Buriani kwa Francisko na kurasa za Injili zilizobembelezwa na upepo
Andrea Tornielli
Kama ilivyotokea tarehe 8 Aprili 2005, miaka ishirini iliyopita, kwa ajili ya Karol Wojtyła, Papa Mtakatifu aliyefariki katika mkesha wa Dominika ya Huruma ya Mungu, ndivyo ilivyokuwa kwa Jorge Mario Bergoglio, Papa ambaye aliyepokea salamu za juu katika mkesha huo wa Dominika: jeneza la mti likiwa katika jukwaa la Uwanja wa moyo wa ulimwengu na upepo ambao kwa tararibu ulifunua kurasa za Injili. Katika siku ya Papa Francisko ilikuwa ni Jumamosi ya jua ambalo limekuwa buriani ya kusisimua, ya kina, ya walishiriki, ambapo sala na umoja vilitawala.
Watu wa Mungu ambao katika Dominika ya Pasaka, walikuwa wamemkumbatia bila kujua kuwa ilikuwa ni mara yake ya mwisho, ambapo leo wamemsindikiza tena kwa upendo katika hatua yake ya mwisho wa safari ya hapa duniani. Na kati ya wale waliokusanyika kumzunguka walikuwa wenye mamlaka duniani, lakini pia vijana wengi ambao walikuwa na ratiba ya safari ya Jubilei ya vijana wadogo. Na pamoja na wawakilishi wengi wa madhehebu mengine ya Kikristo na dini mbalimbali, waliokusanyika karibu naye. Wote wakiunganisha kumpatia buriani mchungaji mwaminifu wa Injili, ambaye alitumia maisha yake kuhubiri udugu na hata akiwa kitandani hospitalini alipaza zauti akisema hapana kufanya vita.
Hatua mbili kwa namna ya pekee zilipigiwa makofi sana kwa Kardinali Giovanni Battista Re wakati wa mahubiri yake. Ya kwanza ilikuwa ile ambayo alikumbusha msimamo wa uongozi wa Papa Francisko ambao ulikuwa ni: “Kuamini Kanisa ambalo ni nyumbani kwa wote; nyumba yenye milango iliyo wazi daima.” Wakati wa Siku ya Vijana duniani, (WYD), Askofu wa Roma alikuwa alirudia mara nyingi akisema: “Todos, todos, todos”, kwa kueleza jinsi gani, hakuna chochote kinachoweza kututengenisha na upendo wa Mungu daima katika matazamio ya mkumbatio wa wazi wa kumkaribisha kila mtu hata katika hali yetu.
Katika nyumba yenye milango wazi ni Kanisa ambalo Papa Francisko alitafuta kulijenga, kwa kupendelea zaidi walio wa mwisho, maskini, wanyenyekevu na wadhambi. Watu wa mwisho amba leo hii wamempokea katika kizingiti cha Basilika ya Mtakatifu Maria mkuu kabla ya kufika mwisho wa mtazamo wa Picha ya Maria Salus Populi Romani-Maria Afya ya waroma. Lakini pia waamini ambao wamemshangilia hata na zaidi katika hatua ambayo Kardinali Re alimkumbuka Papa katika kuombea amani bila kuchoka na mwaliko wa busara wa kuwa na: "mazungumzo ya uaminifu ili kutafuta suluhisho zinazowezekana, kwa sababu vita - alisema - ni vifo vya watu tu, uharibifu wa nyumba, uharibifu wa hospitali na shule. Vita daima huacha -kwa husema - ulimwengu mbaya zaidi kuliko ulivyokuwa hapo awali na daima ni kushindwa kwa uchungu na kusikitisha kwa kila mtu."
Kabla ya ibada ya mazishi kuanza, marais wawili wa Marekani na Ukraine, walikutana kwa dakika kadhaa. Ni matarajio na kuombwa kwamba chochote kilicho chanya kinaweza kuzaliwa kutokana na mabadilishano hayo mazungumzo ya amani muafaka kutoka kwa Mfuasi wa Petro akiwa wa kwanza alipenda kujiita kama mtakatifu wa Assisi, mtakatifu wa amani.