Wa mwisho katika Injili watakuwa ndiyo wa mwisho kumpokea
Andrea Tornielli
Ndivyo hivyo wa“mwisho”watakuwa wa mwisho kumpokea, kwenye kizingiti cha Basilika ya Mtakatifu Maria Mkuu ambayo inatunza picha ya Salus Populi Romani chini ya mtazamo wa kimama, mahali ambapo Papa Francisko atazikwa. Katika sehemu ya mwisho wa safari yake duniani kama Askofu wa Roma aliyekuja karibu kutoka mwisho wa dunia, atazungukwa si tu na wenye nguvu bali na maskini, wahamiaji, wasio na makao, waliotengwa ambao wamewekwa katikati ya kurasa nyingi za mafundisho yake na ambao wako katikati ya kila ukurasa wa Injili.
Tayari katika maneno yaliyotamkwa asubuhi ya Pasaka ya Jumatatu iitwayo ya Malaika, na Kardinali camerlengo Kevin Joseph Farrell wakati wa kutamka kifo kisichotarajiwa cha Papa Francisko alikuwa amesisitiza kuhusu hili msingi wa mafundisho yake kwamba “alitufundisha kuishi thamani ya Injili kwa imani, ujasiri na upendo wa ulimwengu kwa namna ya pekee kwa walio maskini zaidi na waliiobaguliwa.” “Ni kwa jinsi gani ninataka Kanisa maskini na kwa ajili ya maskini” alikuwa amesema, mwanzoni mwa upapa wake. “Kwa kanisa, upendeleo wa maskini ni kategoria ya kitaalimungu kabla ya utamaduni, sosholojia, siasa au falsa. Mungu anawapa wao, huruma yake ya kwanza.”
Upendeleo huo wa kimungu, una matokeo yake yanayasindikizwa na ishara na chaguzi za dhati. Alikuwa Papa wa kwanza kuchagua jina la mtakatifu wa Asisi ambaye amejikita ndani ya njia ya mafundisho ya watanguli wake, kama yale ya Mtakatifu Yohane XXIII, ambaye mwezi mmoja kabla ya kufungua Mtaguso wa II wa kiekumene alikuwa amesema: Kanisa lijiwakilishe jinsi lilivyo na linataka kuwa kama Kanisa la wote na kwa namna ya pekee Kanisa la Maskini.” Hayo ndiyo mafundisho ya maneno na ishara, kwa ajili ya Papa wa kwanza kutoka Amerika Kusini na ambayo yalikuwa ni asili katika Injili na katika mafundisho ya mababa wa kwanza wa Kanisa.
Kama Mtakatifu Ambrose ambaye alikuwa akithibitisha kuwa: Sio katika mali yako unawapa maskini; unamrudishia tu kilicho chake. Kwa sababi ni ile inayotolewa kwa pamoja kwa matumizi ya wote uinayomtambulisha. Dunia imetolewa kwa kila mtu, na sio kwa matajiri tu." Shukrani kwa maneno haya ya Mtakatifu Paulo VI alikuwa ameweza kuthibitisha katika Waraka wa Kitume wa “Populorum progressio”, kwamba mali binafsi haijumuishi haki isiyo na masharti na kamilifu kwa yeyote, na kwamba hakuna mtu aliyeidhinishwa kuweka akiba kwa matumizi yake ya kipekee yale yanayozidi mahitaji yake, wakati wengine wanakosa kile kinachohitajika. Au kama Mtakatifu Yohane Chrisostomu ambaye kwa umaarufu wa mahubiri yake alikuwa amesema:“Unataka kuheshimu mwili wa Kristo? Usiruhusu kuwa kitu cha kudharauliwa kwa wajumbe wake, yaani, katika maskini, bila nguo za kujifunika.”
Usimheshimu Kristo hapa kanisani kwa vitambaa vya hariri, wakati nje unawaacha wanaoteseka kwa baridi na utupu. Yeye aliyesema: Huu ni mwili wangu, piaalisema: mliniona nikiwa na njaa hamkunipatia chakula.” Mbali na uelewa wa kiitikadi, Kanisa halijihusishi na sera za kisiasa zile za kujilinda, wakati huo hu linatoa mwaliko wa kushinda ambao Papa Francisko aliufafanua wa “Ulimwengu wa sintofahamu.” Kwa kuongozwa na maneno ya Injili tu, kwa kusaidiwa na tamaduni ya Mababa wa Kanisa, Papa Francisko alitualika kuelekeza mtazamo kwa walio wa mwisho, na waliopendwa na Yesu. Wale wa mwisho ambao watamsindikiza kwa mkumbatia wa hatua yake ya mwisho katika kizingiti cha Kanisa Kuu la Mtakatifu maria Mkuu.