Tafuta

Shule  ya watoto wadogo sana(asilo nido) "Mtakatifu Francis na Clara" ndani ya kuta za Vatican,itazinduliwa Aprili 14. Shule ya watoto wadogo sana(asilo nido) "Mtakatifu Francis na Clara" ndani ya kuta za Vatican,itazinduliwa Aprili 14. 

Uzinduzi wa shule ya watoto wadogo ya Mtakatifu Francis na Clara ndani kuta za Vatican!

Kwa mara ya kwanza kuta za mji wa Vatican zitakaribisha kituo cha watoto wadogo (Asilo Nido)wa wafanyakazi kitakachozinduliwa tarehe 14 Aprili 2025.

Vatican News

Shule mpya ya kwanza ya watoto wadogo sana (Asilo Nido) iitwayo Mtakatifu Francis na Clara” ndani ya Kuta za Vatican itazinduliwa Jumatatu tarehe 14 Aprili 2025 saa 11.00 jioni masaa ya Ulaya, ikiwa ni saa 12.00 jioni masaa ya Afrika Mashariki na Kati. Majengo hayo ya kituo kipya cha Watoto wadogo yatabarikiwa na Kardinali Fernando Vérgez Alzaga, Gavana Mstaafu wa mji wa Vatican. Miongoni mwa wengine, washiriki watakuwa ni Sr. Raffaella Petrini, Gavana mpya wa mji wa Vatican pamoja na Makatibu Wakuu wawili, Askofu Mkuu Emilio Nappa, na wakili Giuseppe Puglisi-Alibrandi, na Padre  Franco Fontana, Mratibu wa Kikanisa cha Kurugenzi na Ofisi Kuu.

Aatakaye zindua kituo cha Watoto wadogo sana Vatican atakuwa ni Kardinali Alzaga
Aatakaye zindua kituo cha Watoto wadogo sana Vatican atakuwa ni Kardinali Alzaga

Kwa kuhamasishwa na Gavana wa mji wa Vatican, kituo hiki kipya kinahudumia watoto wa wafanyakazi wa Vatican, hasa familia zilizo na watoto kati ya umri wa miezi 3 na 36. Watoto wadogo watapata mazingira ya kujitolea ya kuwakaribisha, na vifaa vya shughuli za elimu na kijamii. Kwa uwezo wao, kuna timu ya elimu ya kuwasindikiza kwenye njia yao ya ukuaji, kukuza maarifa na kubadilishana uzoefu. Ofa hii ya elimu na burudani itafanyika, kuanzia  Jumatatu hadi Ijumaa, saa 1.30 asubuhi masaa ya Ulaya hadi saa 12.30, jioni masaa ya Ulaya kwa kutumia lugha mbili ya Kiitaliano na Kiingereza.

Shule ya watoto wadogo mjini Vatican itafunguliwa
08 Aprili 2025, 12:23