Mkutano wa XVI wa Baraza la Kawaida la Sekretarieti ya Sinodi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Jumatatu, tarehe 7 Aprili 2025, Mkutano wa XVI wa Baraza la Kawaida la Sekretarieti ya Sinodi umefanyika mjini Vatican. Kitovu cha Mkutano huo kilikuwa ni mchakato wa usindikizwaji na wa tathimini ya hatua ya uwajibakaji wa Sinodi, katika “mpango kazi ambao, Baraza hilo lilipendekeza kwa Baba Mtakatifu kabla ya Mkutano wake wa mwisho wa trehe(10.02.2025) na ambapo Baba Mtakatifu aliuridhia katikati ya mwezi Machi 2025(rej. taarifa ya vyombo vya habari tarehe 15.03.2025).
Kuombea Papa
Baada ya muda wa sala, iliyoongozwa na Padre Matteo Ferrari, OSB Cam, mahali ambapo washiriki hapo walisali hata kwa ajili ya afya ya Baba Mtakatifu, wajumbe wa Baraza hilo walianza tafakari katika mtazamo wa Hati ya usindikizaji na tathimini kwa ajili ya ‘hatua ya uwajibikaji’, ambayo inatarajiwa kuchapishwa mwishoni mwa mwezi Mei 2025. Shughuli ambazo zimeunganishwa na Jubilei ya kikundi cha Kisinodi(24-26 Oktoba 2025) zilikuwa pia ni mada ambazo zilijadiliwa. Mkutano uliongoza na Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu.
Mkutano ujao ni katikati ya Mei kuhusu:rasimu ya Hati ya kusaidia hatua ya Uwajibikaji baada ya Sinodi
Katika mkutano huo washiriki walimpongeza Kardinali Jean-Marc Aveline kwa ajili ya kuteuliwa kuwa Rais Baraza la Maaskofu wa Ufaransa. Mkutano ujao wa Baraza la Kawaida utafanyika katikati ya mwezi Mei 2025 kwa ajili ya kujadili rasimu ya Hati ya Kusaidia hatua ya uwajibikaji baada ya Sinodi.