” na kwamba, Senegal ni mfano bora wa diplomasia ya kidini ambapo waamini wa dini mbali mbali wanaweza kuishi kwa pamoja. Kimsingi dini mdaua mkubwa katika kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani, ustawi, mafao na maendeleo ya wengi!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Adui mkubwa wa mchakato wa majadiliano ya kidini ni woga na wasiwasi usiokuwa na msingi, mambo yanayochangia watu wa dini mbalimbali kushindwa kufahamiana na hatimaye, kuishi kwa amani, umoja na udugu wa kibinadamu kwa kutambua kwamba, wote wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na hivyo tofauti zao za kidini si sababu msingi ya malumbano na kinzani zisizo na tija wala mashiko kwa watu. Watambue kwamba, wote ni watoto wa Baba mmoja, Mzee Ibrahimu, Baba wa imani; mwaliko wa kuwa wazi, wenye upendo na ukarimu, kwa kutambua kwamba, wote ni watoto wa familia kubwa ya binadamu. Katika mchakato wa majadiliano ya kidini, Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuhimiza umuhimu wa waamini wa dini mbalimbali duniani kufahamiana, kuheshimiana na kushirikiana kwa dhati katika huduma kwa maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.

Majadiliano ya kidini ni sehemu ya vinasaba vya maisha ya Kanisa
Majadiliano ya kidini ni sehemu ya vinasaba vya maisha ya Kanisa

Majadiliano ya kidini ni sehemu ya vinasaba vya maisha na utume wa Kanisa Katoliki ili kujenga na kudumisha amani, upendo na mshikamano kati ya watu wa Mataifa na wala si kwa bahati mbaya kwamba, Kanisa katika mikakati na vipaumbele vyake katika mchakato wa uinjilishaji linaendelea kukazia majadiliano ya kidini na waamini wa dini mbalimbali duniani. Waamini wanaweza kujenga na kudumisha umoja, udugu wa kibinadamu na urafiki wa kijamii kwa kusaidiana katika hija ya maisha yao huku bondeni kwenye machozi. Ushuhuda wa umoja na udugu wa kibinadamu ni tunu ya thamani kubwa katika ulimwengu mamboleo. Baba Mtakatifu Francisko anasema, majadiliano ya kidini yanayosimikwa katika ukweli na uwazi kati ya Wakristo na waamini wa dini ya Kiislam ni utii kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, ili watu wote waweze kupendana, kusaidiana pamoja na kutatua changamoto za maisha, kwa kusikilizana na kusaidiana; kwa kuelewana katika hali ya unyenyekevu na uvumilivu mkuu.

Majadiliano ya kidini yadumishe haki, amani na maridhiano
Majadiliano ya kidini yadumishe haki, amani na maridhiano   (ANSA)

Majadiliano ya kidini yanasaidia kutambua, kukuza na kudumisha utu, heshima na haki msingi za binadamu. Kati ya haki hizi ni: ile ya uhuru wa dhamiri na uhuru wa kuabudu, kila mtu akiwa huru kufanya maamuzi kuhusu imani yake, na wala kusiwepo wongofu wa shuruti ili mwamini kuweza kujipatia fedha au ajira, wala kutumia ujinga wa waamini kuwaongoa. Kusiwepo na ndoa za shuruti kama njia ya kuwaongoa baadhi ya watu kufuata dini ambayo ni kinyume cha dhamiri nyofu ya mtu. Ulimwengu mamboleo unawahitaji wajenzi wa amani jamii duniani. Huu ni mwaliko kwa waamini kuendelea kuwa ni vyombo na wajenzi amani. Ni katika muktadha wa majadiliano ya kidini huko Senegal kati ya tarehe 7 hadi 8 Aprili 2025 kumefanyika mkutano wa majadiliano ya kidini, nchini Senegal kwa kunogeshwa na kauli mbiu “Diplomasia ya kidini;” na kwamba, Senegal ni mfano bora wa diplomasia ya kidini ambapo waamini wa dini mbalimbali wanaweza kuishi kwa pamoja. Kimsingi dini ni mdaua mkubwa katika kujenga na kudumisha misingi ya haki, amani, ustawi na maendeleo ya wengi. Haya yamo katika ujumbe ulioandikwa na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa kwa washiriki wa Mkutano wa Kimataifa ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Cheik Anta Diop, Dakar, Senegal. Lengo lilikuwa ni kutoa fursa kwa viongozi wa kidini nchini Senegal kuchangia katika mchakato wa ujenzi wa amani na usuluhishi wa migogoro.

Majadiliano ya kidini ni sehemu ya vinasaba vya maisha ya Kanisa
Majadiliano ya kidini ni sehemu ya vinasaba vya maisha ya Kanisa

Mkutano huu umewashirikisha mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao huko Senegal. Mada ya Diplomasia ya Kidini imekuja kwa wakati muafaka, wakati ambapo dini mbalimbali zinajielekeza katika kulinda, kukuza na kudumisha amani duniani. Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, anasema, amani, utulivu na maridhiano ni muhimu sana kama sehemu ya ujenzi wa jamii inayoheshimiana na kuthamiana. Amewashukuru na kuwapongeza viongozi dini walioshiriki katika mkutano huu. Kimekuwa ni kipindi cha furaha. Amana na utajiri uliojionesha wakati wa Mkutano huu unapaswa kulindwa na kudumishwa. Majadiliano ya diplomasia ya amani kwa kawaida yanagusa: akili na nyoyo za watu. Mkutano huu utazaa matunda yanayo kusudiwa kwa wakati wake.

Majadiliano ya kidini
11 Aprili 2025, 14:56